Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nachukua nafasi hii kukushukuru wewe kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia katika Wizara hii. Pili napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Biashara pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika na kuiwasilisha kwa umakini wa ufasaha na hali ya juu. Katika kuchangia hotuba hii ya Wizara ya Biashara na Viwanda napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Matrekta aina ya Ursus. Napenda kuipongeza Serikali kwa azma yake ya kuendeleza mradi huu wa matrekta, kama inavyojulikana kwa dhana ya kuelekea kwenye sera ya viwanda haiwezi kufanikiwa bila ya kuimarisha kilimo cha kisasa. Vitendea kazi katika kilimo moja katika hivyo ni matrekta. Hata hivyo, ni vyema Serikali ikatilia mkazo mradi huu. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 10 imeeleza idadi ya matrekta na idadi ya hekari zilizokwishalimwa uwiano wake ni heka 214.1 limelimwa kwa kila trekta moja. Hii ni idadi ndogo sana kwa nchi inayoelekea kwenye kuimarisha viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba Serikali ipunguze bei ya matrekta na kuondosha vikwazo vilivopo ili wananchi wengi waweze kumudu kununua matrekta hayo. Inaonekana kuwa bado bei ya matrekta sio rafiki kwa wakulima wetu. Tanzania ya viwanda itawezekana ikiwa miundombinu ya kuboresha kilimo ambayo ni pamoja na kupunguza bei za matrekta ni muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.