Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze moja kwa moja kuchangia ajenda hii muhimu sana, lakini nitaiangalia kwa mapana yake zaidi ya badala ya ufinyu unaoangaliwa na baadhi ya watu wengi na nitaiangalia katika upande wa uchumi nikizingatia zaidi balance of payment. Nataka nizungumzie ATC na SGR na kama nitapata muda nitakwenda zaidi katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukianza na ATC, nizungumzie kimapana katika uchumi hasa tukiangalia tourism. Kwa mwaka 2017 tourism iliingiza shilingi bilioni 2.25 sawa sawa na asilimia 27 ya total export zote katika goods and service kwa nchi yetu. Kwa mwaka 2018 iliingiza Dola bilioni 2.45 sawa sawa na asilimia 29. Sasa tukiangalia ATC, nini mchango wake na utakuwa mchango wake katika tourism?

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia sasa hivi, Kenya Airways inafanya safari tano kila siku kutoka Nairobi kuja Dar es Salaam na safari tatu kila siku kutoka Kenya kuja Zanzibar. Kwa nini wanafanya hivyo? Kwanini ATC isifanye hilo? Ni kwa sababu sisi tuliicha ATC. Sasa tuone umuhimu wa ATC katika kuchangia tourism katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapoangalia ATC kwa kusema kwamba watu wa Misungwi watapanda ndege, yaani nashindwa kuelewa, ni kufikiri kidogo sana. Tufikiri kiupana. Tukiangalia ATC pale itakapoanza kwenda katika far East kwamba iende India au China italeta watalii. Watalii watafika Dar es Salaam watachukuliwa watakwenda KIA, watakapofika KIA wale ndugu zangu wenye Land Rover, wale wenye Pick-up watawachukua watalii kufika karibu na Mlima Kilimanjaro.

Mheshimiwa Naibu Spika, watakapofika Mlima Kilimanjaro wale wananchi wa kawaida kabisa kule Kilimanjaro watakuwa wapagazi, watabeba ile mizigo ya watalii kwenda kupanda Mlima Kilimanjaro. Umemgusa raia wa mwisho kabisa na pale hujazungumzia ATC. Uone umuhimu ATC itakaosaidia katika uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuiangalie sasa ATC katika umuhimu wake regionally, halafu tutaangalia intercontinental inachangia vipi? Tutakapokuwa na ATC inaenda India ambayo ni shirika letu, maana yake sasa zile fedha ambazo zinachuliwa na mashirika ya nje kuleta watalii Tanzania zitakuwa zimeingia kwa ATC ambayo ni mali ya Watanzania na zitaongeza hilo pato kwenye tourism katika uchumi wetu. Watu hilo hatuwezi kuliangalia. (Makofi)

Mheshimiwa naibu Spika, siyo hivyo tu, tutakapokuwa tumetoka pale kwenye ATC, wale watalii watakapokuwa ni wengi zaidi wanakuja kwetu, pato la Taifa litakuwa limeongezeka zaidi. (Makofi)

