Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Na mimi nichukue fursa hii kuwapongeza Mawaziri wote watatu wa TAMISEMI, pamoja na changamoto tulizonazo lakini unaiona ile sense ya utendaji kazi na kufika kwa haraka kwenye maeneo ambayo tunafanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hilo tutakuwa tunafanya makosa tusipowapongeza, hasa Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Selemani Jafo, amekuwa msikivu na anajitahidi, pamoja na kwamba vitendea kazi vinaweza visiwepo, lakini niwapongeze kwa ujumla wenu, pamoja na Mzee wangu, Mheshimiwa Kapteni Mkuchika katika eneo lake la mambo ya Utawala Bora ambalo mimi ndiyo nitajikita zaidi na nitakupa vidonge kidogo Mheshimiwa Kapteni Mkuchika kwenye eneo lako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi yetu suala la utawala bora, ambalo kwenye hotuba yake Mheshimiwa Kapteni Mkuchika, amegusagusa tu mambo mengine lakini mambo ya msingi hujayagusa. Ndugu zangu Taifa hili ni letu sote, kwa bahati mbaya kuna watu wengine wana notion kama Wapinzani ni intruders na kwamba kuwepo kwetu hapa ni kama fadhila fulani ambazo tunapewa na mtu fulani. Sisi hapa ni Watanzania halisi, hii ni nchi ya kwetu na tulifanya chaguzi, tumekuja hapa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunazo haki na Katiba yetu inaturuhusu kuwepo kwetu hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali iliyofikia kwa sasa hivi kwa mazingira ya utawala bora ni hali ya hovyohovyo sana katika nchi yetu. Tatizo kubwa katika Taifa letu tuna-embrace mind ndogo na tunapuuza big mind. Taifa ambalo halitaki big mind, watu wenye uelewa mkubwa hawatakiwi, watu wanaohoji, wanaodadisi hawatakiwi katika Taifa letu. Tukitaka kujenga Taifa lenye nguvu, lenye uchumi mpana ni lazima tuwe na hoja zinazokinzana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa na Bunge ambalo linapenda kushangilia vitu vya hovyohovyo na hii inatokana kwenye Taifa letu kunapofanyika promotion au appointment au placement kwenye eneo lolote, haitegemeani na merit. Unapomchagua Katibu Mkuu wa Wizara unamchagua kwa vigezo gani, unataka aka-add value gani? Unapomchagua Mkuu wa Mkoa unamchagua kwa kigezo gani, anaenda ku-add value gani kwenye ule Mkoa? Unapomchagua Mkuu wa Wilaya unamchagua kwa kigezo gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulilalamika wakati Serikali hii inaingia madarakani kwamba mmewatoa ma-DED waliokuwa wazuri, wanafanya kazi, wana weledi kwenye ofisi zao, wakaletwa watu ambao kwa sababu tu walivaa uniform za CCM, leo tumeona jinsi ambavyo Halmashauri zetu zinavyoshindwa kufanya kazi. Kumekuwa na nepotism ya hali ya juu sana, kumekuwa na upendeleo wa hali ya juu sana kwa sababu hawa wote wanaochaguliwa hawaendani na kazi walizopewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano ofisi ya Katibu Mkuu ni ofisi serious kabisa, unamwona mtu kama Profesa Kitila Mkumbo, badala ya kushughulikia na namna ya kumtua mama ndoo kichwani yeye amekazana anaandika kuwajibu Maaskofu ambao wanashughulika na roho za watu mitaani, badala ya kukaa kwenye ofisi haya ndiyo ninayosema mtu hajui anaenda kuongeza value gani na nimezungumza mambo ya placement haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unamchukua mtu kama Profesa Kitila anayezungumzia mambo ya elimu unampeleka kwenye mambo ya maji, anakaa ofisini badala ya kuzungumza mambo ya kumtua mama ndoo ambalo ni wazo zuri, yeye anakazana anataka amjibu Askofu kwa sababu ya mawazo waliyotoa kwamba hakuna demokrasia nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dola karibu milioni 500 za India zimerudi huko kwa sababu ya utendaji wa hovyo kabisa wa Serikali zetu…

