Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na Maduhuli ya Madeni ya Nyuma ya Ada na Leseni za Magari, Riba na Adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na Maduhuli ya Madeni ya Nyuma ya Ada na Leseni za Magari, Riba na Adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nipende tu kusema kwamba kama Mheshimiwa Godbless Lema alivyosema kwamba Serikali imeanza lini kuwa tabia nzuri, naona hii itakuwa ni mwendelezo wa tabia nzuri. Niseme tu kwa kifupi kwamba, kuna maeneo mengine kwenye magari ya Serikali mengi ambayo yamekaa hayajaletwa kufutwa hapa yanaozea kwenye yards.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna dawa ziko kwenye bohari zetu ambazo zime-expire hazijaletwa. Kwa hiyo nimshauri tu Mheshimiwa Waziri kwamba wafanyie kazi ili walete mapema yale maeneo yote ambayo CAG amezungumzia ambayo hawajaleta kwenye Bunge yafutwe ili hoja zisiendelee kujirudia rudia. Ahsante sana. (Makofi)