Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Juma Kombo Hamad

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Wingwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo naomba nilizungumze ni suala la ujenzi wa viwanda. Hakuna Mtanzania yeyote ambaye anakataa dhamira ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, lakini uchumi wetu wa viwanda ulenge pia kwa wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na maneno na yana ukweli kwa kiasi kikubwa sana kwamba, viwanda vinavyojengwa haviwalengi wananchi, viwanda vinavyojengwa havilengi kwenye Halmashauri na Wilaya ambazo zimejengwa. Leo hata kiwanda chenye thamani ndogo tu kikijengwa Serikali inaenda inachukua maeneo yote ya viwanda, inachukua tozo zote katika viwanda, hivyo nitoe ushauri tu kwamba, viwanda vinavyojengwa baadhi ya tozo katika viwanda hivyo, baadhi ya mapato katika viwanda hivyo ziendelee kubaki au tozo hizo au fedha hizo ziendelee kubaki kwenye Halmashauri husika.

Mheshimiwa Spika, vile viwanda vingekuwa na mgawanyiko, kukawa na viwanda vyenye viwango fulani ambavyo pengine ni viwanda vikubwa vikaenda moja kwa moja Serikalini, lakini viwanda vidogovidogo na viwanda vya kati pengine tungefikiria pato lake tukaliacha kwenye Halmashauri husika, ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kufaidika na viwanda ambavyo vinajengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye kitabu cha Mheshimiwa Dkt. Mpango, nafikiri kama sikosei ni ukurasa wa 16 amezungumza kwamba, Tanzania kwa mwaka inatoa wahitimu karibu laki nane, lakini akazungumza kwamba ajira Serikalini zinazowezekana tunatarajia kuajiri watu 40,000. Sasa angalia kwamba, leo tuna wahitimu laki nane, lakini Serikali ina uwezo wa kutoa ajira elfu arobaini tu, wapi na wapi? Watu elfu arobaini ni asilimia tano tu. Mheshimiwa Waziri wa Fedha hivi hajioni kwamba, ana-fail? Kama Watanzania wanaohitimu ni laki nane, hawa wengine waende wapi au wafanye nini?

Mheshimiwa Spika, ipo haja ya sasa Wizara ya Fedha na Serikali kwa jumla kukaa kutafakari hili. Mheshimiwa Mpango amekuja hapa na bajeti yake hii kwa mbwembwe sana, amekuja na mbwembwe nyingi, ving’ora na vitu vingine vingi. Katika bajeti ile Mheshimiwa Dkt. Mpango amekuja na maandiko mengi ya Biblia.

Mheshimiwa Spika, labda Mheshimiwa Waziri anajiandaa na yeye kuwa msaidizi wa kuongoza. Mimi naamini kwa maandiko aliyokuja nayo tunapata matumaini kimsingi kwa sababu, yupo mmoja katika viongozi wakubwa tu alisema anajiandaa kuwa msaidizi wa kuongoza malaika mbinguni.

Mheshimiwa Spika, sasa labda Mheshimiwa Dkt. Mpango na yeye anajiandaa sasa kuwa msaidizi wake. Sasa tuone basi kama ni hivyo, kama unataka kwenda mbinguni na una ndoto ya kuwa msaidizi wa kuongoza malaika mbinguni, basi hayo aliyoyaandika yatekeleze, Yesu hakuwa bahili. Toa fedha kwenye taasisi zinazogusa watu, toa fedha kwenye taasisi ambazo, Wizara ambazo zinagusa maisha ya watu, asitoe fedha kwa sababu ya kutaka kuonekana kajenga reli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, reli ni nzuri inagusa maslahi ya watu, lakini inagusa maslahi ya watu wachache, kuna sekta hapa zinagusa maslahi ya watu wengi, toa fedha. Naamini akija ku-wind up utakuja na maneno mazuri zaidi kuliko yale ambayo…

T A A R I F A . . .

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika, tumuombe Mheshimiwa Waziri kwamba, haya aliyoyaandika basi ayatekeleze na ayatekekele kwa vitendo bila upendeleo, bila hiyana na bila ubahili wa kutoa fedha, hususan fedha katika taasisi ambazo zinagusa watu kama vile kilimo, maji, ili bajeti inayokuja aje hapa azungumze vizuri zaidi kuliko vile ambavyo amekuja hapa.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni suala la Katiba Mpya. Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Nne ilileta mchakato wa Katiba. Katiba ambayo tulikuwa na matumaini ingekuwa ni suluhisho la matatizo ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ninalo lingine, ujumbe umefika kwamba bado Watanzania wana kiu ya kuona Tanzania inapata Katiba mpya. Kwa hiyo hili litambulike wazi kwamba bado hatujasahau kwamba fedha za Watanzania zilitumika nyingi na mchakato huu uli- cost muda wa watu wengi na muda wa taasisi nyingi, lakini baadaye ukawekwa pembeni. Kwa hiyo haja bado ipo.

Mheshimiwa Spika, nije kwenye suala la Deni la Taifa. Kila Mtanzania amekuwa akipiga kelele kwamba deni la taifa linakua kwa kiasi kikubwa sana. Serikali zetu hizi zinakuwa na matatizo, kwamba mpaka jambo litokee ndipo waone kwamba hili suala hili ni la kweli. Watanzania wamekuwa wakipiga kelele wengi wachambuzi wa bajeti hii hata wamekuwa wakisema sana wataalam wamekuwa wakisema sana, kwamba ukuaji wa deni la Taifa ambao unaloendelea sasa hauko salama kwa Watanzania na ni wazi kwamba hautaiacha salama Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ningemwomba tu Mheshimiwa Waziri Mpango awe na tahadhari na hili ili hatimaye mzigo huu asije akaubeba pekee yake kwa sababu mwishowe; Waswahili kule kwetu wanasema vyako vyako vyako na wenzio vikikupata ni vyako pekeo. Mheshimiwa Mpango mzigo huu iko siku utakuja kuelemewa peke yako. Kuna standard gauge inataka kujengwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru na siungi mkono hoja.