Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya siasa nchini si nzuri kabisa. Vyama vingi vilianzishwa kwa Sheria No. 5 ya kuruhusu vyama vingi ndiyo maana hata chaguzi zote zinashirikisha vyama vingi, lakini katika chaguzi za marudio tumeona haki zikivunjwa na upendeleo wa wazi kwa Chama cha CCM. Kwa mfano uchaguzi wa marudio Jimbo la Siha askari polisi walikuwa wanawasindikiza CCM kukusanya maboksi ya kupigia kura.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haki haikutendeka, Mawakala wa Vyama vya Upinzani walikuwa wanapigwa na kunyang’anywa karatasi za matokeo mbele ya askari wa Jeshi la Polisi. Hii ilisababisha hata katika Jimbo la Kinondoni baadhi ya raia kupoteza maisha kwa sababu tu ya kutokutenda haki. Hivi kulikuwa na sababu gani zilizosababisha tume kutokutoa barua za mawakala kwa wakati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikutano ya hadhara. Nchi yoyote yenye kufuata sheria na inayoamini katika demokrasia ni lazima ifuate sheria maana Katiba, Ibara ya 18 inaruhusu uhuru wa kuongea na kujieleza lakini ni wazi kabisa wakati huu katika Serikali ya Awamu ya Tano, vyama vya siasa haviruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara, hata wananchi wakitoa mawazo yao kwenye mitandao wanashtakiwa na Serikali. Maandamano ambayo ni haki ya kikatiba kupeleka meseji kwa watawala yamekatazwa. Je, Serikali hii inaweza kusema ni nchi yenye kujali haki na demokrasia kwa wananchi wake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Makao Makuu Dodoma. Mpaka sasa juhudi kubwa bado zinahitajika kuuendeleza Mji wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi. Bado barabara nyingi hazipitiki. Kwa mfano maeneo ya Kisasa barabara ni mbovu sana. Kuna haja ya kushughulikia suala la majitaka, system iliyopo ilikuwa inahudumia watu wachache, sasa hivi idadi imeongezeka, la sivyo yaliyokuwa yanatokea Dar es Salaam kwa maji machafu kufurika ovyo barabarani yatatokea hapa Dodoma na kusababisha magonjwa ya mlipuko kama kuhara, typhoid na kipindipindu kutokea hapa. Je, Serikali ina mikakati gani ya kuongeza njia za majitaka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni sambamba na kuongeza shughuli za kijamii kuufanya Mji wa Dodoma kuwa kati ya miji ya vivutio kwa watalii. Kuna vivutio kama mashamba ya zabibu na miamba na mawe; mji utengenezwe uvutie watalii, hata Bunge lenyewe ni kivutio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kilomo. Wananchi zaidi ya asilimia 80 ni wakulima na wengi sana walihamasika kulima mahindi, lakini zao hili limekuwa ni mwiba kwa wakulima. Kama tujuavyo mbegu za mahindi ya kisasa huwa zinaharibika haraka sana na storage yake ni ghali sana na wakulima wengi hawawezi nunua matenki ya kuhifadhi. Bei ya mahindi imeshuka sana inapelekea mahindi kupekechwa na wakulima kupata hasara. Je, Serikali ina mikakati gani ya kuwasaidia wakulima hawa kupata masoko ya kuuza hata nje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanzo, mfano Kilimanjaro, ilikuwa haina shida kuuza mahindi Kenya, lakini sasa mpaka upate kibali na vibali vyenyewe kuvipata ni shida na imejaa urasimu mkubwa. Je, Serikali hainunui tena mahindi kwa ajili ya Ghala la Taifa