Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo

Hon. George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia hoja hizi zote tatu. Nawapongeza Wenyeviti pamoja na Wajumbe wa Kamati zote tatu kwa kazi nzuri wanaliyofanya, kwa sababu wao ndio wanaoichambua bajeti na ndio wanaoikagua hii miradi. Mimi ni mjumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, Manaibu Waziri na TAMISEMI kwa kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAMISEMI wamejenga sasahivi vituo vya afya takriban 300, hospitali za wilaya takriban 69. Maeneo hayo wananchi walikuwa wanapata shida sana matibabu, lakini kwa sababu hivi vituo vya afya vimejengwa kwa hiyo huduma za afya zitaboreka. Kwa mfano akina mama wajawazito walikuwa wanapata shida wanafuata matibabu mbali, wataalamu walikuwa wachache, lakini kwa ujenzi wa hivi vituo vya afya mimi nina hakika, kwa sababu katika vituo vya afya hivi madaktari bingwa na manesi watapelekwa, kwahiyo hata operation ndogondogo zitafanyika kule. Kwa hiyo, niipongeze sana TAMISEMI kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala la MKURABITA, kwanza nianze TASAF. TASAF imeanza mwaka 2002 au 2003, imefanya kazi nzuri; TASAF awamu ya kwanza na ya pili walikuwa wanajenga shule, barabara, pamoja na zahanati, lakini TASAF awamu ya tatu ni kusaidia kaya masikini. Wale ambao hawana uwezo kabisa kwa hiyo, ndio wananufaika na Mfuko huu wa TASAF. Ombi langu kwa Mheshimiwa Waziri ni kwamba huu Mfuko wa TASAF unufaishe wananchi ambao hawana uwezo, wasije wakaorodhesha majina ya watu ambao wana uwezo, itakuwa si jambo jema sana kwa sababu, lengo la Mfuko huu wa TASAF ni kuboresha au kunufaisha wale watu ambao wana hali za chini sana. Tumetembelea baadhi ya mikoa na tumewaona watu wamenufaika sana na Mfuko huu wa TASAF. Wamejenga nyumba, wanapeleka watoto shule, wanapeleka watoto kwenye vituo vya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, MKURABITA imefanya kazi nzuri sana. Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais hata juzi alikuwa kwangu pale Mpwapwa, tulikwenda Kijiji cha Izomvu na wamepewa Hati Miliki za Kimila. Zamani vyombo vya fedha walikuwa hawazitambui hizi Hati Miliki za Kimila, lakini nashukuru sana na niwapongeze NMB, NBC pamoja na CRDB, wamezitambua Hati Miliki na wanatoa mikopo kwa hawa watu ambao rasilimali mashamba yamerasimishwa, kwa hiyo, wanapata fedha wanaboresha maisha yao. Ushauri wangu ni kwamba, wale wananchi ambao wanapata mikopo watumie fedha hizo kwa kuboresha maisha yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni kuhusu sheria ndogo. Mimi nampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo. Ombi langu ni kwamba, wazishauri au waziagize halmashauri zote kwa sababu, Halmashauri zimeundwa chini ya sheria kwa hiyo, waendeshe vikao kufuatana na utaratibu, sheria na kanuni. Kuna baadhi ya Halmashauri wanaendesha vikao bila kufuata kanuni. Wawe na Standing Orders kila Halmashauri itumie Standing Orders kuendesha vikao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya nashukuru sana. Na nirudie kumpongeza Waziri wa TAMISEMI kwa kazi nzuri pamoja na Naibu Mawaziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja zote tatu, asante sana.