Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nami fursa niweze kuchangia katika hotuba hii ya Wizara TAMISEMI. Kabla ya yote, kwanza nianze kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema ambaye ametupa nafasi na tumeweza kuamka salama na kufika ndani ya Ukumbi huu wa Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia namshukuru sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya katika nchi hii ya Tanzania; na amekuwa role model pia wa Marais wengine wa Afrika na nchi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pasipo kusahau, niendelee kuwashukuru Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa namna wanavyofanya kazi vizuri. Kipekee sana, nakushukuru sana kaka yangu, Mheshimiwa Jafo, Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI kwa kazi nzuri na kubwa unayoifanya, nawe ukiwa kijana, umekuwa role model pia kwa vijana wenzako. Tunakushukuru sana na pongezi, tumeona namna ambavyo



unapambana kila kona. Vilevile kwa kusaidiwa na wasaidizi wako; Naibu Mawaziri Mheshimiwa Kandege pamoja na Mheshimiwa Kakunda pasipo kuwasahau Watendaji wote wa Wizara hii TAMISEMI, kwa maana ya Katibu Mkuu - Engineer Iyombe, Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Zainab pamoja na wengine wote na Wakurugenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nijikite zaidi katika suala zima la TARURA. Kwanza naipongeza Serikali kwa kuanzisha chombo hiki cha TARURA. Kimekuwa msaada mkubwa sana kwetu Wabunge tunaotoka majimbo ya vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge wengi wamesema kwamba TARURA pamoja na kwamba imeanzishwa, lakini bajeti yake ni ndogo kwa maana ya kwamba ina urefu mpana zaidi na uchumi mwingi unatoka vijijini na malighafi nyingi zinatoka kule, lakini bajeti yake ni ndogo. Asilimia 30 kwa 70 kwa maana ya TANROADS, hii hakika hawataweza kufanya kazi yao na kufikia lengo tulilokusudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiomba Serikali yangu sikivu kwamba kama itaridhia kupitia Waziri Mpango baada ya kuleta bajeti yake ya Wizara ya Fedha, ingekuwa asilimia 50 kwa 50 tuna uhakika kwamba chombo hiki cha TARURA kitaweza kufanya kazi zake sawa sawa na vile ilivyokusudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo, kuna changamoto mbalimbali katika Jimbo langu la Busokelo. TARURA hii baada ya kuanzishwa mwaka 2017 tuna mahusiano mazuri sana na wale managers pamoja na coordinators wa Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mahusiano hayo, barabara ambazo ziko ndani ya Jimbo langu kwa mfumo ambao sasa hivi tuko nao ni kilometa 475 kupitia District Roads Management Systems (DROMAS) ambako ndiko zinakuwa updated barabara zote 475. Bajeti ambayo



Halmashauri yangu inapata ni shilingi milioni 600.6. Sasa unaweza ukapiga mahesabu hapo kwamba kilometa 475 kwa shilingi milion 606 siyo kitu. Kwa msingi huo, kwa bahati mbaya sana pia hizi fedha ambazo zilipangwa bajeti ya mwaka 2017/2018 hazijakwenda kama ilivyokusudiwa, kwa maana ya kwamba imekatwa nusu kwamba alipe madeni ya zamani kwa maana ya kwamba ile mipango ambayo tulikuwa tumepanga kwa barabara zote hadi hivi ninavyosema, haijaweza kutekelezeka kwa sababu fedha hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naliomba pia Bunge lako Tukufu kwamba kwa umoja wetu hii TARURA lazima ipewe fedha nyingi za kutosha. Zaidi pia katika hizi barabara, kuna barabara ambazo hadi sasa hivi ninavyozungumza, wananchi wangu wamenipigia simu tangu juzi, wengine jana kwamba kuna kata ambazo hakuna mawasiliano kabisa. Kuna Kata za Mpata, Isange, Kandete, Rufilyo na maeneo mengine mbalimbali ndani ya jimbo langu, hakuna mawasiliano kabisa kwa maana ya hizi mvua zinazonyesha sasa hivi kipindi hiki cha msimu wa mvua, kumekuwa na changamoto hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali yetu kwa sababu ni sikivu, wale managers wanapokuwa wanaomba fedha za dharura wapelekewe kwa haraka zaidi kwa sababu kunakuwa hakuna mawasiliano kabisa ya wale wananchi, maana wanaishi kama kisiwa. Wakiwa kama kisiwani maana yake hawawezi kufanya chochote. Ikumbukwe kwamba Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ile tunayoiita big four ambayo inazalisha sana raw materials pamoja na chakula katika nchi hii. Kwa hiyo, kama hakutakuwa na uwezekano wa kusafirisha mazao yanayozalishwa kule kuja mijini, maana yake hata huku mijini pia tutapata taabu kupata hayo mahitaji tunayohitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika jambo hilo hilo la TARURA, naiomba Serikali, kwa kuwa Mkoa wa Mbeya, hasa Wilaya za Rungwe, Chunya pamoja na Busokelo, zinapata mvua karibu mwaka mzima, zaidi ya milimita 2,000 kwa



