Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii kutoa mchango katika Wizara hii. Aidha, napenda kumpongeza Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika na kuiwasilisha hotuba hii kwa ufasaha mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii ya maliasili na Utalii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, nianze na vivutio cha utalii, napenda kuipongeza Serikali pamoja na Wizara hii kwa kuendelea kutilia mkazo namna ya kuboresha vivutio hivi vya utalii. Mazingira ya vivutio vyetu vinaonekana kuimarika na kuvutia watalii. Ushauri wangu katika suala hili kwa Serikali ni Wizara kwa jumla ni kuongeza vivutio hivyo na kuviweka katika hali ya kisasa zaidi. Aidha, ni vyema kuwe na vivutio vya namna tofauti katika maeneo yetu ya vivutio kwa mfano, ikiwa kivutio kingine kiwe na wanyama wa aina nyingine ili kuweka variety ya vivutio. Kutatua migogoro ya mipaka ya Hifadhi za Utalii.

Mheshimiwa Spika, hali ya migogoro katika nchi yetu imezidi kila siku. Naipongeza sana Wizara hii kwa kuchukua juhudi za kulishughulikia suala hili. Utaratibu wa kuwashirikisha wananchi walio katika maeneo husika ni jambo jema sana. Ushauri wangu katika suala hili ni kuzingatia kuwapa kipaumbele wakulima wa maeneo hayo ili kuendeleza kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa uchumi wetu hasa tunakoelekea kwenye siasa ya kujenga viwanda. Viwanda vinategemea sana kilimo kama rasilimali kubwa. Hivyo ni vyema Wizara ikazingatia suala la wakulima. Aidha, wananchi wa maeneo husika wewe wanapewa uhuru wa kuzungumza na kutoa maoni yao badala ya kushirikishwa kwenye mahudhurio tu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.