Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Ezekiel Magolyo Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, hususan Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini. Naomba kusema, naunga mkono bajeti hii kama sehemu ya kuunga mkono juhudi hizi za Mheshimiwa Rais na Serikali.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo, naomba yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, ujenzi wa barabara ya Kahama - Geita uanze. Kwa miaka mitatu mfululizo tumekuwa tunatenga bajeti lakini fedha hazitolewi na ujenzi hauanzi. Hii ni bajeti ya mwisho kabla ya uchaguzi mwakani, hatuna cha kuwaambia wananchi. Mheshimiwa Rais pamoja na Ilani kuahidi, pia aliahidi wakati wa kampeni mwaka 2015 na alipofanya ziara Shinyanga mwaka 2017, bado ujenzi hauanzi. Naomba sana, tuanze ujenzi hata kidogo ili tupate cha kusema mwakani.

Mheshimiwa Spika, pili, usanifu wa barabara za Kahama – Bulige – Solwe – Mwanangwa, Kahama - Nyang’hwale - Busisi, Kahama – Kaliua - Mpanda na Kagongwa – Itobo – Bukene – Tabora. Ukamilishwe haraka ili ujenzi uanze kama Ilani yetu ya CCM ya mwaka 2015/2020 ilivyoahidi.

Mheshimiwa Spika, tatu, ujenzi wa reli kwa SGR kati ya Dodoma – Tabora – Isaka - Mwanza utaanza lini?

Mheshimiwa Spika, nne, ujenzi wa reli ya kisasa Isaka - Kigali umefikia hatua gani?

Mheshimiwa Spika, nashukuru.