Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

Hon. Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Mpango ulio mbele yetu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitajikita upande wa TARURA kwa sababu nimeona Wabunge wengi wanaongelea kuhusu masuala ya kilimo. Asilimia kubwa katika nchi yetu ya Tanzania ni wakulima na Wabunge wengi wamesema kuwa kilimo kitatufikisha mbali zaidi kwa ajili ya kuongeza uchumi wa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mifuko mbalimbali ambayo tumeshaiweka katika Bunge hili, mfano Mfuko wa Maji na tumeona jinsi gani mifuko hiyo inavyosaidia maendeleo katika nchi yetu. Naomba kupitia Mpango wetu tuanze kutafuta Mfuko wa TARURA kupitia mitandao yetu ya simu. Tukipata shilingi 10 katika kila call nafikiri tutapata hela nyingi sana ambapo tutafungua mfuko mkubwa kwa sababu kwenye mitandao yetu ya simu hatujawahi kuchukua kitu chochote kwa ajili ya maendeleo ya jambo lolote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua Mfuko wa Maji tunachukua kwenye petroli na dizeli, sasa hivi tuchukue kwenye mitandao ya simu kwa ajili ya TARURA. Wananchi wetu wakilima vizuri na barabara zetu zikawa nzuri ina maana uchumi wa nchi yetu utakuwa mkubwa zaidi kupitia wakulima na vilevile Taifa letu litaongeza kipato kupitia kilimo chetu. Naomba sana TARURA itafutiwe mfuko maalum kwa ajili ya kuchangia mfuko huo ili tuweze kupata manufaa kupitia barabara zetu za vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende upande wa elimu. Najua toka Awamu ya Tano ni bure. Ilivyoingia elimu bure tulianza kupata wanafunzi wengi ambapo darasa la kwanza au darasa la awali tulikuwa tunaingiza watoto 1,000 shule zingine mpaka 1,200. Tutambue kuwa lazima tuweke mpango maalum kuanzia sasa hivi tujipange vizuri ili baada ya miaka saba inayokuja mbele yetu tuwe na madarasa mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tu unakuta darasa moja lina watoto 80, tunakuja kuanza kuhangaika na pressure lakini tutambue kuanzia Awamu ya Tano imeanza kuwa na watoto 1,000 darasa la kwanza ina maana mpaka sasa hivi watoto 1,000 wako darasa la sita kwa darasa moja. Sasa ni lazima tuanze kuweka mikakati ya kuelekea sekondari tuwe na madarasa mengi ili tuweze kupata manufaa zaidi na elimu ikaendelea kuwa bora zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tutambue kuwa lazima sasa tuwekeze katika kutoa ajira. Tutoe ajira kwa walimu elimu ya shule za msingi na sekondari kwa sababu walimu wetu ni wachache sana na kila siku tunajenga shule za sekondari, tunajenga shule za msingi, wanafunzi wanaongezeka lakini kasi ya kuongeza walimu haipo. Naomba sana Serikali sasa hivi ijiwekeze kuanza kuweka mkakati wa ajira kwa ajili ya walimu wa kufundisha watoto wetu kwa sababu ni wachache sana na tunaendelea kufungua shule siku hadi siku, shule za kata zinafunguliwa siku hadi siku…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa, kengele imegonga.

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nashukuru. (Makofi)