Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia kidogo kwa dadika hizi nilizopewa kwenye Wizara hii muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema kwamba kama kweli tunataka kwenda kwenye uchumi wa viwanda ambapo asilimia kubwa inategemea mazao ya kilimo, lazima Serikali kujidhatiti kikamilifu kwenye suala la kilimo. Ukiangalia dhamira tuliyonayo na ukiangalia tunakokwenda havioani! Hatuwezi kuwa tunaenda kwenye uchumi wa viwanda wakati huo huo kwenye kilimo tunawekeza kidogo, hatuwezi kwenda. Pia najiuliza swali pamoja na hicho kidogo tunachopa hiyo bajeti ndogo tu, Waziri umeweza kusimamia kipi kikaonekana kwa uhakika? Hicho kidogo tunachokipata, mimi naona tunalo tatizo la msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwenye utafiti, hatuwezi kwenda kwenye kilimo cha tija kama hatuna utafiti. Tulisema kwenye Bunge hili na imetengwa kwamba tuhakikishe kwenye bajeti ya Serikali tunatenga asilimia moja kwenda kwenye utafiti, leo ni karibu miaka kumi haiendi! Lini Serikali itafikia hatua ya kutoa one percent ya bajeti iende kwenye utafiti, hatuwezi kwenda huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna mazao mengi ndani ya nchi hii yana magonjwa sana kwa miaka zaidi ya 20 hayapatiwi ufumbuzi kwa sababu hatutoi fedha kwenda kwenye utafiti. Kuna mazao ya kilimo cha ndizi kule Bukoba hayaendi nje kwa sababa ya magonjwa hayaponi, tuna mazao ya mihogo, tuna machungwa yenye magonjwa, tuna maembe yenye magonjwa, tuna minazi hata vyuo vyetu vya utafiti hatuvipi uwezo viweze kutumia rasilimali zetu kwa ajili ya utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazalisha, kama hatuna uwezo wa kusafirisha mazao hayo nje tunazalisha kwa ajili ya nini, ukiona maembe yetu wakati wa maembe yanaoza, yanadodoka chini, ukiangalia mengi yana wadudu, kwa nini kwa miaka 10/15 tushindwe kuja na solution ya magonjwa yanayosumbua mazao yetu hatuwekezi? Kwa hiyo, kwanza kabla hatujaamua kuingia kwenye utafiti hatuwezi kutoka, tutalima lakini bado hatutavuna vizuri kwa sababu nguvu zinatumika nyingi za wananchi lakini bado hatutoi kwa tija wala haturuhusiwi kusafirisha nje kwa sababu ya udhaifu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni upatikanaji wa mbegu. Kwa miaka yote mpaka leo tunapozungumzia habari ya uchumi wa viwanda, bado tunazalisha mbegu ndani ya nchi kwa asilimia 20 peke yake, asilimia 80 tunatoa nje. Hii ni aibu kwa nchi ambayo asilimia 80 tunategemea kilimo ni aibu! Kwa hiyo, lazima Serikali ihakikishe kwamba inawekeza. Bahati mbaya hata mbegu hizi za nje bado siyo bora mimi mwenyewe nimejaribu mbegu za nje, lakini mbegu za ndani bado siyo nzuri watu tunaenda kwenye mbegu za nje sababu ndiyo zinazalisha vizuri. Kwa nini tunashindwa kujengea uwezo mamlaka zetu za ndani za mbegu zizalishe mbegu nzuri za kutosha na kwa bei nzuri, hili nalo ni tatizo kubwa sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo ukija hapa utuambie umefanya kazi gani kwa miaka ambayo umewekwa kwenye hiyo Wizara kuweze kumsaidia Mheshimiwa Rais kwenda anakotaka, uje utuambie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kilimo ni suala la mzunguko, kilimo ni mashambani, kilimo ni maghala, kilimo ni usafirishaji na kilimo ni masoko. Kama kwenye mashamba hatuwekezi vizuri, Waziri anazungumzia juu ya uagizaji wa mbolea kwa bulk na kwa urahisi. Nikuambie mbolea hizi haziji kwa wakati, hata bei zake hazieleweki wanasema kwamba ni bei elekezi siyo kweli. Wilaya ya Kaliua mwaka jana tumenunua mbolea mpaka shilingi 140,000 wakati bei elekezi ni shilingi 75,000, wengine shilingi 90,000, mahali pengine shilingi 100,000, shilingi 120,000, shilingi 140,000, bahati mbaya sana mbolea ya Serikali iliyokuja imekuja wakati tunavuna wakati ni mbolea ya kupandia, leo iko kwenye maghala haina kazi, kwa hiyo, liko tatizo la msingi Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuwa anafanya kazi kubwa sana kuisaidia Wizara hii. Kiukweli inapofika mahali panaonekana kitu, Mheshimiwa Waziri anafanya kazi kubwa hata kurekebisha zile AMCOS pamoja na ushirika wetu. Najiuliza swali kama Waziri Mkuu asingekuja Tabora kutusaidai WETCO leo angalau ina mabadiliko tungekuwa wapi na kwa nini Waziri Mkuu atoke alipo aje mpaka Tabora akaangalie kuna shida gani wakati Waziri yupo? Pengine Waziri hatoshi hili ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni muwazi lazima tuseme, Wizara hii inahitaji mtu ambaye ni very straight, very aggressive, mchapa kazi anayeweza kutusaidia tunakokwenda tuweze kufika, lakini kwa Waziri aliyepo naona kama tunalo tatizo ambalo inabidi Mheshimiwa Rais aliangalie kwa karibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima wa Mkoa wa Tabora tunalima tumbaku kwa kiasi kikubwa mwaka jana 2017 tumepa hasara ambayo haijawahi kutokea. Tumbaku yetu tani milioni tano imeuzwa kwa bei ya makinikia, bei ya makenikia kutoka bei elekezi dola mbili tumeuza dola 0.0... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)