Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa nafasi. Kwanza nianze kabisa kwa kuipongeza Serikali kwa mpango huu ambao kwa kweli umeendana na Vision yetu 2020-2025 ambayo tumeikatakata katika vipingili vya miaka mitano-mitano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na hili suala tunalosema kwamba pesa zimepungua. Kwa kweli, nilichukua muda kuzungumza na wataalam wa Benki Kuu walichoniambia money in circulation zinaendana na uchumi na hakuna hata siku moja tumeweza kupungua bali siku zote pesa zinaongezeka. Ikabidi nipige kichwa niweze kufikiria ni kwa nini watu wanasema pesa zimepungua? Tofauti iliyopo sasa hivi na zamani ni kwamba kila hela unayoipata ni lazima uwe umeifanyia kazi. Siku za nyuma wakati mwingine hii magumashi zilikuwa nyingi tunapatapata hela ambazo tulikuwa hatuzifanyii kazi, tufanyeni kazi pesa tutapata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuunge mkono huu mpango kwa sababu wote tuliupitisha kama Mpango wa Miaka sasa umekuja katika mpango wa mwaka mmoja ili tuweze kufanya utekelezaji wake. Nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu kwa jinsi anavyotekeleza maana tukianza kufikiria wengine kabla hatujazaliwa reli iliyokuwepo ilijengwa na Mjerumani lakini kwa sasa hivi tunajenga reli hii wenyewe na tunaijenga sisi Watanzania kwa pesa zetu, hata kama tumekopa. Unaweza ukawa una hela zako kwa kukusanya kodi au unaweza ukawa na hela zako kwa kukopa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuangalia nini nikishauri Serikali ili tuweze kuweka tija zaidi katika uchumi wetu. La kwanza ni katika utekelezaji, je, ni namna gani tutaongeza money in circulation ndani yetu? Ni kweli tuna miradi mikubwa, kwa mfano, tuna ujenzi wa reli yetu, makampuni yanayojenga pale ni ya nje, malipo yatakayofanyika pesa zile zinaweza zikaenda nje, tulenge nini sasa? Kwa sababu Serikali ni moja, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Ardhi na watu wote, pale tunapokuwa tunamuajiri mkandarasi wa nje tuhakikishe kazi ambazo zinaweza zikafanywa na wakandarasi wa ndani, wapewe wakandarasi wa ndani ili wakilipwa hizo pesa zibaki hapa na ziende kwenye mzunguko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuangalie katika upande wa madini. Ukiangalia akina nani hasahasa wanaweza ku-contribute, ukiangalia mwenye mradi wa madini, asset kubwa aliyonayo ni madini yaliyopo chini, kinachofuatia ni ile pesa, kinachofuatia ni ule utaalam aliokuwanao. Sasa madini kama yana-contribute sehemu kubwa basi wenzetu wa Wizara ya Madini wawaangalie wachimbaji wadogowadogo na wachimbaji wa kati ambao ni Watanzania tuwawezeshe waweze kuchimba na hela nyingi zibaki katika maeneo yetu. Hicho ndicho ninachoweza kuishauri Serikali katika mpango wetu huu kwa ajili ya ku-make sure kwamba hizi pesa tunazozipata na huu uchumi mzuri ambao tunao sisi Watanzania leo hii unawafaidisha Watanzania hata kule Koromije. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuangalie sekta ya utalii. Niiombe Serikali iweke nguvu sana katika Shirika letu la Ndege la Tanzania. Watu wanazungumzia Shirika la Ndege la Tanzania lakini contribution yake huwezi ukajua itakuwaje pale litakapokuwa na nguvu. Kwa mfano, chukua jirani zetu wa Kenya, wanaruka moja kwa moja mpaka New York, wanaleta watalii moja kwa moja wao wenyewe. Nchi yetu kama itakuwa na Shirika la Ndege lenye uwezo na lenye nguvu watakaporuka mpaka pale Julius Nyerere International Airport kutakuwa na ndege nyingine itakayoruka kuwachukua watalii kuwapeleka Mwanza ambapo ni karibu na Serengeti. Watakapowafikisha pale Mwanza kutakuwa na mtu kutoka Koromije mwenye Pick-up yake, mwenye Landrover yake, atakayewabeba watalii na kuwapeleka Serengeti. Uchumi utakuwa umeshuka mpaka kwa mtu wa Koromije kule chini. Wasiojua ni wale wa upande huu, eleweni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mfano mzuri mmoja tu ambao watu wataweza kuona jinsi ambavyo pesa zitazidi kubaki hapa Tanzania. Kuna Kampuni ya ESTIM inayojenga barabara kutoka Ubungo mpaka nadhani Kibaha, ile ni kampuni ya Kitanzania na pesa zitakazopatikana pale nyingi zitabaki, lakini ukipita pale utafikiria ni kampuni ya nje, hamna tofauti. Kwa hivyo, niwaombe ndugu zangu waliokaa huku mbele, mliokaa huku mbele kidogo mlitambue hilo na mshirikiane na mimi nilikuwa nikikaa zamani, bado nyie ni wenzangu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie tena kusema Mtanzania anayependa nchi yake ataitumikia nchi yake mahali popote. Let me say this thing once and for all, I have never been in this House drunk, I will never do that and it will never happen. Mnaoendelea kusema hivyo, endeleeni na mtaendelea mpaka Yesu atakapokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa complement. Niendelee kuzungumzia kitu kingine ambacho ni cha muhimu sana kwa Taifa letu, ni hili tunalolizungumzia la Stieglers’ Gorge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, naunga mkono hoja.