Nawaomba ndugu zangu, badala ya kushambulia kununua ndege, tumpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu mwenye mawazo mapana. Anaona mbali zaidi, anaangalia kiupana zaidi lakini sisi tunaangalia kiufinyu kwa kuangalia ndege itabeba watu wa Misungwi. Hiyo siyo nia njema ya Rais wetu kuweza kuisaidia nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba Watanzania wote tumuunge mkono Mheshimiwa Rais wetu kwa kufanya kazi na kufikiri zaidi katika maeneo yetu. Tusianze kufikiri kidogo kidogo. Watanzania na ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, niwaombe sasa tuone ni kwa namna gani tunaweza kuisaidia ATC badala ya kuibeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi itaanza intercontinental flights, kwa maana itakwenda India na China kuleta watu zaidi, lakini biashara tunayoiangalia, tusiangalie utalii tu, tuangalie je, watu watakaotoka uwanja wa ndege watakuwa wametoka wapi? Sasa hivi kuna watu wanakuja pale Kariakoo kutoka Malawi, Zambia, Congo kufanya biashara. Sasa kama tutakuwa na ndege yetu ambayo itaifanya Kariakoo iwe ni Guangzhou ya Afrika, Guangzhou ya Afrika, maana yake ni nini? Maana yake utalii ambao unasababishwa na ATC utakuwa umeleta uchumi kukua zaidi katika nchi yetu. Kwa hiyo, tuangalie kwa mapana, tuache kuiangalia ATC kiufinyu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nishauri kwamba badala ya kuwa na hizi ndege chache ATC waangalia regionally, wa-focus zaidi sasa hivi, ndege hizi Air Bus ziwe ni za regional; ziende South Africa, Burundi, Rwanda, lakini wanunue tena ndege nyingine ambazo zitatusaidia sasa; hao watu wanaokuja kutoka kule watasambaaje katika nchi yetu? Kwa hiyo, waangalie uwezekano wa kununua ndege nyingine za aina hiyo kwa ajili ya local. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, International au intercontinental sasa hivi wameanza ku-focus kule Far East baadaye kwa mipango yao ya kati au ya jinsi wanavyoona waweze ku-focus Europe. Kwa hiyo, wanunue ndege nyingine kubwa zaidi ambazo ni sawa sawa na hizi Dream Liner ziweze kwenda Europe na sehemu nyingine. Vile vile, kwa baadaye zaidi tuweze ku-focus market ya Marekani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nisiishie hapo tu, kwa sababu ya muda niweze kuzungumzia umuhimu vilevile wa reli yetu katika transit trade. Again hii ni mawazo mapana ya Mheshimiwa Rais wetu. Mimi nampenda kwa sababu he think big na watu wengi tuna-think low halafu tuna-think very narrow hatumwelewi. Sasa niwaombeni, mimi nina-think big and I think wide, ndiyo sababu leo naamua kutoa shule hii muweze kuelewa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, transit trade tukiiangalia tuone ni kwa namna gani ita-contribute kwenye uchumi wetu. Tunaposema transit trade tunaangalia nchi zinazopakana nazo. Mimi nashangaa wakati mwingine hatuwazi namna gani tunaweza kuzitumia hizi nchi tunazopakana nazo kukuza uchumi wetu zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiwa na reli ambayo itatoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, Mwanza na pale Fela tukatengeneza Economic Zone, maana yake sasa mizigo itatoka moja kwa moja kwa haraka Dar es Salaam kwenda Mwanza. Ikisafika Mwanza pale, ndugu zetu wa Rwanda na Burundi watachukua ile mizigo kutoka pale Fela na kuweza kuisafirisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tutakuwa na Economic Zones, kwa mfano, tuwe na Economic Zone katikati ya Dar es Salaam na Dodoma ambapo tutakuwa na maeneo maalum ambayo biashara mbalimbali zitafanyika na tutaitumia hiyo reli sasa kusafirisha products zetu kwenda kuziuza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tutakuwa na Economic Zone nyingine, yaani business centers pale katika kwa mfano kati ya Dodoma na Tabora, maana maeneo yale sasa wakiwemo wafugaji, wakulima na wafanyabiashara wengi wakiwa na productions ambazo zinakwenda kwenye centre ambapo kuna businesses wanazozifanya, wasiwe na matatizo ya kuweza kusafirisha vifaa vyao au vitu vyao kwa ajili ya raw material kuja kufanya production. Waweze kupata usafiri wa rahisi na kitu kitakachoweza kutusaidia ni reli yetu hii. Kwa hiyo, Watanzania tuwaze na tuweze kufikiria namna gani hii SGR itatusaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka reliā€¦ (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kitwanga, muda wako umekwisha. Ahsante sana.

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Nina uhakika wale wanaojua upande gani nausema wamepata shule yangu. (Makofi/ Kicheko)