Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hon. Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, mimi naanza kwa kutoa pole kwa ule mradi wa kupima vipande vyote vya radhi Wilaya ya Ulanga, Kilombero na Malinyi, natoa pole nyingi sana kwa misimamizi wa mradi huo, Kijana wetu Machabe chini ya Wizara hii ya Ardhi kwa kifo kilichotokea kwa vijana wadogo kabisa tisa; yaani huwezi kuamini. Sasa siku hiyo tulikuwa yunajipanga mimi na Lijualikali tumeitwa kwa RCO, lakini tukapata habari kwamba gari lililobeba wale vijana, tena walikuwa wanakwenda kukabidhi hati za kimila, likaingia kwenye kidaraja (Korongo) yaani huwezi kuamini. Wengine baba mmoja, mama mmoja wametumbikia mule, gari sijui iliapata matatizo gani, wakafa wale vijana zile na maiti ukiangalia haki ya Mungu unaweza ukatiririka machozi mwili mzima.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo natoa pole sana kwa Wizara, kwa waru wa mradi, kwa wazazi kwa hiyo hali iliyojitokeza pale Kilombero-Ifakara. Ingawaje Mkuu wa Mkoa alifanya siasa, huyo ndiye aliyeagiza twende tukawekwa ndani (lock up) kwenye msiba anasema kwamba Wabunge wenu wako wapi? Jamani msifanye mambo hayo; Mkuu wa Mkoa wa Morogoro; mimi nasikitika sana kama mama.

Mheshimiwa Spika, pili, mradi upo unaendelea lakini ule mradi haukwenda kutatua migogoro. Yaani kama aneo lenu kuna mgogoro ule mradi unawaacha unakwenda kupima ardhi nyingine, ndilo dhumuni la ule mradi. Sasa kuna maneo ambako kuna migogoro ule mradi hauwezi kwenda kutatua migogoro, labda sasa waunganishe kule kule kwenye Wizara hii na uipeleke timu ya kwenda kutatua migogoro pale migogoro inapotokea.

Mheshimiwa Spika, vilevile huo mradi tunaushukuru umekuja katika Wilaya hiyo lakini kwa hito Stiegler’s; wenzenu Stiegler’s imetuumiza nyie ingawa tunapenda huo umeme; kwasababu maeneo yote ya mashamba ambayo vijiji tulikuwa tunalima; maana vijijini kuna makazi, kuna maeneo wafugaji wako wengi kule kwetu na watu walikuwa wanalima lakini maeneo yale yote sasa yameingia kwenye Stiegler kwahiyo wafugaji hawana mahali pa kwenda. Kwahiyo kinachotokea ni nini hususan Jimbo la Mlimba ni migogoro kati ya wafugaji na wakulima, kwasababu vijiji vimebaki na maeneo machache hata kama yakipimwa hata kupanga namna gani tuweke wafugaji hamna, wakulima wenyewe wamekosa mashamba.

Mheshimiwa Spika, kwahiyo mimi ushauri wangu kwa Serikali, sasa kwa vile ule mpaka unawekwa na maliasili na nyinyi ardhi kule bonde uevu la Kilombero basi muone kwamba wale wafugaji walioko kule na wale ni binadamu jamani, wana ng’ombe kule, na wale wakulima ni binadamu. Hebu angalieni, kuna mapori mengi; kwa mfano, hapa Mkata, sijui ranchi hiyo ya Kongwa; mimi napitaga pale kila siku sijawahi kuona ng’ombe anavuka. Kwanini msiende mkawapimie wafugaji muwamilikishe yale maeneo hata kuwapangisha ili waoteshe majani waweke Ng’ombe wa kutosha wale wafugaji waliotoka kule bonde la Kilombero kuliko sasa hivi watu mpaka wanaendelea kupigana kule Kilombero hususani Mlimba?

Mheshimiwa Spika, kwahiyo, ushauri wangu; sawa mmewatoa, mmetutoa wakulima hamuwezi mkatuhamisha lakini wale wafugaji basi muwapatie maeneo kwenye hayo mapori, hizi ranch za taifa. Kongwa hamna hata ng’ombe lakini unaambiwa hapa usipite kuna ng’ombe wanavuka. Mimi tangu nianze Bunge lile la 10, la Mama Makinda mpaka sasa sijawahi kukutana na kundi la ng’ombe likivuka pale. Kama mimi mwongo ninyi Waheshimiwa Wabunge wote bisheni. Sasa ile ranchi pale inafanyakazi gani? Hebu fanyeni mpango ili wafugaji wapate maeneo pale, na wako tayari kulipa hela, kupanga na kuotesha majani, tufuge kisasa na tuone kuna ng’ombe; Mheshimiwa Spika mwenyewe unajua.

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ni kuhusu kitabu chake hiki, kizuri hiki maana alivyosema kuna mipango miji nikafurahia; nikasema Jimbo la Mlimba, Mji wa Mlimba tangu mwaka 1996 kama lilivyosema gazeti la Serikali umetangazwa kwamba unatakiwa uwe mji, lakini mpaka leo ni vijiji, Chita ni vijiji na Mngeta ni vijiji. Kuna takribani, hakuweka hapa iddai ya watu; lakini kwa sensa ya mwaka 2012 hiyo Mngeta tu yenyewe ilikuwa na watu karibuni 19,000 sasa hivi wako wangapi na jinsi watu walivyohamia, kengele hiyo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: …lakini Mlimba nayo ndiyo Makao Makuu ya Wilaya lakini mpaka leo eti ni vijiji. Nimeongea na Mheshimiwa pale wa TAMISEMI anasema hatupandishi, lakini miji kule inaanza kuwa hovyo hovyo kwanini mnatufanyia hivi? Tupeni hata miji midogo ili tupange miji yetu uongo, kweli? Na hizo hela anazokusanya za ardhi hazirudi kwenye Halmashauri, kaulize Halmashauri zako hizo hela zinazokusanywa kwenye ardhi zinarudi kwako? Mimi sijawahi kuona, mimi niko kwenye Kamati ya Fedha, sasa Halmashauri itapimaje? Na hao wataalam hawana magari, hawana chochote, wapo wapo tu. Kwahiyo hebu wezesheni ili tupoate mafuu katika maisha.

Mheshimiwa Spika muda umekwishaee!

SPIKA: Umeshakwisha Mheshimiwa

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. (Kicheko)