Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Wizara hii, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa hotuba nzuri sana ambayo kimsingi jana iliwasilishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sehemu kubwa sana ya baadhi ya hoja ambazo nilitaka kuzizungumza nadhani zimekuwa coverd, kwa hiyo ninawashukuru sana. Lakini ninaomba nizungumzie maeneo machache, la kwanza jana hapa amezungumza Waziri wetu wa TAMISEMI na ameonesha jinsi ambavyo atakwenda kuweka msukumo mkubwa kwenye watumishi waliopo kwenye kada ya TAMISEMI. Lakini nilitaka niongezee na nisisitize eneo moja, niwaombe Waheshimiwa Mawaziri kwenda kutazama vyema mazingira ya ufanyaji kazi ya watumishi ambapo wapo kimsingi kwenye Utumishi na TAMISEMI. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano kupitia ule Waraka wa Elimu Bure sote tulishuhudia jinsi ambavyo tulitoa posho ya madaraka kwa Wakuu wa Shule pamoja na Waratibu wa Elimu Kata, lakini sasa hoja yangu ni nini, niwaomba mkatazame vizuri sana kuhusu watendaji wa kata kwenye nchi hii. Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa hata kwenye vijiji wao ndio viongozi kwenye maeneo yao, Watendaji wa Kata ndio Wakurugenzi kwenye maeneo yao, tumefanya kazi nzuri ya kuwawekea mazingira mazuri ya kazi wenzetu wa elimu na tunao mpango Maafisa wengine wa Ugani lakini bosi ambaye ni Mtendaji wa Kata ana hali gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yeye ndiye anayesimamia madarasa, yeye ndiye anayepeleka taarifa za Kata kwa Mkurugenzi yeye ndiye anayekwenda kusimamia usafi huko, kimsingi hawa ndio wanaofanya kazi kubwa zaidi ya kumwakilisha Mkurugenzi kwenye maeneo yao. (Makofi)

Kwa hiyo hilo ningeomba pia liende sambamba na upande wa Maafisa Tarafa, kada hii huko nyuma kama alivyozungumza mchangiaji mmoja juzi ni kada ambayo kimsingi miongoni mwao ndio tunateua Ma-DAS, tumeteua ma-DED na Ma-DC, lakini changamoto kubwa ipo kuanzia kwenye usafiri ofisi mpaka incentive zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zamani Maafisa Tarafa walikuwa wanapata mishahara ya kiuongozi, baadaye ikaondolewa, ninaishauri sana ikiwezekana tutazame package maalum, maana hawa ndio wawakilishi wa Mkuu wa Wilaya kwenye maeneo yao. Vivyo hivyo kwa ma-DAS katika ofisi zao, utakuta DAS ni kiongozi mkubwa baada ya DC akitoka DAS wanasema anakuja DED, lakini kwa mujibu wa package yake unaambiwa anastahili kupewa gari aina saloon, ni vyema tukahuisha mambo kama haya yaendane sambamba na wakati uliopo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia yapo mambo madogo ninayotaka kuyazungumzia, moja; kuna kitu kinaitwa kupanda cheo kwa mserereko, huko nyuma ilikuwepo, hii ni changamoto kubwa watumishi wetu wanayo sasa hivi. Utakuwa mtumishi alikuwa na haki ya kupanda cheo mwaka 2012 hakupanda, alikuwa na haki ya kupanda cheo mwaka 2016 hakupanda, pengine mwaka 2019 hakupanda, sasa anatakiwa apande cheo leo. Na pengine kutokupanda kwake cheo kipindi cha nyuma si makosa yake ni makosa ya mwajiri wake. (Makofi)

Mheshmiwa Naibu Spika, tuna m-punish yule mtumishi tumeweka mfumo mzuri kwamba kimsingi yule Afisa Utumishi au mwajiri ambaye hakufanya vile atachukuliwa hatua; je, stahiki ya mtu huyu, kwa hiyo niwaomba wenzetu wa Wizara sasa, wakalitazame jambo hili ni watumishi wangapi walistahili kupanda cheo lini kwa haki na kisha waweze kupatiwa stahiki zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni recategorization hii ni kubadilishwa kada hapa kuna changamoto na kilio kikubwa sana kwa watumishi wetu, utakuta mtumishi amesoma, ni mwalimu diploma akaanza kupanda cheo labda TGS C akapanda D akapanda hadi E baadaye amefika mshahara wa shilingi 1,200,000; sasa ameenda kusoma degree nyingine ya Utawala au yoyote ile, wakati wa kumbadilisha cheo kutoka kwenye yale aliyoyasomea mambo ya ualimu kwenda huku kwenye utawala ambapo kimsingi mwajiri ameridhia kuna nafasi tunaanza kumpeleka akaanze kupata mshahara kwenye Utawala pale inapoanzia entry point yaani kwa mfano kama HR anatakiwa kuanza kulipwa labda HR II shilingi 700,000 huyu mtumishi alifikia level ya ualimu ya kulipwa shilingi 1,200,000 anarudishwa kwenye HR II, ushauri wangu ni nini, tunaweza either ku-maintain ile personal salary au tukai-quit mshahara wa kule anapotoka vis-a-vis huko anakokwenda ili tusiwavunje moyo hawa watumishi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine nililokuwa nataka kulizungumzia pia kwa kidogo ni issue ya madai mbalimbali, kwa mfano nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri aende akatazame madai ya wakufunzi wa Vyuo na Udhibiti Ubora, yako malalamiko ya watu ambao hawakupewa stahiki zao kwa zaidi ya pengine kuanzia mwaka 2018 kurudi nyuma, changamoto ni nini, wanastahili kitu gani? Kama wanastahili wapewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ningependa kuzungumzia kidogo kuhusiana na makundi maalum kwenye utumishi ambao kimsingi Wizara naomba ikasaidie kusimamia, hapa nazungumzia walimu, hapa nazungumzia ma-nurse, hapa nazungumzia madereva, yaani zile kada madereva, walinzi na wale wengine zile kada za chini kwenye level za Halmashauri wale wakubwa wanapata perdiem, wanapata overtime, wanapata extra duty, wengine hawa anaweza kukaa kwenye utumishi wa umma, akafika hata miaka 10 hajawahi kupata.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)