Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia kidogo kuhusu hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Niseme tu kwamba hata jana Mheshimiwa Rais ametuambia kwamba sisi kama Wabunge tuchangie bajeti na kuishauri Serikali, mimi naomba niishauri Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze na hii issue ya Madiwani. Mimi nimewahi kuwa Diwani kwa kiasi fulani naelewa namna vikao vinavyoendeshwa katika halmashauri. Nachopenda kuishauri TAMISEMI ni kwamba Madiwani wapewe mafunzo yaani hilo msilikwepe. Najua mnasema bajeti ni ndogo lakini mnaposhindwa kuwafundisha kama sisi tunavyofundishwa, mimi niko kwenye Kamati ya LAAC nakushukuru kunipeleka kule lakini tunapewa semina namna ya kufanya financial tracking, namna ya kufuatilia na hata namna ya kuhoji tupo equipped kabisa tunakwenda kufanya kazi ile. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, halmashauri inaendeshwa na vyombo viwili; executive na politicians ambao ni Madiwani. Madiwani mnawajua, sisi tunajua kusoma na kuandika unakwenda ndani ya halmashauri unakuta Mkurugenzi ana degree yake wengine masters halafu unamuweka Diwani ambaye anajua kusoma na kuandika lazima kwa vyovyote vile Wakurugenzi wata-overpower Madiwani na hicho chombo kinahitaji Madiwani kama wasimamizi na kile ni chombo chao. Kwa hiyo, kuwafundisha mara kwa mara angalau mara moja kwa mwaka ni muhimu sana hata kwa bajeti ndogo kuwapelekea wataalam wawafundishe namna ya kusimamia halmashauri na fedha za umma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ambacho nashauri katika hili ni kwamba...

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nashauri tumsikilize Mheshimiwa Mbunge.

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, Madiwani katika Kamati zote wanapaswa kusimamia miradi, ndani ya halmashauri miradi inasimamiwa na Kamati ya Fedha ambayo inaweza kuwa corrupted kwa urahisi sana. Kwa hiyo, mruhusu TAMISEMI iondoe hizi kanuni za kuzuia Kamati nyingine zisiende kusimamia miradi ambayo inahusu Kamati zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niongee kuhusu ujenzi wa vituo vya afya katika huduma ya afya, hapa nina maana ya zahanati, vituo vya afya na hospitali. Kitu ambacho nimeona ni kwamba hakuna mfumo wa kudhibiti ujenzi wa miradi hii, hakuna mfumo wa ufuatiliaji na hata TAMISEMI haitoi fedha katika Sekretarieti za Mikoa ili waweze kusimamia miradi hii. Kwa mfano, kuna hiki kitu kinaitwa force account inasimamiwa na Kamati ya Ujenzi katika maeneo ambayo miradi hiyo inatekelezwa hawa ujuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kitu kingine hakuna ma- engineer hata ukisoma tu haraka haraka tu katika ukaguzi wa CAG japokuwa hatujafika mahali paku-discuss lakini tunaweza kufanya reference ametuambia kwamba ma- engineer karibu asilimia karibu 75 walihamia TARURA, kwa hiyo, halmashauri inafanya kazi zake kwa kutumia Kamati za Ujenzi ambazo hazina ujuzi lakini pia kwa kutumia mafundi mchundo (technicians). Kwa hiyo, unaweza kukuta majengo haya ambayo tunajenga ili kutoa huduma kwa wananchi yanaweza kukosa tija kwa sababu hayakusimamiwa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naishauri Serikali iangalie utaratibu wa kuajiri ma-engineer katika halmashauri. Mara nyingi tumependekeza kwamba kuwepo na ma-engineer, juzi hapa tulikuwa Singida na bahati nzuri tulikuwa na Naibu Waziri hapo, tulichokiona na yeye alikiona nisiseme mengi, hiyo inadhihirisha kwamba majengo yanayojengwa na watu hawa kupitia force account na usimamizi wa Kamati hizi kwa kweli mengine nina wasiwasi yakaleta crisis siku zijazo; yakabomoka mapema wakati yametumia fedha nyingi kwa sababu hayako vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ufuatiliaji CAG ametueleza kwamba kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016 mpaka 2019/ 2020 miaka mitano TAMISEMI haijawahi kupeleka fedha ya usimamizi katika Sekretarieti za Mikoa. Ina maana mnawanyima uwezo Sekretarieti za Mikoa kufuatilia na kusimamia miradi hii jinsi inavyojengwa katika halmashauri zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niongeza machache kuhusiana na force account, nashauri iwe na limitation ya fedha, haya ni mawazo yangu, kwamba una mradi wa shilingi bilioni moja na kitu au bilioni mbili, tatu inasimamiwaje na force account? Kwa hiyo, Serikali mtazame kwamba force account kama ni mradi wa shilingi milioni 100, 200, 300 unaweza ukasimiwa na zile Kamati lakini ukishavuka pale ni lazima tufikirie namna nyingine ya usimamizi. Kwa hiyo, tuweke limit katika jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo, niongelee uwezo wa utendaji wa halmashauri zetu. Nimefuatilia hapa wakati Waziri anasoma hotuba yake amegusia kuhusu halmashauri kupewa hati chafu. Unajua mimi huu ukaguzi umenitisha na umenishangaza sana kwa sababu katika Kamati ya LAAC tumefanya kazi kubwa na wewe umetuwezesha, tumejaribu kusimamia na mimi nashangaa hizi hati zimetoka wapi, kwa kweli mimi sikufurahi lakini nilichoona ni kwamba kuna uwezo mdogo wa watendaji ndani ya halmashauri. Kitu kingine hata uteuzi wa Wakurugenzi hauzingatii uwezo wa kusimamia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni kwa sababu gani nasema hivyo? Local government ina tofauti na Serikali Kuu, kuna chuo pale Hombolo special kwa sababu hiyo, kwa hiyo, Wakurugenzi wanapaswa kufanyiwa vetting japokuwa Katiba inasema tuwatue. Mimi kwa mawazo yangu nafikiri watu wangeomba, wakafanyiwa vetting ndiyo waajiriwe au mtazame wale ambao wameshafanya kazi kwenye local government; amekuwa Mweka Hazina au Afisa Mipango ana uzoefu wa aina fulani wa kuendesha local government. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hali ilivyo kiutendaji ndani ya halmashauri kwa kweli hata kwenye idara huku mnapatupa lakini mkumbuke bajeti mliyoomba leo shilingi trilioni saba na kitu is a lot of money. Kwa hiyo, mnakwenda ku-deal na pesa nyingi sana na halmashauri ndiyo zinasimamia maendeleo ya watu, zinatekeleza sera ya Serikali Kuu, ndiyo zinaelekezwa kama ni kuandikisha watoto kwenda shule kila kitu ninyi kama Serikali Kuu mnaelekeza halmashauri inafanyia kazi. Kwa hiyo, tunapaswa kuwa na watendaji wazuri lakini pia tunapaswa kuziwezesha kwa sababu sasa hivi mnajua kwa muda wote tulikuwa tunalia halmashauri zimenyang’anywa mapato yote.

