Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia kuhusu miradi ya Kimkakati ya Mchuchuma na chuma na Liganga.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda Wizara hii ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ieleze Umma kama ni kweli katika sehemu hii ya Liganga kuna aina ya madini (products) zinazojulikana kama Vanadium Pentioxide na Titanium ambayo vinatumika katika kutengeneza ndege kwa kuwa ni vyepesi (light) na hivyo kuwa na thamani kubwa ukilinganisha na Chuma? Pia, je, baada ya ku-extract madini haya, chuma kinaweza kuchukuliwa kama by product? Ni vyema jambo hili likaangaliwa kwa ukaribu zaidi ili nchi isije ikapoteza mali nyingi zinazotoka ardhini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Same, kuna madini mengi sana ya Jasi (Gypsum), maeneo ya Makanya na Bendera. Jasi huwa inatumika kutengenezea “POP” (Plaster of Paris), kutengenezea mabomba ya majitaka, ceiling boards, mbolea na sehemu nyingine inatumika kwenye Viwanda vya Saruji.

Mheshimiwa Naibu Spika, “Deposits” zilizoko maeneo tajwa hapo juu ni mengi kiasi kwamba kungeweza kuanzishwa viwanda takribani vinne hivi. Naishauri Wizara hii ya Viwanda, isaidie kutuma wataalamu maeneo haya ili kufanya uchunguzi juu ya deposits hizi za gypsum na uwezekano wa kuanzishwa viwanda hivyo kwa kushirikiana na Wizara ya Uwekezaji. Lengo ni kutekeleza Azma ya kuifanya Tanzania Nchi ya Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.