Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwa sababu mimi naongea pole pole, nimeomba wakubwa zangu waniongezee dakika kidogo. Naomba nizungumzie bajeti hii ambayo ni nzuri sana inayoendana hasa na ile vision yetu ya 2025. Vision 2025 ndiyo the plan. That is the plan, lakini hii vision imekuwa cascaded into strategic plan za miaka mitano. Tumeanza na kujenga misingi. Sasa hivi tunajenga uchumi wa viwanda ili tuende kwenye uchumi wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunapojenga uchumi wa kati we must sacrifices, kwa sababu hapo unachukua decision nzito na kubwa zinazokuwezesha kumlisha ng’ombe ili baadaye uanze kumkamua. Watu tunaanza kulalamika kwa sababu tulikuwa tumezoea ule uchumi tunaotaka kuondokana nao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Rais wetu, ana long vision and wide. Nawaomba sisi ambao tumepewa nafasi za kumsaidia tuelewe anachofanya, nasi tuwe na long vision and wide ili tumsaidie sasa kuhakikisha kwamba tunafika kwenye huu uchumi wa kati. Hizi strategic plans za miaka mitano zinakuwa again cascaded into yearly operation plan. Hizi operation plans ndizo plans tunazoletewa sisi hapa kuziangalia. Hizi yearly operation plans ndiyo zinatuwezesha kutengeneza bajeti. Hii bajeti ina-support sasa kuweza kutekeleza hii miradi tuliyo nayo. Nafurahi sana kuona jinsi ambavyo tunakuwa na big project. Hizi big projects zimelenga kuhakikisha kwamba huu ndiyo ulishaji wa ng’ombe ili anenepe tuweze kupata maziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mafanikio makubwa ambayo tumeyapata na hii sasa nianze kutoa ushauri kwa Serikali yangu. Cha kwanza, naishauri Serikali yangu iendelee kutoa elimu bure na kuwalipia wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu ambao wanapata sasa hivi mikopo yao bila matatizo. That is how you think big na unatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya mafanikio hatuyaoni, tunapiga kelele tu, lakini mafanikio ni makubwa sana kwa sababu hii ni mojawapo ya pillar ambayo inatuwezesha kwenye education tuwe na wanafunzi, tuwe na watendaji watakaokuwa ni wa kwetu tuliowajenga kwenye vyuo vyetu. Tumetoa hela zetu kwa ajili ya watakaokuja sasa kufanya kazi kwenye viwanda vyetu. Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Elimu, anasimamia vizuri na hapo kwa kweli siwezi kusema sana pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuko kwenye umeme; niseme ukweli, hata kama wasio na macho wanaona, mabadiliko ni makubwa sana. Maendeleo ambayo yamepatikana kwa kuweka umeme vijijini yanaonekana, watu wote wanaona. Watu ambao sasa hivi wamekuwa active na wamekuwa knowledgeable kwa kutazama hata TV tu hizi ndogo, wanachomelea, wanaendelea kujipatia kipato kutokana na umeme kufika vijijini, lakini wengi wetu ambao tumekuwa na narrow mind na short vision hatuyaoni hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye health. Wananchi wetu wakiwa na afya kwanza watafanya kazi lakini zitakuwa ni resources za kununua product zetu ambazo sisi tunazizalisha. Ukiwa na wananchi wenye afya njema, wanafanya kazi, wanajipatia kipato, utaweza kuzalisha katika viwanda vyako na wananchi wataweza kuwa na vipato hivyo waweze kununua hizo mali na uchumi utakua.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba ndugu zangu ushauri tu wa health pamoja na vituo vya afya vizuri tunavyovijenga, dispensaries, hospitali zetu za Wilaya ambazo zinaonekana, Hospitali za Rufaa katika mikoa yetu ambazo zinaonekana, sasa tujikite kuwa na wataalam waliobobea na kuweka mfumo mzuri hao wataalam waliobobea waungane na utafiti wa wagonjwa. Pale mgonjwa anapoingia hospitalini isichukue muda mrefu kupimwa na kujua afya yake na kumwezesha aweze kutibiwa ili atoke haraka hospitalini aende kuendelea kuchapa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika na Watanzania wenzangu, niliseme hili linalotusumbua sana. Huko nyuma tulizoea sana kupata hela za magumashi, sasa hivi fanya kazi ndipo upate hela, bila kazi huwezi kupata hela. Ndiyo sababu imeandikwa hata kwenye vitabu vyetu vya dini, asiyefanya kazi na asifanye nini? Asile. Tufanyeni kazi, mambo ni mazuri, yanaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije la mwisho sasa katika ushauri wangu, good governance. Hili ni eneo ambalo kwa kweli tunahitaji kuongeza nguvu, ndilo linalotusababisha tusi- perform katika baadhi ya sekta. Tunahitaji tuhakikishe kwamba kila usimamizi, kila senti inayopatikana, ni senti ambayo inaenda kuzalisha au kutumika kama ilivyokuwa imepangwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika upatikanaji wa resources hizi za pesa, ziko za aina mbili; pesa zetu na pesa za misaada. Pesa zetu zipo za aina mbili; zile tunazokusanya kodi na zile tunazokopa. Tunapokopa pesa ni za kwetu, maana mbeleni tutazilipa kwa kutumia zile tulizokusanya. Kwa hiyo, tunapopata mkopo tuhakikishe ule mkopo tunautumia vizuri, tusiwe na hali ya kwamba tunawekewa masharti, unajikuta zile pesa nyingi zinarudi tena kwa yule aliyetukopesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe mfano mzuri tu kwa ndugu zangu wa Wizara ya Maji. Pale Wizara ya Maji kuna matatizo, maana kutokea Awamu ya Nne kulikuwa na mradi wa kutoa maji Ruvu kwenda Kimara. Kulikuwa na mradi wa Ukerewe, sasa hivi tuna mradi wa kutoa maji Shinyanga kwenda Nzega, Igunga na Tabora; na sasa hivi tuna mradi huu unaoitwa wa Wilaya 29, una matatizo. Kwa sababu pale kuna Mhandisi Mshauri ambaye kwa miradi yote niliyoisema ameshiriki na kushiriki kwake hakina tija sana kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba, nitakuletea makaratasi ambayo yanazidi kiasi hiki uipelekee Serikali ijue kwamba Watanzania wanajua, wanaelewa; na nini kinachoendelea. Maana mimi nilifikia hatua maana mimi nilifikia hatua nikaenda nikatafuta, huyu Mhandisi Mshauri, ofisi zake ziko wapi?

Ukiona mahali ofisi zake zilipo ndipo hapo itabidi ofisi yake iwasiliane na Serikali, hatutakuwa na muda tena wa kuona tunafanya yale yaliyotokea wakati wa Symbion, wakati wa Lugumi, wakati wa IPTL, haya yatakuwa mabaya zaidi kwa jinsi nilivyoona na nilivyosoma. Nitakuletea hayo makaratasi uyasome pamoja na Serikali itayarishie kwamba hapo mambo siyo mazuri maana tuna umeme, tuna nguvu kazi, tutawezaje kuwa na viwanda vinavyofanya kazi kama havipatiwi maji? Maji ni resource kubwa sana katika uendeshaji wa viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunivumilia, naunga hoja hii mkono asilimia 100. (Makofi)