Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Haji Khatib Kai

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Micheweni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Awali ya yote nianze kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu siku ya leo kuweza kunifikisha katika Bunge hili Tukufu na mimi kuweza kutoa mchango wangu katika hoja iliyoko mbele yetu. Pia niwatakie rehema Waislam wote ambao wamekabiliwa na mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sekta ya Mifugo na Uvuvi ni sekta ambayo imekuwa ikibeba Watanzania wengi ambao wamekuwa wakijiajiri wenyewe ambapo Serikali imeshindwa kuwaajiri. Hata hivyo, pamoja na kujiajiri wenyewe Serikali imekuwa ikiwakwamisha kwa visingizio ambavyo wakati mwingine havina msingi wowote. Mwaka 1995 Serikali ilipiga marufuku uvuvi wa kokoro. Mwaka huohuo Serikali ikapitisha sheria ya ring net kuvua katika bahari kuu ambayo itakuwa ni kuanzia mita 50.

Mheshimiwa Naibu Spika, mita 50 za deep sea ni mita kubwa sana ni tofauti na uvuvi wa kokoro ambao wamekuwa wakivua maji ya kina kidogo. Hata hivyo, kwa masikitiko makubwa Serikali ambayo imepitisha sheria ya kwamba uvuvi wa ring net wavue kuanzia mita 50 wamekuwa wakiwazuia wavuvi hawa wa ring net kutumia chupa za oxygen ambazo zinaweza zikawawezesha kutumia upepo wa oxygen ili kuwasaidia katika uvuvi huo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uvuvi wa ring net ni uvuvi ambao hauna madhara yoyote. Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa kwa sababu uvuvi wa ring net hauna madhaa yoyote, lakini kupitia Wizara yake imepiga marufuku uvuvi wa ring net kwa sababu ambazo hazina msingi, kwa hivyo kama kuna matatizo yoyote au kama kuna tatizo lolote ambalo wameliona Wizara kwamba uvuvi wa ring net kwa kutumia chupa kuna matatizo, basi namwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa atueleze ni matatizo gani ambayo yanasababishwa na chupa ambazo wanaweza kutumia wavuvi wa ring net. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilimsikia Mheshimiwa Waziri akiwa hapa Bungeni akijibu swali la Mheshimiwa Maryam Msabaha ambaye alitaka kujua ni kero ngapi za Muungano hadi sasa zimetatuliwa. Mheshimiwa Waziri ambaye wakati huo alikuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira alisema kwamba kati ya kero za Muungano ambazo zimetatuliwa moja ni uvuvi katika ukanda wa Pwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni hivi karibuni tu wavuvi wangu wapatao 54 wakitokea nchini Kenya kwenye dago walikutana na meli ambayo inafanya patrol ya uvuvi haramu na ugaidi baada ya kupatikana wavuvi hao walisimamishwa wakaulizwa maswali na wakajibu na masuala waliyouliziwa ni kama yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ninyi ni nani, mnatoka wapi na mnakwenda wapi? Wavuvi hawa walijibu sisi ni Watanzania na ni wavuvi na tunatoka Dagoni Kenya. Hata hivyo, meli ile ambayo inafanya patrol ya uvuvi haramu na ugaidi ilitaka kujiridhisha kwamba kweli ninyi ni Watanzania na mnatoka Kenya. Wavuvi wale walitoa passport zao wakaonesha, lakini hiyo haikuwanusuru. Kwa masikitiko makubwa sana wavuvi hawa wakiwa maeneo ya Pemba kabisa, lakini waliambiwa watoke kwenye chombo chao na waliingizwa kwenye meli wakapelekwa Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwa sana kutoka Pemba na Tanga ni mbali sana, lakini hata hivyo wavuvi hawa waliwaomba kwamba ikiwa tunaomba kwa sababu tuko Pemba na vyombo vya ulinzi ni Muungano tunawaomba basi kama kuna tatizo, kama tumevunja sheria mtukabidhi vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo viko huko kama tumevunja sheria tuchukuliwe hatua. Pamoja na hayo, lakini walipelekwa Tanga wakiwa wamechoka sana na wakaenda wakadhalilishwa pale, zaidi ya wiki nzima wako Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Katibu Mkuu wa Wizara kwa kweli alinipa ushirikiano, tulisaidiana na kuhakiksha kwamba wavuvi wale hawabambikiziwi kesi nyingine. Kwa kweli nchi hii kama kuna watu ambao wamekuwa wakionewa ni wafugaji na wavuvi.