Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

Hon. Riziki Saidi Lulida

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana na nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyenijaalia kunipatia afya njema na kuwaombea Wabunge wenzangu Mwenyezi Mungu awabariki sana tusimame kwa pamoja tuweze kuwasaidia wakulima ambao wengi wanahangaika na wakiwa katika mazingira magumu ya mafanikio yao. Msimamo wa Wabunge kuwasaidia wakulima utainua uchumi na kumsaidia Rais wetu katika kuleta maendeleo yaliyokuwa ya kweli.

Mheshimiwa Spika, bado ni mtoto ambaye nimezaliwa katika zao la korosho, korosho ndio zao la kwanza toka tumepata uhuru ukichukulia madini tunaweza kupata fedha za kigeni. Kutoka mwaka 1961 tunapata uhuru mpaka mwaka 2017 zao la korosho lilichezewa danadana sana, tulikuwa tunapata haizidi bilioni 141. Lakini mwaka 2017 baada ya kusimamia mifumo na kuona hapa tunapigwa tuliweza kuuza korosho kwa dola milioni 530 tukapata trilioni 1.2 ikaitwa dhahabu ya kijani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii dhahabu ya kijani haikuja hivihivi, ilikuja kwa kusimamiwa; tujiulize kwa nini tuliweza kuleta mafanikio ambayo yalichezewa kwa muda wote pana kundi hapa linacheza na wakulima ambao hawawatakii mema wakulima.

Mheshimiwa Spika, wakulima hawa unaowaona wanapalilia mashamba yao kwa hela yao, wananunua pembejeo kwa hela yao lakini siku ya stakabadhi ghalani mabenki yote yapo pale na wafanyabiashara wote wapo pale wanataka kuhakikisha mkulima huyu kazi aliyoifanya wao wawe wanufaika zaidi kuliko wao, haikubaliki. Huu ni unyonge wametufanyia kwa miaka mingi hatukubali, nataka niwe mkweli na ni mzalendo wa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna lugha wanazungumza wafanyabiashara wanaonewa, sikubali kama wafanyabiashara wanaonewa, wanaoonewa katika kilimo ni wakulima sio mfanyabiashara. Kama tuliwezanyonywa kuhakikisha tunapata bilioni 141 zaidi vis-a-vis ya trilioni 1.2, nani alimuibia mwenzake hapa? Aliyeibiwa hapa ni mkulima. Watanzania tufunguke, hali ya uchumi wetu tunaweza kuusimamia na tukaweza kutoka hapa, tuache longolongo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, viwanda, biashara na kilimo vinakwenda sambamba; leo enzi ya Mwalimu alitengeneza mifumo ambayo tungeenda nayo mpaka sasa hivi tungeruka. Mikoa yote inayolima korosho tulikuwa na viwanda, viwanda vyote vimefungwa mpaka leo hatujui mwisho wake ni nini. Tumemnyima ajira Mmakonde, Mngoni, Myao na mtu wa Liwale kwa ajili ya uhuni wa kibiashara halafu mnasema wanaonewa,nani anamuonea? Tuachane na lugha ambazo zinatufanya tuna- paralyze katika akili na mifumo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumeonewa sana katika kilimo halafu bado wameonewa, wameonewa; amemuonea nani, wao walizoea kutuonea. Korosho ilikuwa inauzwa shilingi 600 lakini ghafla mwaka 2017 korosho iliuzwa 3200, nani alikuwa anamuonea mwenzake? Na hiyo 600 kuipata kamilifu haiwezekani, tukapata hela ya mfuko. Mfuko wa kwanza ilikuwa bilioni 97 macho yalianzia hapo, baada ya kuona bilioni 97 pakaleta siasa za uongo na vitu mbalimbali ambavyo vilifanya zile hela hazikumsaidia tena mkulima, korosho imeanguka chini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mikoa iligawanyika kwa ajili ya mazao yanayolima, kahawa Kilimanjaro, Kagera na Mbeya, korosho Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani tuendeleze hapa kwanza na mikoa ya Tanga ya Pwani ambayo hali ya hewa yao inakwenda sambamba na korosho. Leo tumeitoa korosho tukapeleka sehemu ya baridi unafikiri korosho inastawi, haistawi, itaota lakini haitakuwa na yield ya kutosha. Sasa hela zikagawanyishwa peleka huku, peleka huku matokeo yake mkulima wa korosho aliyesafisha shamba na kutafuta pembejeo yeye mwenyewe inapatikana hela hana thamani tena, hela ya mfuko inapelekwa sehemu zingine mkulima wa korosho ameachwa anahangaika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nililizungumza viwanda vilifungwa makusudi na wawekezaji na wawekezaji wapo humu ndani ni wafanyabiashara, wamevifunga mpaka leo havifanyi kazi maana yake hakuna ajira kusini. Tuambieni kusini kuna kiwanda gani, Mkoa wa Lindi, Mtwara na Ruvuma hakuna viwanda nenda Tunduru viwanda vimefungwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili achukue ile korosho anaipeleka nje kama as a raw material, malighafi na kule anapopeleka anasimamia kwa viwanda vya kule vitafanya kazi na itatoa ajira kwa watu wa kule sio kwa ajili ya mtu wa kusini. Tujiulize tunafanya nini, Watanzania tunasomesha vijana wana degree mbalimbali za kilimo lakini unaona bado tunahangaika na kilimo.

Mheshimiwa Spika, tunaomba viwanda vya korosho vifunguliwe tupate ajira ili matatizo ya kutaka korosho ile kuipeleka nje wanaotufanyia baadhi ya wafanyabiashara korosho ya Tanzania italiwa na Mtanzania humuhumu ndani na brand itatoka Tanzania. Leo brand ya korosho inatoka Sri Lanka wewe hujawahi kusikia vitu kama hivi; kahawa ya Tanzania inakuwa branded Uganda, parachichi la Njombe linakuwa branded Kenya, tuko wapi? Unaletewa wataalam wa shamba shape kuja kutusaidia kutoka Kenya, hivi hatuna vijana tuliowasomesha wanaojua suala la kilimo, tume- paralyze. Na kama hatujifungui kwa hilo nakwambia tutaendelea kupiga kelele na siasa ambazo hazitamsaidia mkulima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mkulima anahitaji akombolewe, tulijua kuanzia mwaka 2017 tumeshatatua tatizo la korosho tungekwenda kwenye kahawa lakini leo kahawa ya watu wa Bukoba inauzwa Rwanda na Rwanda wanapata uchumi kwa kupitia mazao ya Tanzania, sisi wenyewe tupo wapi? Tunasema tuna asilimia 29, haiwezekani, hii ni asilimia ndogo sana sio ya kuridhika na kufurahia nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ufuta; zao la ufuta la piliā€¦

SPIKA: Mheshimiwa Riziki muda haupo upande wako.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naunga mkono hoja. (Makofi)