Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. SAADA M. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii na naunga mkono hoja za Kamati zetu mbili ambazo zimewasilishwa hapa na tunaendelea kujadili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mchango wangu leo kwanza nataka nitumie forum hii ya Bunge kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na Baraza lake la Mawaziri kuona umuhimu mkubwa uliopo wa kuondosha tozo ya Ongezeko la Thamani kwa umeme ambao ZECO wananunua kutoka TANESCO. Tunashukuru sana sana na kutokana na jambo hili tunaona spirit kubwa iliyopo katika Serikali ya Awamu ya Tano kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo katika Muungano wetu. Kwa hivyo, tunamshukuru sana na naamini Wazanzibari wamefurahi sana kwenye hili na wanaishukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na shukurani hizo, vilevile naomba kuzishukuru Kamati zetu za Bajeti na Kamati yetu ya Nishati na Madini kwa sababu kwa pamoja walitoa uzito mkubwa kuona kwamba Serikali inalitatua tatizo hili kwa haraka zaidi. Tunazishukuru sana Kamati hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee, naomba nitoe shukurani hizi kwa Mheshimiwa Spika kwa sababu alipobaini jambo hili hakusita kulipa uzito unaostahiki na hatimaye limekwenda kutatuliwa. Tunawashukuru sana pia Wabunge wote ambao walikuwa wamelichangia jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na VAT, kiukweli VAT ni jambo moja dogo katika mambo mengi ambayo yanaikabili Shirika letu la Umeme la Zanzibar (ZECO) wakati linaponunua umeme kwa TANESCO. Lazima nikiri, Waziri wa Nishati na Naibu wake wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana na kwa nia hasa ya dhati inaonekana. Nikiongea na Mheshimiwa Waziri ananipa commitment ambayo inatoka kabisa moyoni kwake kwamba wanajitahidi kuhakikisha hata zile gharama nyinginezo ambazo zimeonekana ni mzigo mkubwa sana kwa ZECO ambazo zinakwenda kwa wananchi wanaotumia umeme kule Zanzibar, amekuwa akinipa comfort na commitment ya hali ya juu. Tunataraji sana, sana, sana hili jambo litafanyika kwa uharaka zaidi ili kuona kwamba tunakwenda kupunguza ule mzigo wa gharama ya umeme ambao unanunuliwa na ZECO kutokea TANESCO. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo hili nadhani tunapata mafunzo ya mambo mawili; kwanza ni kuhakikisha ama ni kuona kwamba hata katika zile sekta ambazo hatuzioni ni za Muungano lakini tunajua katika utekelezaji wa activity zetu zina athari katika pande mbili za Muungano. Kwa mfano, kama utaangalia tozo hizi ambazo zinatozwa utaona kwamba Zanzibar wanaweza tu wakanunua lakini kuna athari kubwa katika upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano ambapo vilevile kuna wananchi wa Tanzania nao wanatumia. Kwa hivyo, hilo ni funzo moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini funzo la pili, ni kuona ushirikishwaji wa taasisi zetu hata kama siyo za Muungano. Kwa vile tuko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna umuhimu mkubwa hata katika sekta zile ambazo siyo za Muungano kufanya kazi kwa pamoja ili kuona kwamba hali hii ambayo inaweza tu ikatokea ikaleta mgogoro somewhere inaondoka. Kwa hivyo, hata tunapokwenda katika bajeti tunaomba consideration ya taasisi ambazo zinafanya kazi zinazofanana zifanye kazi kwa pamoja ili kuona kwamba manufaa yanayopatikana yanakuwa ni ya pande mbili za Muungano. Tunaipongeza sana Serikali, tunampongeza sana Mheshimiwa Waziri, tunampongeza sana Naibu Waziri kwa sababu tunaona kwamba ile commitment ni ya dhati kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati imeoimba sana Serikali kuona ule mchakato ama yule consultant ambaye anafanya