Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji

Hon. Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niungane na wenzangu kuweza kuchangia. Kwanza nianze kwa kumpongeza sana Waziri pamoja na Naibu Waziri na Katibu Mkuu na Manaibu pamoja na Wizara nzima kwa kazi nzuri wanayowatendea haki Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimpongeze Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaamini hawa ambao wanawatendea Watanzania wanakwenda kwa kasi. Nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na miradi kadhaa ya maji katika Jimbo la Makambako. Nimeona kwenye bajeti wametutengea fedha, ombi langu Mheshimiwa Waziri na kundi lako, pale Ikelu pana mradi unaoendelea, mkandarasi yuko pale. Ombi langu tunaomba mkandarasi huyu kwasababu amesimama na yuko hatua za mwisho, mumlipe fedha ili aweze kumalizia mradi wananchi wa Ikelu waweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile tuna mkandarasi yuko pale Ibatu. Mkandarasi huyu amesimama kwasababu hamjamlipa fedha. Tunaomba alipwe fedha ili kusudi aendelee kukamilisha ule mradi ili wananchi wa Ibatu waendelee kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna mkandarasi yuko pale Usetule Mahongole, vilevile amesimama. Niombe sana Mheshimiwa Waziri na timu yako tuhakikishe tunawalipa ili wamalizie kwasababu, wamebaki hatua za mwisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mkandarasi wa mwisho yuko pale Nyamande, Mbugani na Mtulingala, Mkandarasi huyu anafanya kazi nzuri, lakini amesimama hawezi kuendelea kwasababu, hajalipwa fedha. Niombe sana aweze kulipwa fedha ili aweze kumalizia kazi iliyokusudiwa wananchi wale waweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini niungane na Wabunge wenzangu, tuna miradi ile ya miji 28. Katika miji 28 ikiwepo na Makambako. Na katika Makambako kuna kata tisa zinazotegemea mradi huu au miradi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba utakapokuwa unahitimisha hapa uwaambie wananchi wa Makambako ni namna gani wana imani kubwa ingawa katika maelezo yako umeeleza vizuri tumepata imani kwamba, mradi huu sasa unakwenda kutekelezwa. Sasa kwenye hitimisho hapa useme ili wananchi wa Makambako waweze kupona; wajue katika kata zao tisa wanazosubiri katika mradi huu mkubwa ni lini mkandarasi atakuwa katika Mji wa Makambako ili wananchi wa Makambako waweze kupata maji? Na wakati huo unapohitimisha na hii niliyoisema ya makandarasi waliosimama nayo useme hapa, ili wananchi wa Makambako wapate imani kama ambavyo ulituambia kwenye kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa leo nilitaka nizungumzie hili ambalo wakandarasi hawajalipwa na hii miradi ambayo ya miji 28. Watu wana imani kubwa sana ya miji hii 28 hasa ukiwepo na Mji wa Makambako ambao wananchi wanausubiri kwa hamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, ahsante sana.
(Makofi)