Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani zangu kwako kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Watendaji wake wote kwa kutayarisha na kuwasilisha hotuba ya Wizara yao kwa ufasaha zaidi katika Bunge lako hili. Katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza Wizara pamoja na Serikali Kuu kwa kuweka Baraza la Mitihani la Tanzania ambalo ni chombo muhimu sana katika Sekta ya Elimu. Hivi karibuni kumekuwa na matokeo ya mara kwa mara ya uvujaji wa mitihani katika daraja tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika suala hili ni kwamba, Wizara iendelee kuwa na makini mkubwa katika kudhibiti jambo hili. Wizara katika kutatua suala hili inabidi ilitafutie Baraza vitendea kazi kama magari ya kuweza kusafirisha mitihani kutoka Makao Makuu au sehemu moja kwenda nyingine. Tukiwa tunasafirisha mitihani hii kwa magari ambayo hayana uhakika, inatoa mianya ya kuvuja mitihani hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Naipongeza Wizara hii kwa kubuni na kuendeleza mradi wa ukarabati wa Vyuo vya Ualimu, mradi ambao ni muhimu kwa kuwatengenezea mazingira bora ya walimu. Walimu ni rasimali kubwa katika jamii, ni watu ambao wanatakiwa wafanye kazi kwa utulivu ili waweze kufundisha vyema kazi zao. Ushauri wangu ni kwamba, Wizara hii iendelee kuongeza ukarabati huu katika maeneo yote ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.