Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Nami nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Elimu ambaye ni mwalimu wangu wa Research Methodology ingawa ulinibania bania sana.

SPIKA: Mchoyo wa marks eeh!

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, nianze kwa neno moja halafu niendelee. Hilo neno atanisaidia kutafsiri baadaye Mheshimiwa Mwantumu Dau, linasema Iqra. Nami niseme kama walivyosema wenzangu. Mitaala yetu ya elimu ni mizuri, sio mibaya. Tatizo mitaala yetu ya elimu ni mikubwa (loaded) mno. Kwa hiyo, cha kufanya nimshauri tu Mheshimiwa Waziri aunde timu, wafanye in depth review ya program zote na hasa vyo vikuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unakuta leo hii ukianzisha chuo chochote kikuu, mtu anayazoa ma-program ya Chuo Kikuu fulani yote anayaweka kwenye chuo chake. Kwa hiyo, ni copy and paste. Kwa hiyo, tunakuwa na ma-program mengi. Mengine wakati mwingine ndiyo hayo ambayo mtoto akimaliza anakosa ajira. Kwa hiyo, hapa Mheshimiwa waziri ana kazi nzito. Watu wameongea sana kuhusu elimu. Inaonekana tayari kuna tatizo na wakati huu uliopo. Kwa hiyo, waka echini wa-review program ya elimu iwe reviewed in depth ili waje na zile special program ambazo tunazihitaji kwa wakati huu na wakati ujao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine nililizungumza lakini leo nizungumze kuhusu ku-post au kupata wahadhiri kutoka nje. Yaani tunatakiwa sasa tubadilike. Vyuo vikuu vyetu wahadhiri ni wale wa hapa Tanzania, hatukatai lakini tunatakiwa tuwe na angalau asilimia tano ya professors kutoka nje. Tukiwa na mchanganyiko wa professors wengine wakapata kibali cha kutangaza Internationally halafu tukapata wahadhiri kutoka nje kwanza itaongeza hadhi ya vyuo vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni jukumu sasa nimuombe Waziri watangaze kazi Internationally ili tupate maprofesa waweze kusaidiana na hao waliopo na hiyo itasaidia kuongeza exchange programs, itasaidia kuleta projects lakini pia hivi vyuo vyetu vitapanda hadhi. Tukiendelea tu kuwa wenyewe, local, local tu, laizma tufanye sisi wenyewe vile ambavyo leo kuna Watanzania Maprofesa wanaenda kufundisha South Africa, wengine wanaenda kufundisha Rwanda somo la Kiswahili. Kwa hiyo, na sisi lazima tujipange tuwe na wahadhiri kutoka nje. Na hapo ndiyo tutaleta maana ya neno University. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna hili suala la Sheria za Extension. Pale Chuo Kikuu ukichelewa kumaliza program za master’s au PHD unapewa extension na unalipa fine zaidi ya milioni moja. Sasa niombe, wanafunzi wanalalamika sana. Anayesababisha hawa wanafunzi mara nyingi kuchelewa ni yule supervisor. Kwa hiyo, kinachotakiwa hapa ile fine igawanywe. Mwanafunzi alipe nusu na yule supervisor nusu. Kwa kufanya hivyo, hawa ma-supervisor watakuwa wanasoma kazi za wanafunzi, wanamaliza kwa wakati, hakutakuwa na extension fine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakishamaliza mwanafunzi yule anajulikana details zake zote. Siku anamaliza ana-graduate kupata cheti anaambiwa rudi Songea, au nenda Kagera uje baada ya wiki mbili. Hiyo nayo imekuwa inasumbua sana wanafunzi. Mheshimiwa Waziri asimamie. Akimaliza chuo, anapata cheti chake anaondoka. Lakini imekuwa ni usumbufu mno. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho niwaombe sana Wizara pamoja na halmashauri tumekuwa tukilalamika vyuo vikuu hawafanyi utafiti…

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Ntara.

MHE. DKT. THEA M. NTARA: … aaah! Hivi ni kweli?

SPIKA: Haya, nakupa dakika mbili au tatu umalizie. (Kicheko)

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, sasa niwaombe sana Wizara na halmashauri tutumie vyuo vyetu kufanya kazi ndani ya halmashauri na wizara. Mfano mzuri ni Mheshimiwa Sajin alipokuwa RAS Simiyu. Alichukua wale wanafunzi kutoka ardhi Tabora kwenda kupima viwanja vyote kule Simiyu, wakammalizia kazi tena kwa bei ya chini. Kwa hiyo, tutumie vyuo vyetu. Tutumie TIA, IFM, Ardhi, tutumie University of Dar es Salaam, UDOM. Tuwatumie wakafanye kazi zetu. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, Taarifa!

SPIKA: Mheshimiwa Thea Ntara, kuna Taarifa unapewa. Endelea nimekuruhusu.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Nimekuruhusu, jitambulishe tu.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, naitwa Cosato Chumi…

SPIKA: Cosato Chumi, nimekuona sasa.

T A A R I F A

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, naomba kumpa Taarifa Mheshimiwa Mbunge anayezungumza kwamba hata sisi Halmashauri ya Mji wa Mafinga tumetengeneza Master Plan kwa kutumia wanafunzi wa Chuo cha Ardhi kwa hiyo hoja yake ni ya msingi sana. (Makofi)

SPIKA: Unaipokea hiyo hoja Mheshimiwa Ntara?

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, nimeipokea halafu nawapongeza sana. Hiyo ndiyo namna tutakuza hawa watoto wetu waonekane wanafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nikushukuru sana. (Makofi)