Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

Hon. Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa kibali cha kusimama tena katika Bunge lako Tukufu. Pili, niwashukuru wa kina mama wa Mkoa wa Kagera kwa kunipigia kura nyingi za kishindo. Tatu, nikishukuru Chama changu cha Mapinduzi kwa kunipitisha tena kuingia tena Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Rais wetu wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri anazozidi kuzifanya katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Pia nampongeza Waziri wa Fedha na Mpango kwa kutuwasilishia Mpango ili tuweze kuujadili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nijielekeze moja kwa moja katika mchango wangu. Nitachangia kuhusu vituo vya afya na elimu kidogo. Vituo vyetu vya afya vilivyojengwa sasa hivi ni vya kisasa kabisa, vina maternity ward, theatre, maabara, mortuary na nyumba ya daktarin. Hata hivyo, changamoto iliyopo hakuna wodi ya wanaume wala wanawake. Kwa hiyo, naiomba Serikali Tukufu waweze kujenga wodi za kina baba na kina mama kwa ajili ya kusaidia wale wananchi wa hali ya chini ili wakifika pale waweze kupata first aid, labda wanaweza kupata drip wakapumzishwa pale kabla hawajaenda kwenye vituo vikubwa vya afya. Kwa hiyo, naomba Serikali yangu Tukufu iweke mpango mzuri wa kujenga hizo wodi za kina baba na kina mama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kwa moja nijielekeze katika suala zima la elimu. Nashukuru Serikali yangu Tukufu imetelekeza vizuri Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi kwa suala la elimu, kuanzia darasa la kwanza hadi form four elimu ni bure. Hata hivyo, mwanafunzi wa hali ya chini akimaliza form four, form five na six kama amefaulu vizuri hawezi kwenda shule. Kwa hiyo, naomba Serikali yetu Tukufu kwa sababu imeshajitoa yaani hapo imekula ng’ombe mzima bado mkia, iweze kuangalia watoto wetu waweze kufika mpaka form six kwa elimu bure kwa sababu akishaingia chuo kikuu anapata mkopo. Kwa hiyo, naomba Serikali yangu Tukufu iliangalie hilo kwa kwa ajili ya kuokoa kizazi chetu na watoto maskini kama Rais wetu wa wanyonge anavyosaidia. Kwa hiyo, naomba aendelee kusaidia hawa watoto waweze kusoma vizuri mpaka form six ili waweze kuingia chuo kikuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijielekeze pia kwenye miundombinu ya barabara. Kule kijijini kwetu miundombinu siyo mizuri, unakuta hakuna barabara, mkulima ameshalima mazao yake ili aweze kuyafikisha kwenye soko barabara ni changamoto kubwa sana. Kwa hiyo, naomba Serikali yangu Tukufu isiangalie barabara kuu tu iangalie na Kisingimbi kwetu kule vijijini waweze kuweka barabara Rafiki, mkulima akimaliza mazao yake mazuri aweze kufika katika masoko kuuza mazao yake ili kujikwamua kiuchumi aweze kusaidia na familia yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yangu yalikuwa ni hayo, nashukuru san ana naunga mkono hoja. (Makofi)