Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019

Hon. George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019

MHE GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hoja hizi mbili. Kwanza kabisa nizipongeze hizi Kamati zote mbili, niwapongeze Wenyeviti pamoja na Wajumbe kwa kazi nzuri kwa sababu hawa ndiyo wanaochambua bajeti ya wizara zinazohusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie hasa masuala ya barabara, barabara ya kutoka Mpwapwa kwenda Kongwa ni barabara muhimu sana na nashukuru katika Bajeti ya mwaka 2019/2020 walitenga fedha kidogo kwa ajili ya kuanza kutengeneza kwa kiwango cha lami. Pamoja na kwamba ni fedha kidogo lakini nina uhakika bajeti ya Mwaka 2020/2021 Wizara ya Ujenzi watapanga fedha za kutosha kwa ajili ya kutengeneza barabara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni muhimu sana na inawezekana hata wewe Mwenyekiti umewahi kupita barabara ya kutoka Kongwa kwenda Mpwapwa. Barabara hii ndiyo inayotumika na wakandarasi Waturuki wanaotengeneza reli ya kati SGR sasa mitambo yote mikubwa, malori yote makubwa, yanapita katika barabara hii. Kwa hiyo, naomba sana Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Wajumbe, wakati wa kuchangia bajeti ya 2020 naomba sana mzingatie hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni barabara ya kutoka Gulwe – Berege – Chitemo – Mima – Igojimoja – Isalaza – Chitope. Barabara hii iko chini ya TARURA na ni barabara muhimu sana, niliomba barabara hii kwa sababu TARURA hawana uwezo, bajeti yao ni ndogo sana, hawawezi kuifanyia matengenezo makubwa barabara hii yenye urefu wa kilometa 58. Niliomba TANROADS wachukue kwa sababu TANROADS ndiyo wenye fedha za kutosha kuweza kuitengeneza barabara hii kwa matengenezo ambayo yanatakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, barabara hii inahitaji bilioni 1.6 ili iweze kufanyiwa matengenezo makubwa. Sasa naomba bajeti ya TAMISEMI mwaka 2020/2021 waifikirie barabara hii, waitengee bajeti ya kutosha. Lakini kutenga bajeti ya milioni 120 haitoshi kabisa! naomba zitengwe fedha za kutosha kabisa ili barabara hii kwa sababu barabara hii inahudumia wananchi wa kata 7 na ni barabara muhimu sana kwa maendeleo ya Wilaya ya Mpwapwa. Kwa hiyo, nilikuwa naiomba sana TARURA watenge fedha za kutosha ili barabara hii iweze kufanyiwa matengenezo makubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza haya, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia na naunga mkono hoja mbili zote. Ahsante sana. (Makofi)