Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwanza niungane na mzungumzaji aliyepita kuhusiana na mchango wa teknolojia na ukuaji wa teknohama katika ulimwengu. Pia, sisi kama Taifa, kama sehemu katika ulimwengu miongoni mwa washiriki katika maendeleo makubwa sana ya sayansi na teknolojia, hatuwezi kuishi kama kisiwa. Kwa hiyo, ni lazima kama nchi kwa pamoja tukubaliane kwamba tunapozungumza uchumi wa kidijitali, digital economy kwanza siyo terminology mpya, siyo neno jipya, pia siyo myth, yaani ni kitu ambacho kinaishi na kinafanyika kwa sababu nchi za wenzetu duniani sasa hivi wanazungumza kuhusu digital economy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunazungumzia digital economy au uchumi wa kidijitali, hatuwezi kumaliza bila kuzungumzia miundombinu. Kwa hiyo, tunapongeza jitihada kwa sababu kimsingi sisi kama nchi mkiangalia hata namna ya utekelezaji wa mambo yetu, bado tuko kwenye makabrasha sana. Ndiyo maana hata Bunge hili ni miaka michache tu iliyopita ndiyo tumeingia kwenye teknolojia, hata tunatumia vishikwambi sasa hivi. Tuna mabunge mawili nafikiri ndiyo tumeanza kutumia vishikwambi. Kwa hiyo, maana yake ni lazima pia tukubali kwamba tulikuwa somewhere behind kwa sababu dunia ilishakwenda huko ambako sisi tuna-struggle kwenda ama tuko sasa hivi tunapambana kufika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napongeza kwa namna yao Wizara na Serikali kwa upande fulani wamejitahidi sana, kwa sababu mpaka sasa hivi wameshaunganisha Makao Makuu ya Mikoa 26 na Wilaya 42. Wamejitahidi, tunakwenda kwa maana ya connectivity, kwenye miundombinu ya kusaidia Watanzania kufikiwa na huduma za kimtandao. Pamoja na hayo, bado tuna changamoto kubwa sana, kwa sababu wananchi asilimia 68 maeneo wanayoishi wana uwezo wa kupata huduma za mtandao (internet), lakini ni asilimia 26 tu ndio ambao wanaweza kufikia (access) kupata huduma ya mtandao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua mpaka uwe na simu janja ndiyo unaweza ukatumia internet. Kwa hiyo, ni asilimia 26 tu. Wakati Serikali inajaribu kuweka miundombinu na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ya kimtandao, bado wananchi wetu sisi kufikia kumiliki vifaa vyenye uwezo wa ku-access internet, bado ni asilimia ndogo sana. Kwa hiyo, hii inatuelekeza kwamba hata tunavyozungumza digital economy bado kuna sehemu tuko nyuma. Kwa sababu ili tuweze ku-access digital economy ni lazima wananchi wetu wawe wana vifaa vyenye uwezo wa kutumia hizo internet ambazo tunazizungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mtu anafahamu kwamba simu janja gharama yake ni kubwa mno. Kwa hiyo, wananchi wengi unakuta wana simu ndogo tu ya kutumia, lakini kupata kifaa au kupata simu ambayo inaweza kumpa access ya kuweza kutumia internet, wengi bado hawana uwezo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa Wizara na Serikali kwa namna yao waangalie namna gani wanaweza wakapunguza gharama ya vifaa hivi vyenye uwezo wa ku- access internet ili wananchi wetu wengi waweze ku-access internet, waweze kupata taarifa nyingi sana ambazo zinapatikana kwenye mitandao na faida kubwa inayopatikana kwenye suala zima la digital economy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hata wale ambao wana vifaa vyenye uwezo wa ku-access internet, bado kuna gharama kubwa sana za data ambazo zinasababisha hata Serikali ikose mapato kwenye kiwango ambacho ilistahili kupata. Mpaka sasa kuna ongezeko kubwa sana la matumizi ya data asilimia 35, lakini Serikali inapata asilimia 16 tu kwenye pato la Taifa kutokana na matumizi ya data. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba najua kuna Tume inaitwa Tume ya TEHAMA, nafikiri miongoni mwa jukumu ambalo naweza kushauri, waongezewe, wapewe uwezekano wa ku-regulate, kuhakikisha kwamba makampuni ya simu yenye kupewa jukumu na TTCL kwa ajili ya kusaidia wananchi kupata internet, waweze ku-regulate. Kwa sababu unaweza kujiuliza kwa nini data ni asilimia 35, lakini asilimia 16 tu ndiyo tunayochangia kwenye pato la Taifa. Maana yake kuna tofauti katika utoaji wa huduma za data. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maana yake ile Tume sasa ya TEHAMA itusaidie kuwa na segment at least ya kushauri na kuangalia namna wanaweza ku-regulate ili bei zisiwe tofauti sana. Kwa sababu, pamoja na kwamba ni huduma, tunajua pia wanafanya biashara, lakini isifike hatua kwamba wanawaumiza wananchi, wanashindwa ku-access.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hili nami nina direct interest kwenye upande wa vijana, kwa sababu, ni ukweli usiopingika kwamba watumiaji wengi wa mitandao ni vijana. Mheshimiwa Jenista Mhagama anajua tatizo kubwa la ajira nchini, pengine vijana wengi wangekuwa na uwezo wa ku- access internet kwenye vifaa pamoja na data, wangekuwa na uwezo mkubwa pia hata wa kujiajiri. Nitakwenda moja kwa moja kwenye namna ambavyo kama Taifa, kama vijana tunaweza kupunguza tatizo la ajira na kusaidia vijana wetu kwenye kujiajiri na tukaishi kwa vitendo katika digital economy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mtu sasa hivi anafuatilia kwenye mitandao anaona kuna debate kubwa kuhusiana na namna ambavyo wasanii wetu wanatengeneza pesa kwenye viewers you tube. Tunaishi kwenye ulimwengu ambao ni tofauti sana, inawezekana vitu vingine watu wakashangaa kabisa. Ukiwa na viewers milioni moja katika YouTube una uwezo wa kupata USD 5,000. That is money na hauhitaji subscribers; unahitaji u-post content You Tube ili watu waka-view content yako ili you tube waweke matangazo kwenye channel yako upate pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa vijana wengi sasa hivi hawaelewi hiki kitu ndio maana mpaka sasa hivi wana-discuss kwamba, inawezekana kweli watu wanatengeneza viewers YouTube; kwamba Diamond katoa nyimbo siku mbili tu ina viewers milioni 10! That is money, that is money. Yaani hiyo ni pesa, kwasababu, YouTube wanaweka matangazo yao kwenye ile video. Wakishaweka hayo matangazo yao, wewe wanakulipa pesa.

