Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia suala la uhifadhi na uendelevu wa mazingira. Dhana hii ni pana na inajumuisha vitu vyote vinavyotuzunguka katika sekta mbalimbali kama vile maji, kilimo, nishati na kadhalika. Bado sekta hii ya utuzaji wa mazingira na uhifadhi haijapewa umuhimu na uzito unaostahili, kwani utekelezaji wake unakumbana na changamoto kadha wa kadha hasa upatikanaji wa rasilimali fedha zinazoendana na Ofisi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Iringa hasa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa sehemu kubwa ni kame kwa sababu ya matumizi mabaya ya mbolea ya chumvichumvi bila kufuata ushauri wa wataalam pamoja na kukata miti hovyo. Nashauri Wizara itenge fedha kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kupitia luninga, redio vipeperushi na wadau hususan Serikali za Vijiji na Vitongoji pamoja na sekta binafsi kueleza madhara ya uharibifu huo wa mazingira, ikiwemo Operesheni Kata Mti Panda Mti itengewe fedha pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifuko ya plastiki. Waziri Mkuu alivyokuwa akihitimisha hoja ya Wizara yake, alipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia miezi miwili ijayo. Hata hivyo, nitaomba Mheshimiwa Waziri wa Mazingira anavyohitimisha hoja yake aje na mbinu mbadala kuhusu vifungashio vitakavyotumika katika nchi yetu na namna watakavyoweza kuzibiti mifuko itokayo nje ya nchi yetu. Vilevile ashirikiane na wahusika wa viwanda vilivyokuwa vikitengeza mifuko hiyo ili kuona namna watakavyoshirikiana nao kufanya kazi mbadala kwa sababu ughafla wa taarifa hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kampeni ya upandaji miti. Katika Mkoa wa Iringa kuna ustawi wa miti, matunda na mboga mboga. Nashauri Serikali iweze kutenga fedha ili kusaidia kampeni ya upandaji miti ya matunda ambayo pamoja na kuhifadhi mazingira itasaidia wananchi kupata kipato na kuboresha afya zao. Kwa mfano, wananchi wakipatiwa miti ya miparachichi na apple (matufaa) itakuza sana pato kwa wananchi na kuhifadhi mazingira.