Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimechangia kwa kuongea na malizia point yangu ya mwisho ambayo muda haukutosha. Naishauri Serikali kule bandarini iweke single receiving point ya mafuta, faida kubwa ya hii kwana hupunguza dermrage charges, ambayo humpunguzia mzigo muagizaji wa mafuta au mfanyabiashara wa mafuta.Vilevile itampunguzia gharama mlaji ikiwemo gharama za kuendesha viwanda zitaungua. Serikali pia itapata faida endapo tukipunguza dermrage change ambazo zinaingia kwenye gharama ya uendeshaji kwa mfanyabiashara wa mafuta ambayo inaathiri mapato ya Serikali kwa maana ya corporate tax.

Mheshimiwa Naibu Spika, single receiving point ya mafuta hii itaondoa utunzaji wa mafuta kwenye matanki ya makampuni binafsi kuwepo unafuu wa upotevu wa mafuta kwa 3% mpaka 5% kitu ambacho hupunguza mapato ya Serikali sababu wafanyabiashara wa mafuta wanaingiza kwenye gharama za uendeshaji ambazo zinaenda kuathiri corporate tax. Kwa kuwa hii ni sheria watu wanataka advantage kukwepa kodi.