Mheshimiwa Spika, nimalizie haraka haraka nasikia kengele ya kwanza imeshagonga, hata hii ten percent ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ni kitu kizuri kabisa lakini ukitazama ametueleza ni zaidi ya shilingi bilioni 29 ambazo zimeshatolewa kwa makundi. Naomba niulize hizo pesa huwa zinarejeshwa na zinawekwa wapi?

Mheshimiwa Spika, kama hamjawahi kuona kama kuna pesa inapigwa, ni pesa hii. Nenda kwenye Halmashauri, ikirejeshwa inawekwa kwenye akaunti ipi? Hakuna rotation hapo. Maana yake, nafikiria kwamba tungeweza kuwa na bar kwamba sasa Halmashauri ina mfuko wenye shilingi bilioni tano, hiyo pesa nyingine itajenga kitu kingine na hii itakuwa ina-rotate. Fedha hizi hazirudishwi, yaani inakuwa kama zaka; kama sadaka vile. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi fedha zinapelekwa kisiasa, watu hawazirudishi. Zikirudishwa, uliza Halmashauri, zinawekwa akaunti ipi? Tulipewa taarifa kwamba kuna akaunti zimeelekezwa kufunguliwa, hatujafuatilia sana labda tutafuatilia wakati huu tukienda kugakua baada ya CAG kutoa ripoti yake, lakini hakuna akaunti yoyote ambayo inahifadhi hizi fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, zinarudishwa, zinawekwa kwenye akaunti ya amana; mara zisemwe ni za maendeleo na kadhalika. Huwezi kumwuliza Mkurugenzi ziko wapi? Ina maana anapashwa kukata kila mwaka. Anapaswa kukata kwenye kila mapato, anakata wee, mpaka lini? Kwa hiyo, anapaswa kukata, lakini kuwepo na bar ili huu mfuko ufanye rotation. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)