Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Asha Mshimba Jecha

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayofanywa na Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kasi na ufanisi mkubwa. Awamu hii tumeona miradi mikubwa inayofanywa kwa fedha zetu za ndani na kwa muda mfupi. Naamini uthubutu wa Mheshimiwa wetu, Watanzania tukiacha kufanya kazi kwa mazoea, tukiungana na mwendo kasi wa Rais wetu, muda mfupi ujao Tanzania itakuwa ya kupigiwa mfano kwa mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali kwa kuamua kukifanya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kihinga Mkoani Kigoma kuwa Kituo cha Utafiti wa Mbegu Bora za Chikichi. Ushauri wangu kwa Serikali, kupitia kituo chetu hiki kuangaliwe uwezekano wa kufanya utafiti kwa zao la tende kwa Mkoa wa Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zao la tende Dodoma, kwa mitende iliyopo inazaa vizuri sana na tende kiafya zina lishe nzuri. Hivyo, ni chakula kizuri kinacholiwa Tanzania kutoka nchi za Kiarabu. Kiufupi mitende Dodoma inazaa vizuri kuliko hata huko nchi za Kiarabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiujumla utafiti wa mazao mbalimbali unahitajika ili kuondokana na kilimo cha mazoea tulichokirithi kwa wazee wetu ili mazao yetu yawe bora na kuweza kuuza nje ya nchi na kutuingizia fedha za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaipongeza Serikali kwa hatua za makusudi za kunyanyua mchezo wa soka katika nchi yetu na tumeshuhudia timu zikifanya vizuri ndani na nje ya nchi, pamoja na mchezo wa ngumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali na soka, pia tuna michezo mingi ambayo ikiangaliwa ipasavyo na kupewa msukumo nayo inaweza ikaitangaza nchi yetu na kuiletea faida kubwa. Hivyo ni vyema Serikali kupitia Wizara ya Michezo kukaa na vilabu vya michezo mbalimbali kuona mipango yao ili kuweza kuandaa mikakati ya kunyanyua michezo hiyo, mfano, netball, riadha, basketball, volleyball na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaipongeza Serikali kwa maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2020. Sambamba na hilo, nashauri upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa vya Mtanzania, kwani vijana wengi waliotimiza umri wa miaka 18 bado wanahangaikia vitambulisho. Hivyo hawajapatiwa na bila ya kitambulisho huwezo kuandikishwa kwenye Daftari la Wapigakura.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.