Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kulipongeza Jeshi letu kwa kazi nzuri wanayoifanya katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi. Katika nchi zilizoendelea duniani, nchi kama Marekani, bajeti ya ulinzi wa nchi hiyo ndiyo inayopewa kipaumbele cha kwanza katika bajeti ya nchi hiyo duniani. Kwa kuzingatia kuwa bila ulinzi na utulivu wa nchi maendeleo endelevu hayawezi kutokea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Tano, malengo yake ya msingi ni kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na ikizingatiwa kwa sasa kuna miradi mikubwa ya kimkakati ambayo itachochea uchumi wetu kwa haraka zaidi. Miradi hiyo ni kama ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme Rufiji, Mradi wa Reli wa SGR, ununuzi wa ndege mpya (ATC) na Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda - Hoima - Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hizo na nyinginezo, naomba Serikali ingeangalia upya upangaji wa bajeti kwa kuzingatia uhalisia na bajeti hiyo iongezwe maradufu. Jinsi maendeleo yanavyoendelea ndivyo wahalifu na wapinga maendeleo waongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi linahitaji fedha zaidi ili kujumuisha kiteknolojia (kiulinzi), mafunzo mbalimbali, kununua vifaa vya kisasa, mitambo ya kung’amua uhalifu, mafunzo ya ndani na nje ya nchi, ujenzi wa nyumba za askari, kuazisha viwanda, maslahi ya wanajeshi na mambo mengine ya kijeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, JKT iongezewe fedha ili iweze kuzalisha zaidi kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo katika makambi yake. Hii itasaidia kuwapatia ajira vijana wetu wanaohitimu mafunzo ya JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi liendelee kuongeza ulinzi kwa maeneo nyeti ya Serikali na pia Jeshi liimarishe zaidi ulinzi kwa viongozi wetu wakuu wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudi kumpongeza sana Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa Tanzania, CDF, Makamanda wote na Wizara ya Ulinzi kwa kazi njema ya kulinda nchi yetu. Mungu libariki Jeshi la Wannachi wa Tanzania. Amina. Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja 100%.