Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuniteua kuwa Waziri wa Mambo ya ndani. Nawashukuru sana wananchi wa Misungwi kwa kuendelea kuniamini na kupata asilimia themanini na kitu, haikuwa jambo dogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, niende moja kwa moja kwenye hoja ambazo Waheshimiwa Wabunge wamezitoa. Naanza tu kwa kusema, upande mmoja una haki lakini upande mwingine lazima kuwe na wajibu. Ukidai haki, timiza wajibu wako. Ndugu zetu kwa mfano, kama jana walikuwa wakidai haki, lakini hawakutimiza wajibu wao kwa kufanya fujo na ndiyo sababu Wizara yangu iko pale kuhakikisha kwamba nchi yetu inaendelea kuwa tulivu na salama. Hilo tutalifanya kwa nguvu zetu zote kwa sababu hatuwezi kufanya biashara, wala shughuli zozote katika mazingira ya ambayo hayana utulivu na siyo salama. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie mambo machache tu ambayo Waheshimiwa Wabunge wameyazungumzia tukianzia na malalamiko mengi hasa oparetion ya bodaboda yaani ya pikipiki.
Waheshimiwa Wabunge, pamoja na wananchi wote, mtakumbuka kwamba hivi karibuni limejitokeza wimbi kubwa la uhalifu unaosababishwa na watu wanaoendesha pikipiki. Kwa hiyo, hapa hatuzungumzii bodaboda peke yake, tunazungumzia pikipiki zote.
Kwa hiyo, oparetion tunayoifanya sasa hivi ni ya kujaribu kuhakiki na kuona kama pikipiki zote zinamilikiwa kihalali na watu gani na kuhakikisha kwamba kila mmoja anayepita katika eneo linalotakiwa, anapita kwa kufuata Sheria za Usalama Barabarani.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili ni jambo la usalama zaidi ili tuweze kuishi katika mazingira salama na wananchi wasiwe na wasiwasi, vilevile watu wote walio na pikipiki za kawaida au bodaboda wasiwe na wasiwasi, hili ni kwa nia njema na kuhakikisha kwamba nchi yetu inaendelea kuwa salama na tulivu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo limezungumziwa, ni la wakimbizi. Ni kweli wakimbizi kwa miaka ya nyuma walifikia kwenye 800,000, lakini walipungua sana na sasa hivi hali inaanza kurudia tena. Kwa sasa hivi tuna wakimbizi kwa mfano tuna Wakongo 63,000; tuna Warundi wapya ambao wameingia 124,000; tuna wakimbizi kama 199 wengine kutoka hata nchi kama Syria, lakini bado wanakuja kwetu, lakini tuna wakimbizi wengi tu, Warundi wapya ambao wamekuja tena sasa hivi ni 124,637.
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kinachotupa nia ya kujipanga upya sasa hivi ni kwamba baadhi ya wakimbizi wanaokuja wametoka katika maeneo ya majeshi. Wanapofika katika maeneo ya wakimbizi wanaanza kufanya recruitment ya askari. Hili tumeliona na tumejipanga na tunahakikisha kwamba halitaendelea. Nchi yetu haiwezi kuwa chanzo cha askari wanaokwenda kufanya vurugu katika nchi za majirani zetu. Nihakikishe tu kama alivyosema Mheshimiwa Rais katika hotuba yake kwamba, wale watakaokuwa wanahitaji Uraia, utaratibu utafuatwa kulingana na sheria zetu na tutaweza kuwapatia uraia.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo limezungumziwa na watu wengi, ni hili la maisha mazuri ya askari polisi wetu. Kitu cha kwanza wamezungumzia…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa
muda wa Mzungumzaji)
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Kitu cha kwanza ambacho wamezungumzia ni nyumba. Niseme tu kwa sababu ya muda, kwamba tuna mpango wa kujenga nyumba mpya 3,500 kila mwaka kwa ajili ya polisi wetu. Nakushukuru sana. (Makofi)