Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru. Nami nianze kuzungumzia ambapo ameishia Mbunge mwenzangu wa Iringa kuhusiana na ugonjwa wa CORONA.

Mheshimiwa Spika, kiukweli mimi pamoja na mambo mengine mazuri ambayo Waziri Mkuu ameyasema lakini katika hotuba yake sijaridhika kabisa na jinsi ambavyo amelizungumzia suala la huu ugonjwa wa Corona, amelizungumza kwa kifupi sana. Jana wakati ulitupa nafasi ya kujadiliana hapa tulisema kwamba tuko vitani na tunapokuwa vitani lazima tujiandae kwa kiwango kikubwa sana. Tukiwa wa kweli kama Watanzania na kama Wabunge suala la kunawa mikono ambalo Serikali inajua imechukua hatua, suala la hygiene, masuala ya kunawa mikono wenzetu Ulaya, Marekani, ni kitu cha kawaida kabisa. Sipingani kabisa na hatua zilizochukuliwa na Serikali za kunawa mikono, lakini kama tunataka tudanganyane hapa tu kwa kunawa mikono na visabuni vile tumeweka kwenye maduka kwamba tunapambana na Corona wenzetu Ulaya suala la kunawa mikono sio swali. Ndiyo maana unawakuta wanakula bila kunawa wakati mwingine lakini suala la kunawa mikono haliko kwenye akili kwa sababu wakati wote wananawa mikono. Kwa hiyo, mimi nadhani…

SPIKA: Katika watu ambao hawanawi mikono Wazungu namba moja.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, hapana, sio kweli. Sio kweli, tabia ya kunawa mikono Wazungu ni ya kawaida kabisa, ni maisha yao.

MBUNGE FULANI: Hamna!

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliongea bila utaratibu)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, mimi naomba nipewe nafasi nizungumze. (Kicheko)

SPIKA: Waheshimiwa namlinda Mheshimiwa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, naomba unilinde, inategemeana, mimi nimekaa na Wazungu sana, nimeishinao.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Kwa hiyo, huwezi kunidanganya, suala la kunawa mikono sio suala la kufundishana.

SPIKA: Mchungaji, Wazungu hawanawi wala hawaogi. (Kicheko)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, wananawa.

SPIKA: Mzungu anaoga mara moja kwa wiki. (Kicheko)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, kwa hilo nitawapinga.

SPIKA: Namlinda, namlinda jamani, endelea.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nachoweza kusema kama tunadhani kukabiliana na CORONA ni kunawa mikono tu peke yake tutakuwa tunajidanganya, kuna hatua za zaidi kama nchi tunatakiwa tuzichukue. Huu ndiyo wajibu wetu sisi kama Wabunge kui- task Serikali kwamba ni mipango gani ya dharura ambayo Serikali imeifanya.

Mheshimiwa Spika, takwimu nilizonazo mimi Tanzania nzima pamoja na kuwa na watu milioni 58 tuna ICU 38 in case tukipata matatizo, haya ni masuala ya kujadiliana hapa tupewe ripoti. Kama nchi nzima tuna ICU 38 …

MBUNGE FULANI: Vitanda.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, vitanda 38, kama ugonjwa huo…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Afya nimekuona.

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, nalazimika kusimama kwa sababu mchangiaji ambaye anachangia sasa hivi anapotosha sana na nataka nimpatie taarifa za kitaalam tu kabisa. Corona Virus ambaye ni COVID19 ukuta wake umetengenezwa na mafuta na sababu ni silaha ya kutosha ya kuki-destroy kirusi hiki. Hatutoi hizi taarifa kwa ajili tu ya kuudanganya umma, sabuni na maji tiririka ni silaha ya kutosha kabisa kukiuwa kirusi cha Corona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini la pili, muongeaji ambaye ametoka kuongea sasa hivi anasema Tanzania tuna vitanda 38 vya ICU. Hospitali ya Muhimbili peke yake ina vitanda zaidi ya 40, hizo taarifa anazitoa wapi? (Makofi)

SPIKA: Ni taarifa tu hiyo Mchungaji kukuweka sawa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nadhani tunajaribu kukimbia hoja ya msingi tunayoijenga hapa. Nimesema sipingani na masuala ya kunawa na sabuni zilizowekwa barabarani na kwenye maeneo mengi. Nimesema kama tunadhani tutaondoa Corona kwa sabuni tunazonawa tunajidanganya. Hoja ya Corona ni zaidi ya tunavyodhani na ndiyo maana nchi za wenzetu zimeamua kuwatoa watu wake Barani Afrika. Jana nilikuwa nasikiliza Al- Jazeera wanasema ndani ya wiki tatu ugonjwa huu tutaanza kuyaona matokeo yake katika Bara la Afrika kwa sababu measures tunazochukua haziendani na tatizo tulilonalo, hili ni tatizo kubwa. Bunge saa hizi hapa tunajadili bajeti as if hakuna chochote kitakachotokea.