Mheshimwia Mwenyekiti, mwaka 2018 kuna kijana mdogo wa miaka saba anaitwa Riyans’ Toys Review, ana- post midoli; ndio alikuwa anaongoza YouTube, analipwa milioni 22 USD. Sasa hivi nafikiri ana miaka 12 ama 10 hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tuna Jeffry Star analipwa dola milioni 200 net worth yake na alikuwa ame-bankrupt kabisa. Huyu content yake anatangaza bidhaa za urembo. Actually ni mwanaume, lakini anafanya mambo ya entertainments. Kwa hiyo, ana bidhaa za make up, anaimba music. Kwa hiyo, ana-post YouTube halafu anatengeneza subscribers.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna robots wanatengeneza subscribers YouTube. Wale subscribers wanakusaidia kuita watu waka-view content yako YouTube. Waki-view content yako YouTube wewe unapata pesa kwa sababu YouTube wanaweka tangazo kwenye account yako na you get paid, lakini kuna procedure za kufuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wengi wa Kitanzania hawajui kwamba you can get paid by just posting your content. Hata Wizara ya Maliasili na Utalii…

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumpa taarifa tu mzungumzaji kwamba anachosema ni kweli asilimia 100. Wasanii wetu wa Tanzania hawajui ku-monetize, kugeuza viewers wao kupata fedha, matokeo yao wanafanyiwa na Wakenya. Kwa hiyo, fedha zinaenda Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa taarifa tu mzungumzaji. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya Mheshimiwa Nusrat, taarifa hiyo umeipokea?

