Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mungano na Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mungano na Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nikushukuru, ntakuwa mchoyo wa fadhila kama sikukushukuru kwa kupata nafasi hii. Niyakumbuke maneno ya Mheshimiwa Rais Mstaafu, Mheshimiwa Salmin Amour Juma, almaarufu Komando, alikuwa na maneno mawili akisema urafiki na nchi, kwanza nchi urafiki baadae.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa sijamtendea haki Mheshimiwa January Makamba, Waziri wa Wizara hii jinsi anavyojituma bila kujali mvua, jua, usiku au mchana, anapoitwa Zanzibar wakati wote anatii amri; nimpongeze sana Mheshimiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kitu cha kupendeza sana Wizara hii, hasa Naibu, angetoka angalau Zanzibar, ingeleta sura nzuri sana ya Muungano, ndiyo Wizara ya Muungano, ingeleta sura ya Muungano. Hata hivyo, siwezi kuingilia mamlaka ya Mheshimiwa Rais, nataka kujua nini Muungano, nini definition ya Muungano; what is union? Umuhimu wa kuungana watu, kuwa pamoja, kushirikiana katika nyanja mbalimbali kiuchumi, ulinzi, ajira, huu ndiyo Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini Muungano, definition yake ni hii; umuhimu wa kuungana watu kushirikiana, kuwa pamoja kiuchumi, nchi, ulinzi, ajira. Hata Tume ya Mheshimiwa Jaji Warioba ilisisitiza sana umuhimu wa Muungano huu kuwepo, katika watu 1,000 labda watu wawili watakataa Muungano huu kuwepo. Lakini kuna mambo muhimu au fomula gani ya kuendesha Muungano wetu huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Mheshimiwa Jaji Warioba haikukataa Muungano huu kuwepo, katika watu



1,000 labda watu wawili watakataa Muungano huu. Kwa hiyo Muungano huu tunauhitaji na ukizingatia keshokutwa, Mheshimiwa Machano amezungumza, tunatimiza miaka 54 ya Muungano wetu huu. Hata hivyo, kuna baadhi ya watu mnawalea vibaya, wanachafua Muungano huu bila kuwaonya. Tatizo tutafute formula ya kuendesha Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kupoteza muda, nije kwenye changamoto za Muungano, akiwemo Mheshimiwa Keissy. Ya nini kusema … (Kicheko)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

T A A R I F A . . .

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, narudia yaleyale, ni mzee wangu, adabu kitu cha bure, nitaendelea kumheshimu hata tukatoka nje. Mimi ni jirani yangu, nikianguka leo ataniokota yeye na akianguka leo nitamuokota mimi, sisi sote Waislamu, sisi ndugu moja lakini ukweli utabaki ukweli; moja moja mbili mbili, kavu kavu mbichi mbichi, mimi naendelea kukuheshimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye changamoto mwaka jana Mheshimiwa January alizungumza zimebaki changamoto tatu, nimpongeze. Hata hivyo, changamoto hizo mpaka leo nafikiri zipo ICU, hazijapata ufumbuzi, wanakaa vikao lakini zinafika mahali zinapata kigugumizi. Angalia Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ukurasa wa sita Sura ya Saba, vifungu 133 na 134, huu ndiyo mzizi wa fitna yetu ya Muungano, ni Joint Finance Commission, ukamaliza huu Muungano umekwisha, Mungu atuweke hai. Joint Finance Commission, Jamhuri ya Muungano Katiba 1977, nafikiri ukurasa wa sita, kifungu 133 na 134, huu ndiyo mzizi wa fitna uliobaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi wamezungumza humu katika mahali palipokuwa nidhamu yake siwezi kusema nzuri bandarini. Watu wamekuwa wanapata mpaka maradhi. Waziri wa Fedha hayupo hapa, Naibu Waziri ampelekee salamu Mheshimiwa Waziri. Huu Muungano tumeungana kwa nia njema, isiwe kama Lugha ya Kiarabu



ukiandika unavutia kwako tu, maandishi ya Kiarabu ukiandika unavutia kwako tu. Naibu Waziri wa Fedha, Waziri wa Fedha hayupo hapa, lakini mahali wanapoteseka watu, Mheshimiwa Tauhida kazungumza, mtu kavunja TV kwa uchungu, ule ni uchungu, tunaumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyabiashara Rais wetu tumemuona shahidi anawatetea wanyonge, anasimamisha misafara njiani kuwasikiliza wananchi, Wamachinga kaachia huru wafanye biashara. Leo mtu katoka Zanzibar, Zanzibar uchumi wake ukiacha karafuu ni biashara, tuwe wakweli. Imefika mahali kero hizi hazijafika mahali, double standard, VAT imekuwa kupita kiasi, tutaendelea kusema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kuna msemo usemao asemaye hachoki…

T A A R I F A . . .

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa aliyonipa nimeipokea kwa mikono miwili. Taarifa nzuri, taarifa ambayo inaleta sura ya Muungano wetu; nimshukuru sana Mheshimiwa Mattar kwa umakini wa hali hiyo. Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukizingatia kuna mambo matatu ya uchumi haya yako Tanzania Bara, sera za kodi ziko Tanzania Bara, sera ya sarafu iko Tanzania Bara. Hebu tufike mahali haya madogomadogo wenzetu mtuachie au tubadilishane, miaka mitano mchukue ninyi, miaka miwili tupeni sisi. Sera hizi muhimu, nyenzo hizi muhimu mnazo ninyi, Sarafu ya Tanzania, Benki Kuu, kodi hizi, mna mbuga nyingi za kuendesha, mna madini mengi. Zanzibar uchumi wake ni biashara, mambo madogo madogo haya ifike mahali… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.