Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, ahsante. Awali ya yote, nimshukuru Mwenyezi Mungu kutusajili siku ya leo kuwa miongoni mwa viumbe ambao wana uhai na wana afya. Pili, nikushukuru kwa kunipa hii nafasi ili niweze kuchangia katika hotuba ya Rais ambayo ameitoa mwezi wa 11 wakati wa kufungua Bunge.

Mheshimiwa Spika, lingine nikishukuru chama changu na wananchi wa Jang’ombe kwa kunijalia kurudi tena hapa Bungeni kwani si kazi ndogo kufikia ukarudi. Kwa hiyo, nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuendelea kuliongoza Taifa hili hali ya kuwa tuko katika uchumi mzuri na katika utulivu na usalama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja yangu mwanzo nitajikita katika ukuaji wa uchumi. Mheshimiwa Rais ametuongoza katika kukuza uchumi na ameeleza katika ukurasa wa 18 kwamba kila mwaka uchumi wetu ulikuwa ukikua kwa asilimia 7 kutoka 2015 hadi 2019 hata na hii 2020. Imeonyeshwa hapo kutoka shilingi trilioni 94.4 mpaka kufikia shilingi trilioni 140 maana yake ni kwamba katika miaka mitano hii tumeongeza karibu ya one third katika GDP yetu ambayo imeanza tokea miaka ya nyuma. Kwa hiyo, katika kipindi cha miaka mitano tumefikia hivi.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi tuko katika uchumi wa kipato cha kati lakini pia Mheshimiwa Rais amesisitiza kwamba tunataka kuendeleza ukuaji wa uchumi na ndipo katika eneo hilo ninapotaka mimi kuchangia. Katika eneo hilo nataka nijikite zaidi katika uvuvi wa bahari kuu. Kuna msemo wa wahenga wanasema mtemewa mate na wengi hulowa, kwamba lilishazungumzwa hili eneo la uchumi wa bahari kuu lakini na mimi nalirejea tena kulizungumza kwa umuhimu wake ili lipate kutiliwa mkazo zaidi.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 35, 36 na 37 wa hotuba ya Mheshimiwa Rais ameelezea kwamba ana azma ya kukuza pato la Taifa kwa kuimarisha uvuvi wa bahari kuu lakini pia ameelezea mapato ambayo tunayapoteza ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 350, lakini pia ameelezea makusanyo ambayo sasa hivi tunapata kupitia uvuvi wa bahari kuu kwa sababu tunafanya katika ufinyu wake tunapata shilingi bilioni
3.3 kila mwaka. Kwa hiyo, tunapoteza shilingi bilioni 352 kila mwaka lakini tunachopata sasa hivi kutokana na ufinyu wa uchumi wa bahari kuu tunavyoutumia ni shilingi bilioni 3.3. Taarifa hizi ni rejea za ripoti ya Bunge la Kumi na Moja, tunakupongeza sana Mheshimiwa Spika kwa kulisimamia hili na data hizi sasa hivi zinatumika huko.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameeleza kuwa miaka hii mitano atasimamia vizuri uchumi huu. Pia katika shughuli hii ya uvuvi wa bahari kuu tayari sheria yake imeshapitishwa na Bunge lako Tukufu lakini pia Rais amepanga kununua meli nne Tanzania bara na meli nne Zanzibar. Pia kujenga bandari moja kubwa ya uvuvi itakayoajiri zaidi ya watu 30,000. Vilevile atahamasisha sekta binafsi kuwekeza katika viwanda vya kuchakata samaki ambapo huko ajira zitazaliwa.

Mheshimiwa Spika, haya ni maelezo ambayo yako katika hotuba ya Mheshimiwa Rais, sasa ushauri wangu. Ili tufaidike kikamilifu katika fursa hii basi ni lazima tuwekeze katika ukamilifu wake, tusipowekeza katika ukamilifu wake zile faida tunazozifikiria kwamba tutazipata hatutoweza kuzipata. Soko la samaki linategemea mazingira ya samaki tokea anavyuliwa, bandari gani amepokelewa, store gani amehifadhiwa na mengine mengi ambayo yako katika facilities katika uvuvi huu wa bahari kuu.