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeipokea. Tuseme tu kwenye hilo, hata Kiswahili, Wanaijeria wananunua online vitabu vya kufundisha a, e, i, o, u Dar es Salaam kwa shilingi 500/= wanaenda kufundisha watu Kiswahili YouTube na they get paid for that, nasi tumezaliwa na Kiswahili na tunakuwa nacho na tunakiangalia. We don’t know how to get money on it. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitoe kama changamoto; kwanza kwenye uwasilishaji wa juzi wa TCRA, Mheshimiwa Waziri na watu wako wa TCRA kweli mmeleta wasilisho zuri. Kwenye issue ya maudhui, pamoja na capacity building mnahitaji kufanya capacity building kwa vijana wengi ili tuache sasa, tutoke kwenye ku-complain watu waende waweke content. Kwa sababu, hawa waliotengeneza hizi pesa kwanza wengi ni watu ambao hawana hata kazi rasmi, ni watu wanaoishi tu nyumbani, unahitaji tu kuwa full time YouTube, unahitaji tu kuwa na kitu cha ku-post, kwa sababu money is the reward after solving somebody’s problem. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tajiri namba mbili anayelipwa pesa nyingi YouTube, ana-post video games, yeye ndio anacheza games; zile play station, anaji-record reaction yake wakati anacheza na ana-post na watu wanakuwa inspired, wanakwenda ku-view. Sasa hiyo ni pesa. Watu wa utalii wanahitaji kutangaza utalii. Sisi kama nchi tunahitaji kutangaza, lakini sijui kama Wizara ya Utalii wana YouTube Channel. We need YouTube Channel for that. Tunahitaji kuwa na YouTube Channel kutangaza nchi yetu. (Makofi/Kicheko)

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Taarifa, Mheshimiwa Shangazi.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda tu kumpa taarifa Mheshimiwa Nusrat kwa mchango wake mzuri kwa vijana wetu, lakini nimwambie tu kwamba kwa hapa Tanzania mwanamuziki Nassib Abdul Diamond Platnum analipwa kuanzia kati ya dola 75,000 mpaka 100,000 kupitia YouTube. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya Mheshimiwa Nusrat, taarifa hiyo.

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea kwa maana ya nia njema ila namshauri pia Mheshimiwa Shangazi akaangalie vizuri kwa sababu hii ni updated na Diamond hayuko kwenye list. Hata hivyo is a good thing, kwa sababu kama anaweza aka-hit viewers wengi kwenye muda mfupi sana, maana hiyo ni opportunity kubwa sana.

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Ehe taarifa.

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, anachokisema Mheshimiwa Nusrat ni sahihi kabisa. Regulator wa YouTube yuko Kenya, kwa hiyo, anatujengea hoja kwamba tunapoteza mapato mengi kwa sababu regulator wa YouTube Tanzania kwa hao wanaolipwa yuko Kenya. Kwa hiyo, tunatakiwa tuwe na regulator wetu sisi hapa Tanzania. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya Mheshimiwa Nusrat na Mheshimiwa Waziri, umelisikia hilo? Endelea Mheshimiwa Nusrat.

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru maana yake kama Wizara wanaona sasa kuna kazi ya kufanya. Lazima tuweke nguvu, tuweke teknolojia, tuweke utaalam, watu wakafanye tafiti watuletee ili tuone namna gani tutatengeneza pesa. Siyo tu kuweka miundombinu, tukajenge minara, hatuwezi kuishia kuzungumza minara, lazima tuzungumze tunanufaika vipi na hivi vitu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo yote, ili hivi vitu vyote tufanikiwe kwa sababu tunazungumza faida tutakayoipata baada ya miundombinu kukaa sawa, hatuwezi pia kuacha kuwa-recognise TTCL ambao mpaka sasa hivi wanaidai Wizara Dola za Kimarekani milioni 68. Kwa kweli mnawakwamisha sana TTCL, kwa sababu tunawategemea, ndiyo wanaosimamia, wanatumia mapato yao ya ndani kuendesha mfumo mzima na kuhakikisha kwamba Mkongo wa Taifa unafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunategemea hawa ndio wafike, kwa sababu tunaweza tukawa tuna ideas nzuri kweli watu wanapewa mafunzo waende waka-monetize YouTube Channels zao wapate pesa, lakini kama hatuna connectivity, hatuna miundombinu na hawana access ya kutumia internet bado tutakuwa tuko nyuma sana, bado tutakuwa tuna lag behind.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja la mwisho, pamoja na kwamba tumeweka kwenye data kwamba watu inabidi walipe ili kununua data wa-access internet, lakini kama Wizara tunaomba mwangalie upya kwenye machapisho ya kielimu na kwenye document za Kiserikali, hebu waondoe cost za downloading.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanahitaji kupata information. Sasa ili ni-download kitabu ambacho kitanisaidia kupata maarifa ambacho pengine mwalimu anaenda kufundishia au mwanafunzi anajifundishia; wanafunzi wa vyuo vikuu mnajua, kuna amount unapata darasani na kuna amount unaenda kutafuta mwenyewe. Wako kwenye internet wanatafuta materials. Sasa kuna vitu vya msingi kama hivyo ambavyo tunaomba mwondoe downloading cost ili waweze ku-access kwa sababu ni muhimu kwao. (Makofi)