Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika Wizara hii. Pili, napenda kuwapongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na wasaidizi wake wote kwa kuendelea na kuiwasilisha kwa ufasaha mkubwa hotuba hii. Hii ni Wizara muhimu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Kwanza ajira katika Jeshi letu, naipongeza Wizara kwa kuendelea kuchukua vijana wa nchi hii kwa mujibu wa uwezo na sheria ya nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika suala hili ni kuitahadharisha Wizara iendeleze umakini wa kuwapembua na kuwafahamu vyema vijana ambao wanawaajiri. Nchi yetu imezungukwa na nchi jirani ambazo baadhi yao zina matatizo yao na kukimbilia katika nchi yetu, vijana wa nchi hizi wanapokimbilia katika nchi yetu huwa wanajiingiza (wanaweza kujiingiza) katika jamii ya Watanzania na kuweza kujipenyeza kuweza kujiunga na Jeshi letu. Hivyo Wizara naiomba iendelee kuwa makini sana katika kuwachukua vijana na kujiunga jeshini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhana ya Jeshi la Wananchi; Jeshi letu limekuwa na kazi ya kulinda na kuhakikisha usalama wa mipaka yetu lakini Jeshi hili pia linapaswa kuangalia maeneo mengine ya kuweza kusaidia wananchi hasa katika nyanja za kiuchumi. Mfano maeneo yafuatayo yanaweza kusaidia kwa kutoa elimu ya kiuchumi kwa wananchi kama Kiwanda cha Ushonaji, Kiwanda cha Samani Chang’ombe ambacho hutengeneza samani, ufugaji wa samaki katika mabwawa na uvuvi. Maeneo hayo niliyoyaorodhesha nashauri Jeshi lipeleke ujuzi wake kwa wananchi ili na wao waweze kutumia ujuzi wa maeneo hayo kuweza kujikwamua kiuchumi .

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.