Mheshimiwa Spika, kiufupi facilities zote zipatikane ndiyo tutafikia katika haya maono ambayo Mheshimiwa Rais ameyaona na ndipo tutafikia katika ripoti ambayo imetolewa na Bunge hili kwamba tukiwekeza katika bahari kuu tutafaidika na hayo. Sasa ili tufaidike na uvuvi huu tuangalia resources tutapata wapi? Serikali peke yake haitotosha kutoa resources zake kwa ajili ya kuwekeza katika uvuvi wa bahari kuu. Kwa hiyo, inputs ni lazima tuchanganye kutoka katika sekta ya umma, sekta binafsi, lakini pia katika mchanganyiko wa sekta ya umma na sekta binafsi yaani ubia (PPP). Pia siyo makosa tukawaalika wenzetu wa nje wakaja wakatusaidia katika uwekezaji kwa sababu hii sekta inatakiwa kufanywa katika ukamilifu wake. Pia siyo vibaya kupata uzoefu kutoka katika mataifa mengine wanafanyaje wenzetu mpaka wanafaidika na mambo hayo?

Mheshimiwa Spika, lakini pia kwa kuwa Rais amesema na kwa kule Zanzibar atanunua meli nne, ina meli nne hazitoweza kufua dafu hizo meli zitavua lakini wapi tunaweza kupeleka itakuwa hakuna kwa kupeleka kwa sababu hakuna bandari na ikiwa hakuna bandari hiyo hata viwanda vya kuchakata havitakuwepo na hivyo kufanya marketing yake samaki hao itakuwa ni vigumu, kwa hiyo, hii fursa tunaweza tukaikosa. Sio vibaya na sisi tukawa na dhana au aspect hii ya uchumi wa blue tukiwa na huo uchumi wa blue nao pia unaweza ukatusaidia.

Mheshimiwa Spika, hoja ya pili, Mheshimiwa Rais katika ukurasa wa 62 na 63 ametambua shughuli nyingi sasa hivi zinafanywa kwa kutegemea TEHAMA. Kwa hiyo, TEHAMA ameipa kipaumbele na ameeleza katika kurasa hizo kwamba amepanga kuongeza wigo wa matumizi wa mawasiliano ya kasi lakini pia kufikisha miundombinu ya mkongo wa Taifa ameeleza ili iwafikie wananchi wengi wa Tanzania na mambo mengine mengi ameeleza katika kurasa hizo ambayo yanahusiana na mambo ya TEHAMA.

Mheshimiwa Spika, pamoja na haya ambayo Mheshimiwa Rais amesema, nampongeza sana ameweka Wizara inayoshughulikia masuala ya TEHAMA. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuliona hilo.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna dhana ya digital economy, hapo ndiyo kwenye hoja yangu mimi, pamoja na uwekezaji huu hivi sasa kutokana na digital economy transactions nyingi sana zinafanyika online kwa maana hiyo tunakosa kukusanya mapato kikamilifu kutokana na dhana hii. Sasa hivi hapa ukienda katika makampuni mengi unaweza ukaagiza unachotaka, ukalipa na ukaletewa lakini Serikali haipati kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kupitia mfumo huu wa TEHAMA, naomba Serikali ijaribu kuangalia katika eneo la ulinzi na usalama kwanza lakini pia Serikali ikasomeshe vijana hapa tunakosa vitu vingi sana ambavyo vinatokana na tax zinazopatikana kutokana na hizo transactions zinazofanyika off show. Tusiseme watu wasifanye hiyo biashara ya off show lakini mpiganaji mzuri ni yule mtu anayemfuata mtu angani kuliko kusema umpopoe mawe aanguke chini um-charge huku chini. Kwa hiyo, Serikali itafute na isomeshe hao vijana ili tuweze kufaidika na hicho kitu.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ni la umuhimu sana katika uchumi wetu wa Tanzania ili uweze kukua tumeanzisha hii standard gauge reli na imeanza Dar es Salaam tumekusudia inakwenda mpaka kwenye mipaka yetu, lengo letu tuitumie vizuri bandari yetu ya Dar es Salaam. Kwa hiyo, hoja yangu inaanza kujikita kutokana na ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na hili amelieza Mheshimiwa Rais na hoja yangu pia inajikita katika utoaji au upatikana wa fedha.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, muda wangu umeishia hapo na nashukuru kupata nafasi hii, naunga mkono hoja. (Makofi)