Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja na ninapenda kupongeza juhudi kubwa za viongozi wote kwa mbinu mbalimbali inazofanya kuongeza ujio wa watalii nchini. Aidha, ninapenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, bado naleta hoja ya kuruhusu vipepeo hai viruhusiwe kwenda nje kibiashara na kitalii hapa nchini. Vipepeo ambao wanavunwa na kutunzwa na baadhi ya wananchi wangu maeneo ya amani ingewaongezea kipato. Aidha, ni ubunifu wao binafsi; sasa ni ubaya gani wanaofanya wa kupeleka nje ya nchi kwa biashara? Nchi nyingine wanafanya hiyo biashara. Vipepeo si hao wanyama kama ambao Serikali imefanya vizuri kuzuia. Nashauri leteni hiyo sheria Bungeni ifanyiwe marekebisho kwenye maeneo kama haya ya vipepeo. Haileti mantiki kulinganisha vipepeo na faru n.k.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaishukuru Wizara kwa juhudi kubwa (TFS) inazofanya kumaliza tatizo la wananchi wa Derema (1,028) ambao walihamishwa katika hifadhi. Kwa sasa tunamalizia wachache waliobakia kuwapatia ekari tatu tatu ila bado wanalalamikia wapunjo ya fidia ambayo bado hayajashughulikiwa. Naomba suala hili lishughulikiwe ili kuondoa haya malalamiko. Uhakiki na taarifa nzima ilikwishatumwa hapo Wizarani. Pamoja na Naibu Katibu Mkuu kuja na kufanya kikao na wahusika, bado tatizo hilo halijatatuliwa, naomba lipewe umuhimu tumalize hili tatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muheza tuna sehemu nzuri ambayo watalii wameanza kuja kwa wingi sana, sehemu ya Magoroto. Ni muhimu sasa hivi wataalam wa Wizara watembelee eneo hilo washauri namna bora na hatimaye waliingize kitaifa kama ni moja wapo ya vivutio hapa nchini kupata matangazo mengi.