Mheshimiwa Spika, Spain na Italy walipuuza kwa sababu waliona hilo suala halitawafikia, lakini mtu yeyote mwenye busara anajiandaa kabla ya vita. Tunachozungumza hapa ni kutaka kufahamu ni kwa kiwango gani tumejipanga. Wakilipuka wagonjwa laki moja hapa tutawalaza wapi? Hayo mambo tunatakiwa Serikali ituambie. Haya masuala ya kusema kuna vitanda 40, nyumba za ICU ziko 38, huwezi kukataa hiyo hatuna ICU za kutosha hapa. Mimi ndiyo nasema Serikali ituambie incase wakizuka wagonjwa laki moja tutawaweka wapi kama nchi? Serikali muwe na majibu hapa, hamna majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini la pili, consenquences za ugonjwa huu zina athari za kiuchumi. Wewe ni shahidi, sekta ya utalii kuna direct employment zaidi ya milioni moja na laki tatu au laki nne ambao sasa hivi hawana kazi na wengine wanaathirika, sekta ya utalii karibu watu milioni mbili hawako kazini kwa sababu hamna kazi. Hoteli zimefungwa, Zanzibar kule zaidi ya hoteli za kitalii 250 zimefungwa, Bara zaidi ya hoteli 250 zimefungwa, these are the issues tunatakiwa tu- discuss hapa, revenues mtakusanya kutoka wapi? Utalii unaingiza 25% ya forex, hiyo forex inatoka wapi? 25% ya forex katika nchi siyo kitu kidogo, haya ndiyo mambo tunatakiwa tuyajadili hapa, sio stories. Serikali ituambie ina mpango gani tuweze kuishauri. Hili ndiyo Bunge tushauriane hapa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MBUNGE FULANI: Anza wewe kutoa ushauri.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, kuna watu katika industry hiyo wamekopa…

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika,
taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Serikali haijatuambia ime-negotiate vipi na mabenki…

SPIKA: Mheshimiwa Mchungaji, namwona Mheshimiwa Waziri wa Nchi amesimama.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika,
naomba tu kumpa taarifa Mheshimiwa Msigwa kwamba, kwanza anapoona hali hii ya mwenendo wa Corona tunavyokwenda nayo inaonesha dhahiri shahiri ni kwa namna gani Serikali imejitahidi na iko kazini. Naomba tu nimwambie Mheshimiwa Msigwa ili tuweze kuwa pamoja, huu ndiyo muda muafaka nadhani badala ya kuendelea kulaumu ilikuwa ni fursa kwake…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika,
ilikuwa ni fursa kwake na yeye kutushauri kwa sababu tumeshapokea maagizo yako kwamba hata sisi tutakuja kama Serikali na umetuambia tutoe taarifa mbili; taarifa ya mwenendo mzima wa tatizo la Corona na tatizo la mafuriko nchini. Sasa anaposimama ajue sio kwamba Serikali imekaa tu ila tungefurahi sana Mbunge atushauri kuliko kulaumu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba tu nimpe taarifa kwamba tunajiandaa, hili ni tatizo la dunia. Hata huko anakosema Ulaya hata ICU za Ulaya hazitoshi na wao wana shida hiyohiyo. Kwa hiyo, kila mtu anapambana na Corona kwa mazingira aliyonayo na kwa namna anavyoweza kukabiliana nayo. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Msigwa unapokea taarifa hiyo?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, mimi hapa silaumu. Serikali yoyote duniani ipo kwa ajili ya kulinda uhai wa raia wake, that is a paramount, hicho ni kitu cha kwanza. Wao hapa waje na mpango kwamba jamani wakilipuka wagonjwa elfu hamsini tumepanga hivi, Wabunge mnatushauri nini? Waje na plan, tuko vitani hapa. Waje na plan Wabunge tuwashauri, wamekaa kimya muda unaenda, tunavyoviona tu ni visabuni huko barabarani, ndiyo hicho nachozungumza.

Mheshimiwa Spika, tunazungumzia uchumi hapa, kuna wafanyabiashara wamekopa benki, Serikali haijatuambia…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)