Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru wewe binafsi kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia kwa maandishi katika hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika na kuiwasilisha kwa umakini wa hali ya juu hotuba hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ni Shirika la Utangazaji Tanzania. Napenda kuipongeza Wizara kwa kuendelea kuliboresha Shirika hili la Utangazaji, ni shirika linalopiga hatua katika utangazaji. Ushauri wangu kwa Wizara, iendelee kutoa mafunzo kwa watendaji wa shirika hili ili kwenda na wakati. Bado kuna wafanyakazi hawaoneshi mabadiliko ya kiutendaji kutokana na pengine kukosa elimu na maelekezo ya kikazi. Mfano kwenye mavazi ya mtangazaji baadhi ya watangazaji hawaoneshi kuwa na elimu ya mavazi (dressing code). Aidha, naomba Wizara iboreshe usikivu katika maeneo ya vijijini, bado kuna maeneo ambayo usikivu sio mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, viwanja vya michezo. Bado viwanja vyetu nchini haviko vizuri. Tunaendelea na kuwa na viwanja vya kurithi, vya karne zilizopita. Ushauri wangu kwa Wizara ni kuboresha viwanja vya michezo ili viwe vivutio kwa wachezaji na wananchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.