KUHUSU UTARATIBU . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndiyo mambo ninayozungumza. Dada yangu namheshimu sana na ni Engineer huyu, anashindwa kuelewa, yaani anashindwa kuunganisha utawala bora ninaouzungumza na natoa kwa mifano. Sasa hizi ndiyo appointments ambazo zinatolewa, haelewi kabisa hapa ninapozungumza. Nimezungumza kuanzia uteuzi wa Katibu Mkuu, ukienda kwenye Wakuu wa Mikoa watu kama akina Mnyeti, anasimama kinyume kabisa na utaratibu wa sheria, Mkuu wa Mkoa kabisa anagawa kadi za Chama cha Mapinduzi barabarani. Mtumishi wa umma, tunazungumzia masuala ya utawala bora, anagawa kadi na anasema sitashirikiana na Wapinzani, halafu mtu kama huyu bado yuko kwenye ofisini, halafu mnakuja hapa mnasema kuna utawala bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, analipwa kodi ya nchi hii, halafu…

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna-embrace vitu vidogovidogo; huyu kijana mdogo, msomi, anashindwa kutofautisha kazi ya Mkuu wa Mkoa na kwenye vikao ndani ya Chama cha Mapinduzi, this is very sad, hawezi kuelewa tofauti hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu kama Mnyeti hapaswi kuwa kwenye ofisi ya Umma ya Serikali, mambo ya CCM akayafanye kwenye ofisi ya CCM huko. Unamchukua mtu kama Makonda, kila siku anaharibu, alianza madawa ya kulevya, leo…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

T A A R I F A . . .

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii hotuba ya Serikali imeandaliwa si chini ya miezi sita na haijaandaliwa na Waziri, imeandaliwa na timu kubwa, leo mnataka sisi tuandae kwa dakika moja kwa sababu mnaamini tunafanya mchezo hapa, nakupuuza wewe, sijui Daktari wa wapi wewe. Sasa narudi kwenye hoja yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tumekuwa tukiishauri Serikali hii na tutaendelea kuishauri. Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliwashauri juu ya makinikia ni aibu kubwa mkagonga ukuta kwa sababu ya utawala bora ambao hauendani. Tuliwashauri juu ya sukari, tuliwashauri juu ya Bombadia ni kwa sababu ya kuweka watu ambao hawaendani kwenye ofisi, hili ni suala la utawala bora ambalo nazungumiza. Leo mnakosa hoja hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunapozungumzia utawala bora, wengi hapa tunapozungumza tumekuwa tukishauri na ndiyo wajibu wetu, tumetoa ushauri mkapiga kelele hapa kwamba tutapewa trilioni 490 ziko wapi leo? Leo kuna watu wanapitapita hapa kuwaambia Wabunge wa CCM msizungumze masuala ya makinikia kwa sababu ni aibu, hakuna hela hizo. Akaja Dokta yule akawaambia atawapa hela, bilioni 300, ziko wapi? Mheshimiwa Dokta Mpango atuambie ziko wapi kwenye bajeti kwenye vyanzo vyake, kwenye mpango wake ziko wapi hizo hela za Acacia? Mambo yote yamekuwa ni aibu kwa sababu hamtaki ushauri na unakosekana utawala bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kipaumbele cha nchi hii ni kipi katika masuala ya utawala bora?

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie Mbunge; mama nataka nikwambie niko vizuri sana, kama mnataka suala la DNA niko vizuri, labda kama mnahitaji vitu vingine, napo niko vizuri kabisa, anayetaka kuja aje tu. Kama mnadhani hiyo ni kiki mnapoteza muda niko vizuri kabisa na nina watoto saba. Mawaziri wote tutawapima DNA humu ndani, si mnataka tupimane, haina shida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachozungumza ndiyo haya, tunaacha kuzungumza mambo ya maana tunazungumza mambo ya kipuuzi kwa sababu tuna-embrace akili ya kijingajinga, tunaacha kuzungumza mambo ya uchumi wa nchi hii unahangaika na DNA yangu, ya nini? Au unanitaka? Hapa we are talking about serious matters... (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza masuala ya uchumi katika nchi hii…

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza masuala ya barabara mbovu katika nchi hii, tunazungumza masuala ya utawala bora, watu wanakufa, watu wanauawa, unahangaika na DNA ya kwangu, haya ndiyo mambo ninayoyazungumza… Bunge ambalo linatakiwa…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa muda wako umekwisha, inatosha. Ahsante sana.