kazi ya kuangalia gharama nyinginezo aweze kuharakisha. Vilevile tunapokwenda huyo consultant, of course, amepewa terms of reference lakini nadhani hajui kwa dhati jinsi gani hasa hasa hizi sekta mbili zinavyofanya kazi yaani sekta moja lakini katika pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, pengine ingewezekana sisi kama wananchi ama watu wetu wa ndani hata kama ni consultant awe ni mtu wa ndani ambaye anajua kiundani operations za Serikali zetu mbili. Kama tunatafuta mtu mwingine ambaye hata hajui operation yenyewe inavyofanya kazi hataweza kujua kiundani tatizo lililopo na yeye ataangalia katika business level. Hiyo inaweza kabisa kuleta utata katika mapendekezo ambayo atayatoa na pengine sana azimio ambalo tumeazimia lisiweze kufikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna doubt kwamba umeme ni nyenzo kubwa sana katika uchumi wa Taifa hili. Kwa upande wangu unajua sometimes unaweza ukawa unashangaa mtu anapinga mradi wa umeme kwa mfano wa Stigler’s Gorge. Sasa hivi Tanzania tuna uhaba wa umeme na Serikali inafanya initiatives kwa ajili ya kutafuta umeme. Wenzetu pengine walioko nje ambao kwa namna moja ama nyingine wanahisi kutakuwa kuna maslahi wao wanaangalia katika aspect ya mazingira lakini tunaojua hitaji hasa la changamoto hii ni sisi Watanzania. Kwa hiyo, kwenye suala kama hili la kitaifa tukiacha tofauti zetu za kisiasa na kimtazamo, nadhani kuna umuhimu mkubwa wa kui-support Serikali yetu kwenda kuangalia jinsi gani tunaweza kupata umeme wa uhakika na wa kutosha ili kuona kwamba uchumi wetu unapaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tukiangalia tuko katika tuko hiyo development stage tukiwa tunaangalia uchumi kukua, tunakua katika kiwango ambacho bado hatujakua vizuri lakini kinaweka miundombinu ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa uchumi wetu uweze kubeba development za watu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo tunaomba wenzangu hata katika maeneo kama haya ya kitaifa ni lazima tuwepo pamoja na ni lazima tuungane pamoja tuone kwamba tunai- support Serikali kwa nguvu zote kuona kwamba inakwenda kutekeleza jambo hili. Mtu mwingine atakuwa anaangalia kwa mawazo yake mengine, of course tunajua kwamba kuna choice baina ya ukuaji wa uchumi na mazingira, lakini sisi kwa sababu ni Taifa ambalo linaloendelea tunahitaji development, tunahitaji uchumi wetu ukue, lazima choice tuangalie lile ambayo utaleta impact kwa wananchi wengi walio maskini rather than kuangalia hasara kidogo ya upande mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naipongeze sana Serikali na tunatarajia kwamba hizi process ambazo zinaendelea zinakamilika kwa haraka zaidi ili kuona kwamba stiegler’s gorge project ile inafanikiwa na tunataka kuzalisha umeme ili umeme ufaidishe wananchi mmoja mmoja. Naamini the more umeme utakapokuwa unapatikana Tanzania Bara pengine inawezekana hata ile multply effect ikaenda mpaka Zanzibar. Kwa hiyo, kwenye suala la maendeleo hakuna budi lazima tuungane kwa pamoja, tuone kwamba hili jambo linapatiwa ufumbuzi wa haraka na tunaweza kufaidi matunda ya uhuru wetu kama vile ambavyo tumekusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Serikali vilevile kuona kuna umuhimu wa kuanzisha Balozi kule Cuba. Hili suala nadhani tumelisema sana humu ndani na limejadiliwa kwa mapana, lakini kwa sababu Serikali yetu ni Serikali sikivu imeona kuna umuhimu sana wa kufungua ofisi kule Cuba na tunatarajia sana mafanikio yale ambayo tunayo sasa yataendelea kuleta athari chanya zaidi katika uchumi wetu kutokana na kazi ambazo Balozi atakuwa anazifanya kule Cuba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)