mwaka, tungetamani sana kama suala la kutangaza zabuni kwa wakandarasi zingeanza mwezi wa saba na wa nane ili wa tisa mkandarasi aanze kufanya kazi na wa kumi awe kazini, wa kumi na moja amalizie kazi. Ingetusaidia zaidi, kuliko sasa hivi wakandarasi wengi wamekimbia site kwa sababu mvua zinanyesha usiku na mchana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kulizungumzia ni suala la afya. Afya ni uzima na roho. Kwa kweli kipekee sana Mheshimiwa Jaffo nikupongeze tena sana, niipongeze sana Serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi ambavyo mmejenga vituo vingi vya afya katika nchi hii ya Tanzania. Historia itandikwa kwamba kipindi fulani ndipo tulijenga vituo vingi vya afya. Hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo, nipongeze pia suala zima katika Halmashauri yangu ya Busokelo, nimeona mmetutengea bajeti ya shilingi 1,500,000,000 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya. Ninawashukuru sana katika jambo hili. Pia ikumbukwe kwamba katika maombi ambayo tuliomba, kuna kituo kimoja najua Mheshimiwa Jafo atakifanyia kazi, kinaitwa Isangi. Tulishaandikiwa barua na Mheshimiwa Waziri wa Afya, lakini hadi leo hii fedha hazijaingia. Ninaamini utalifuatilia na tutaweza kupata fedha hizi ili tuweze kuendelea kufanyia kazi hicho kituo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala zima la jengo la Halmashauri. Tunashukuru Halmashauri yetu mmeipa shilingi 2,300,000,000 kwa ajili ya kukamilisha jengo. Tunawashukuru sana katika jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie kuhusiana na suala zima la utumishi. Watumishi wetu katika Halmashauri ya Busokelo limekuwa na shida na changamoto kubwa. Tuna upungufu wa watu takribani 516 katika Halmashauri yetu, kwa maana Halmashauri ni changa na watumishi 516 ni wengi kwa maana hawapo kazini. Wengine ndio hao wamefukuzwa na wengine hawana vyeti. Kwa hiyo,



tunaiomba Serikali kwamba maombi maalum ambayo Mheshimiwa tulikupelekea uweze kuyafanyia kazi na bahati nzuri mzee wangu nilikupelekea uweze kuyafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, hatuna. Ofisi hii ilijengwa tangu mwaka 1930. Kwa maana hiyo, nazishukuru sana Kamati zote za Bunge ambazo zimepita pale, ninyi ni mashahidi. Kuna Kamati ya PAC, lakini pia Kamati ya Maendeleo na Huduma za Jamii, mmeona jengo lile kwamba limekuwa la miaka mingi. Tuiombe Serikali, tunajua kwenye mwaka huu hamjatenga fedha, lakini tukuombe Mheshimiwa Waziri kwamba mwakani tuweze kujenga Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikizingatiwa kwamba Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo pato lake la Taifa sasa hivi ni Mkoa wa pili baada ya Dar es Salaam. Kwa hiyo, ni vizuri tungeweza kuuboresha zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kuzungumzia ni suala zima la mifumo ya computer. Mimi nikiwa mdau, nimeona katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumzia mifumo mingi ya computer na wana mifumo mingi kweli kweli. Niwapongeze sana kwamba sasa nchi yetu inaenda katika digitali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningeweza kutoa mapendekezo ama maono kwa maana ya moja, mifumo hii mingi baadhi yake inatoka nchi za nje.