Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Hon. Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na niweze...

NAIBU SPIKA: Utafatiwa na Mheshimiwa Mwanaidi Hamis.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, niweze kutoa mchango wangu katika Wizara hii ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze jambo la kwanza kuhusiana na kampeni ya usafi wa mazingira kitaifa, kampeni hii ililkuwa inafanywa na wadau muhimu ambao walikuwa na slogan yao ya nyumba ni choo. Mradi huu uliendeshwa kwa kuijenga jamii kuelewa namna bora ya kuwa na vyoo bora lakini kunawa mikono na kuhakikisha kwamba wanakuwa na vyoo vinavyotumika kwenye kila kaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kampeni hii ilikuwa ina ufanisi mkubwa sana kwasababu imezunguka kwenye mikoa 18 na matokeo yake ni kuongezeka kwa kaya zenye vyoo bora kutoka asilimia 39 mwaka 2017 hadi asilimia 67 mwaka 2021. Haya ni mafanikio makubwa, lakini pia kampeni hii inasaidia mwisho wa siku kuibadili jamii kitabia na kimienendo lakini inasaidia kuweka kinga kwenye jamii ili kusiwepo na magonjwa mbalimbali ya maambukizi ambayo yanatokana na ukosefu wa vyoo katika maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi ni vyema Wizara natambua mradi huu unaisha na mradi huu ulikuwa funded na Wizara basi ni vema Wizara ikaendelea kuwekeza kwenye kampeni hii ambayo itaendelea kuisaidia jamii kujiandaa kukabiliana na magonjwa mbalimbali lakini kuwa na vyoo bora kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni hii mwisho wa siku inasaidia hata katika magonjwa mbalimbali ya milipuko kama Corona na mengine ambayo hatujui kama yatakuja au hayaji kuisaidia jamii kuiandaa katika ustawi bora Zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili kuna hii dawa ya Phyt Exponent, ninaushahidi imesaidia kwa mtu ambaye alikuwa anaumwa corona lakini wako wengine ambao walikuwa wanaumwa kansa imeonyesha matokeo bora na mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa dawa hii ni ghali na upatikanaji wake kwa watu wa kawaida siyo rahisi inauzwa 150,000 sababu za kuuzwa 150,000 kwasababu haijasajiliwa kama dawa tunaiomba Wizara kwasababu imeshathibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, na imeshaonyesha matokeo na hata hivyo mtu anapougua mwisho wa siku imani ya mtu kutokana na anachokitumia kinasaidia kuponya, watu wanaimani na hii basi tunaomba Wizara isajili hii diet Supplement ili iweze kupatikana kwa urahisi na kwa unafuu na iweze kusaidia jamii yetu kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu, ni Idara ya Maendeleo ya Jamii Idara hii ya Maendeleo ya Jamii ina watu wa Ustawi wa Jamii na Watu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii. Watu wa Ustawi wa Jamii ni muhimu sana kwenye jamii yetu na watu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu sana kwenye jamii yetu kwasababu inaiandaa jamii kukabiliana na changamoto mbalimbali lakini inaleta chachu ya maendeleo katika jamii kwa kuihamasisha jamii. Lakini Idara hii sina hakika kama Wizara na Serikali kwa ujumla mnaona umuhimu wa Idara hii na kuhakikisha kwamba kunakuwa na rasilimali watu wa kutosha katika idara hii ili isaidie jamii kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mahitaji ya watu ustawi wa jamii ni 22,000 lakini walioajiriwa ni watu 744 kwa hiyo kuna ajira iliyotolewa walioko kazini Maafisa Ustawi wa Jamii ni asilimia 3.2 ya uhitaji wote wa nchi nzima hiki ni kiwango kidogo kabisa. Ni vema Serikali ikaweka umuhimu kwa kuhakikisha tunaajiri maafisa ustawi wa jamii wa kutosha hawa maafisa ustawi wa jamii wa kutosha wakipatikana ndivyo ambavyo tutaijenga jamiii yetu kimaadili tutachochea maendeleo, tutahakikisha ukatili tunaouongelea kila siku ukatili wa watoto, ukatili wa kijinsia, mambo mengi yanayoendelea katika jamii yetu kama tuna watu kama hawa wa kutosha kwenye halmashauri zetu tutahakikisha tunakuwa na jamii yenye ustawi yenye amani yenye kuwa na maendeleo ambayo tunayahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie hoja yangu ya mwisho upungufu wa watumishi katika sekta ya afya, takwimu zinaonyesha kuna upungufu wa watumishi wa afya ni asilimia 53 sasa kama tutakuwa tunajivunia tunajenga zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya tunaimarisha hospitali za kanda tutabakiwa na majengo yasiyokuwa na watumishi wa kutoa huduma muhimu za afya kwa watu wetu. Tunataka Serikali muwe na mpango sambamba mpango wa kujenga zahanati zetu vituo vya afya na hospitali za wilaya uendane na mpango wa kukajiri watumishi kuhakikisha watumishi wanapatikana wakutosha watanzania wanatamani kupata huduma iliyobora ya kutosheleza na ya uhakika kwa kuwa na watumishi wa afya wakutosha ahsante sana. (Makofi)