Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, ahsante awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametujaalia neema hii ya uhai siku ya leo tukapata fursa ya kuchangia katika katika Mpango wa Taifa letu ambao utakuwa ni chachu ya maendeleo na kuweka sawa hali za Maisha za wananchi.

Mheshimiwa Spika, nianze na dhana au dhima ya mpango huu ni kuwa na uchumi shindani lakini pia kuangalia na maendeleo ya watu na maana ya kuwa na uchumi shindani maana yake tunawashindani na kwa kuwa tunawashindani kwa maana hiyo tuna watu ambao pia tunawashindania kwamba hawa wawe wetu.

Mheshimiwa Spika, sasa tukiangalia kwenye maana hiyo Taifa letu sasa kwa kuwa tuna ushindani na uchumi wetu uwe shindani siye tuwe juu tunapaswa kuwa na miundombinu mizuri na kuondosha vikwazo ili hao tunaoshindana nao sasa sisi tuibuke kuwa champion. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano katika sekta ya usafirishaji tunajua tunaanza kuanzia bandarini tunashukuru tumejenga bandari zetu vizuri tumeimarisha lakini kama tunahisi tunavikwazo hivi vikwazo ndivyo vya kupambana navyo ili tuondoshe. Kwasababu katika eneo la bandari majirani zetu wa Kenya ndiyo tunashindana nao kwa bandari ya Mombasa, Msumbiji tunashindana nao kwa bandari yao ya Beirra lakini Durban pia tunashindana nao na hakuna bandari nyingine.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo kama mnataka kujenga uchumi shindani katika sekta ya usafirishaji ina maana kwamba sisi tuwe na bandari bora lakini pia tuwe na mambo mazuri ambayo yataondosha vikwazo watu waweze kuraghibika kupita katika bandari zetu wapiti kwenye mabarabara yetu wapite katika railway zetu wapite na maeneo mengine ili ule usafirishaji uende vizuri.

Mheshimiwa Spika, lakini pia tutizame wateja wetu hawa tunaowasafirishia wako wapi na wapi na sasa hivi katika usafiri wa barabara ukiangalia tunaweka maeneo ambayo ya mizani. Pengine linaweza likasababisha pengine sisi ku-slow down watu wakatukimbia wakaenda katika maeneo mengine. Kwa hiyo, tufikirie tuwe na hikma ya kutizama katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, eneo jingine ni kodi ambazo zinahusiana na usafirishaji tukiweza kuondosha kikwazo hicho kwa hiyo, tutaweza kujenga huo uchumi shindani lakini pia tutapata kuwagharamia watu wetu katika maendeleo yao hilo ni moja.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili niende katika sura inayozungumzia ugharamiaji wa mpango tumesema mpango wetu utagharamiwa kwa trilioni 114 tukaweka Serikali itachangia trilioni 74 na sekta binafsi tukasema itachangia trilioni 40.6. Sasa nije katika upande wa Serikali, Serikali tumesema kwamba tutakuwa tuna mapato ya ndani ambayo ni trilioni 62 katika kuchangia mapato ya ndani sasa mapato haya ya ndani yanachangiwa na mapato ya kodi sasa hapa kwenye mapato ya kodi ambayo yanachangia 65% mapato ya kodi tunaweza tukaja tuka tukaona kwamba kumbe tuna vikwazo kwenye mapato haya ya kodi.

Mheshimiwa Spika, vikwazo vyenyewe ni vipi zipo kesi kule TRA katika Bodi na katika Baraza ambazo zina fedha trilioni lakini kesi zile zimesimama hazijaendeshwa au nyingine zimekaa zimedunda ina maana pale pana mapato ya ndani ya kodi lakini tunayakosa, tukiboresha tukienda kwa wakati tukawa na ufanisi katika mashauri haya ya kodi ina maana kwamba tutaongeza mapato ya kodi na tunaweza kufika vizuri katika mpango wetu huu katika utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ripoti ya CAG ya mwaka 2018/2019 ambayo tuliijadili hapa Bungeni imeelezea kesi ambazo zimekwama kwasababu Bodi haitimizi quorum au hilo Baraza halitimizi quorum na halitimizi quorum kuna mtu ana mamlaka ya uteuzi? Hakuteua huyo mtu hao wajumbe hajawateua. Sasa tukiondosha hivi vikwazo ina maana kwamba hizi fedha tuna uwezo wa kuzipata na tukagharamia miradi yetu wka kupitia mapato ya kodi. Kwa hiyo, Serikali tusikilize katika hili kuna nafasi zinahitaji uteuzi kesi haziendi kwa hiyo kama tutafanya hivyo tutaongeza mapato ya ndani.

