Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Mbaraka Kitwana Dau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii. Nami niungane na wasemaji walionitangulia kumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana hapa na kuweza kujadili masuala yanayohusu Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba nzuri iliyojaa weledi mkubwa sana. Kwa namna alivyoiwasilisha jana hapa, mimi nasema hotuba ile ilistahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu.

Mheshimiwa Spika, nikupongeze sana na wewe mwenyewe. Kama ingekuwa ndiyo ile miaka ya nyuma ile, sisi wengine ni form one humu, saa kama hizi hapa umezungukwa na milima ya ma-volume, tukianza kuperuzi, kutafuta votes na vitu kama hivyo, lakini mwaka huu mambo mazuri kabisa hapa, tuko ki-digitali zaidi. Hili ni matunda yako wewe na tunakushukuru sana kwa kweli, umetuwezesha sasa tunaweza tukatekeleza majukumu yetu humu kisasa zaidi.

Mheshimiwa Spika, mimi pia nitie neno kwenye hili janga la Corona. Hili janga ni kubwa na katika muda ambao Watanzania tunatakiwa tuwe na mshikamano wa hali ya juu basi ni katika kipindi kama hiki cha sasa. Hili jambo si dogo, rai yangu ni katika maeneo makubwa mawili. Eneo la kwanza tuendelee kufuata maelekezo ya wenye mamlaka, viongozi wetu namna gani tutakavyoweza kufuata miiko na makatazo mbalimbali, kupeana mikono, kukumbatiana, kuepuka mikusanyiko isiyokuwa na lazima na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Spika, lakini zaidi ya hapo naomba sana Serikali sasa ianze kuyafanyia kazi yale ambayo yanasemwasemwa kwamba ni lapse ndogondogo kwenye system zetu. Kwa mfano, sasa hivi kuna habari zinasemwa kidogo kwenye mipaka yetu, hususan kwenye kiwanja cha ndege bado panaonekana kama kuna ulegevu kidogo. Kuna watu wanapenya, watu wanasema kwamba kuna watu wengine wanapelekwa hoteli kwenye quarantine kuna wengine wanapita. Mambo kama haya katika kipindi kama hiki ni vizuri sana wenye mamlaka sasa wakatupia macho kwa sababu kila aina ya habari si ya kuidharau katika nyakati kama hizi, tuko katika nyakati ngumu sana.

Mheshimiwa Spika, mimi niingie kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kwenye hotuba hii ukurasa wa 10 tu mwanzoni pale imeelezea mafanikio mbalimbali ya Serikali ya Awamu ya Tano. Yamezungumzwa mengi, mimi nitazungumza moja tu hapa, suala la Standard Gauge Rail.Nalizungumzia hili kwa sababu Kamati yetu ilipata fursa ya kutembelea pale na tukaangalia toka pale mwanzo, Dar- es-Salaam kwenye station kubwa mpaka huku Soga. Tulipita na gari sambamba na zinapojengwa zile track, tumeona uwekezaji ule ni mkubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli katika namna ya kipekee sana tumpelekee pongezi Mheshimiwa Rais, hili wazo kwa kweli ni kubwa na mradi ule ni mkubwa na hali inayokwenda pale kwa kweli isvery promising. Niseme tu kwamba yale masuala mengine ambayo tuliyaona kwenye Kamati na tukatoa ushauri pale na namuona Mheshimiwa Naibu Waziri basi muyafanyie kazi kwa sababu, by July tumeambiwa kwamba kipande cha Dar-es-Salaam – Morogoro kitaanza kazi, lakini bado masuala ya kununua vile vichwa vya treni na mabehewa bado halijakaa sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini lingine nitachanganya kwa sababu naona kengele imeshaanza kuni-alert, ukurasa wa 14, 50 na 57, nitayazungumza kwa pamoja. Limezungumzwa suala la utalii na miundombinu ya usafirishaji. Suala la utalii, mimi natokea katika Kisiwa cha Mafia, ni kisiwa cha utalii. Suala la utalii linakwenda sambamba na miundombinu yake, pale tuna miundombinu mbalimbali ikiwemo ya gati pamoja na Kivuko kile cha Nyamisati. Naishukuru sana Serikali gati lile limekamilika na kivuko kile kinajengwa. Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ametoka lakini Mheshimiwa Naibu Waziri namwona, tuna tatizo pale kwenye kile Kivuko kinachoundwa cha Nyamisati kazi ilikuwa inakwenda kwa kasi sana lakini ghafla kasi imepungua.

Mheshimiwa Spika,mimi pale Mheshimiwa Waziri aliniambia kwamba ninakupa jukumu kila mwezi uje hapa kufuatilia na mimi ninakwenda pale kila baada ya wiki mbili. Mara ya mwisho mkandarasi analalamika pale fedha zake hajalipwa lakini nimekwenda kufuatilia kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha, tayari fedha zile ameshazitoa ziko Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi. Kwa hiyo, naomba mharakishe tu kumlipa yule mkandarasi ili amalizie kile kivuko tuwe ndani ya muda na tuweze kusonga mbele.

Mheshimiwa Spika, kwa harakaharaka kule Mafia tuna barabara inayotoka pale Kiwanja cha Ndege pale Kilindoni kwenda mpaka Rasi Mkumbiambayo ni kama kilometa 55. Barabara ile imo ndani ya ahadi ya CCM na ni ahadi pia za Rais Mstaafu. Hata hivyo, hivi sasa tuna changamoto pale, tunaona nia ya Serikali na Wizara kuhakikisha kwamba barabara ile inawekwa lami na sasa hivi pale yupo yule consultancy anamalizia suala la usanifu na kuangalia namna watakavyowalipa watu fidia, imeleta sintofahamu kubwa sana kule Mafia, sasa hivi wananchi wengi wameondolewa kwenye hili sakata la kulipwa fidia zao.

Mheshimiwa Spika, siyo kwa kiburi wala jeuri tunachosema kwamba sisi Mafia tuko tayari barabara hii ichelewe kwanza lakini masuala ya malipo ya wananchi hawa yazingatiwe. Kwa sababu mimi nina uzoefu barabara ambayo nimeirithi kutoka kwa mwenzangu ambayo ilijengwa kwa lami mpaka leo ofisini kwangu kuna mafaili na mafaili ya madai mbalimbali ya wananchi ambao fidia zao walikuwa hawajapata.

Mheshimiwa Spika, sisi tunaishukuru Serikali kwa nia njema kabisa na naiona nia ya Mheshimiwa Waziri mwaka ujao wa fedha kuanza kuweka lami barabara ile lakini suala hili la fidia la wananchi wangu inaniuma sana kuona kwamba hata kama tutapata barabara ya lami lakini mwananchi wangu akakosa kulipwa fidia yake kwangu mimi haitanipa comfort sana. Nipo tayari kusubiri lakini tuhakikishe kwamba suala hili linashughulikiwa.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)