Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangie machache juu ya Wizara hii ya Maji na Umwagiliaji.

Kwanza nitoe pole kwa Wizara hii nyeti sana kwa kuwa wanapewa fedha kidogo sana kwa ajili ya kusambaza maji. Kwa sababu hiyo, naomba kupendekeza kuwa Serikali ichukue hatua madhubuti ya kutenga fedha angalau si chini ya asilimia 60 ili kuondoa tatizo kubwa linalowakabili wananchi wengi hapa Tanzania. Nchi haiwezi kuwa ya uchumi wa kati wa viwanda kama hata maji nchi imeshindwa kupelekea wananchi wake. Ni wazi kwamba ukosefu wa maji unasababisha magonjwa ya milipuko na hivyo kuongeza matatizo ya wagonjwa kujazana hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili naishauri Wizara ya Maji na Umwagiliaji ianze kuweka takwimu sahihi za vyanzo vya maji ili ianze kuyatumia kikamilifu kabla ya kuchimba visima ambavyo baada ya muda mfupi vinakauka. Jimbo la Same Mashariki lina maji mengi ya mito, lakini maji yote yanaelekea baharini badala ya kupelekwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kufanya uamuzi mzuri wa kutenga fedha za upembuzi yakinifu na usanifu wa Bwawa la Yongoma. Mradi huu wa Bwawa la Yongoma utaweza kuinua uchumi kwa kiwango kikubwa katika vijiji vikubwa vya Ndungu, Misufini, Kalemawe na Makokane. Naamini baada ya upembuzi huu na usanifu mradi utatengewa fedha ili tupunguze matatizo ya maji kwenye Jimbo la Same Mashariki. Ahsante.