Mheshimiwa Spika, pia kuna fedha ambazo zipo katika kesi, kesi ambayo anayeshitakiwa anatakiwa alipe 1/ 3 yake fedha zile zikikwama 1/3 ya yule mtu imekaa pale imeganda hawezi kujiendeleza kuajiri wala kufanya jambo jingine. Lakini 2/3 ya Serikali ambayo kama Serikali itashinda ina maana kwamba pia itakuwa imekosekana kwa hiyo, tunaomba Serikali hili ikalifanyie kazi ili katika kugharamia mpango wetu tuende vizuri.

Mheshimiwa Spika, jingine katika sekta binafsi ambayo inagharamia trilioni 40 mpango uliopita sekta binafsi tulilipa trilioni 48 lakini ikafanya vizuri mpaka kufikia miaka minne katika mpango uliopita sekta binafsi ilikuwa tayari washatumia trilioni 32 kati ya trilioni 48. Kwa maana hiyo ukiweka average kwamba kila mwaka sekta binafsi ina uwezo wa kuchangia trilioni 8. Kwa maana hiyo ndani ya mwaka huu sekta binafsi itakuwa tayari inakamilisha trilioni 40 ingawaje zile 8 kwamba zitakuwa hazikuweza kupatikana.

Sasa safari hii tumeweka blue print, tunaondosha vikwazo lakini bado sekta binafsi tuliweka hii trilioni 40 ina maana hapa ni lazima kuna jambo la kufanya kwa sekta binafsi pamoja na kutumia uwezo huo ambao tumeondosha ina maana ilikuwa sekta binafsi hapa ni lazima tuzidi kwasababu tayari watu watakuwa washashawishika katika kuendelea kutu-support katika miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niiombe Serikali izidi kushirikiana na sekta binafsi ili ugharamiaji wa sekta binafsi ukiongezeka itakuwa vizuri kwasababu Serikali haijaipata ki- percentage sekta binafsi. Sekta binafsi ki-percentage iko juu kuliko Serikali, kwahiyo hilo ilikuwa nalo pia nilikuwa naomba tuliangalie.

Mheshimiwa Spika, jingine ni jambo muhimu sana ambalo kamati ya bajeti imeshauri tuwe na sera ya monitoring and evaluation tuwe na sera hiyo tusipokuwa na sera hiyo ina maana hata sisi hapa Wabunge tutakuja kujadili mwezi wa tano lakini bila kuletewa ripoti ya utekelezaji ambayo ipo sahihi. Kwa mfano kama tukiwa na monitoring tu peke yake tutajua base line tutajua kwamba hapa tunaanza kutokea ngapi kwenda ngapi. Tuna set target zetu tutapata kupima target zetu whether tumeshindwa katika kupata input tutajua kwamba tatizo ilikuwa ni input na input hizo zimeshindikana na kitu gani tunaweza tukabadilisha msimamo katikati kabla ya kufika miaka mitano. (Makofi)

Mheshimiwa Spka, lakini tukisubiri miaka mitano ina maana kwamba tutakuja kupima matokeo makubwa tutashindwa kujikosoa katikati na ndiyo maana mfano tuna miradi hiyo ambayo imetajwa na kamati hapa miradi ya Mchuchuma Liganga Magadi soda kule Engaluka kwasababu haiwezi kufanyiwa hivyo kwasababu kila mwaka inapita vilevile na mpaka sasa hivi ukiuliza utaambiwa kwamba iko katika hatua ya kulipiwa fidia mradi wa miaka 20 uko katika hatua ya kulipiwa fidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini ingelikuwa kunafanyika monitoring wapi tunakwamba tungeweza kutatua vikwazo na sisi Wabunge tungeweza kushauri. Niseme hayo ingawaje na wengine watayasema haya haya kwasababu mtemewa mate na wengi hurowa tunapenda ushauri wetu huo uchukuliwe nashukuru sana naunga mkono hoja. (Makofi)