Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Juma Hamad Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ole

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba kuchukua fursa hii kukushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna siku nilifarijika sana katika Bunge hili ka Kumi na Moja ni siku ambapo Katibu Mkuu wetu Maalim Seif Sharif Hamad alituita kwenda kutuasa sisi Wabunge. Hiyo aliifanya baada ya kile kikao cha kuapa. Naomba ninukuu; alitueleza hivi:

“Mnapokuwa Bungeni jaribuni kuikosoa Serikali ili ifanye vizuri na mnapoikosoa, basi mkosoe kwa maana ya constructive criticisms kwamba muwashauri, kama hili halikufanyika vizuri, basi wafanye nini?” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili akasema, “mnapokuwa Bungeni pale ambapo Serikali inafanya vizuri, basi muisifu.” Huo ndiyo ulikuwa wasia wa Maalim Seif Sharif Hamad. Wenzangu wa CUF kama nasema uongo wanisimamishe hapa wanipe utaratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, Mama Lulida amesema, tuliapa na sisi wote ni waumini wa Mwenyezi Mungu. Tuliapa kwa kutumia Biblia na Quran kwamba tutaitumikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maslahi ya wananchi wetu ambao tumewawakilisha hapa. Kama hiyo haitoshi, kila siku hapa asubuhi tunasoma Dua ya kuliombea Bunge na kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Dua zetu za kila siku, maana nataka ninukuu kipande kidogo tu: “Ewe Mwenyezi Mungu, Muumba Mbingu na Ardhi, umeweka katika dunia yako hii au katika Ardhi yako hii Mabunge au Mabaraza ya kutunga sheria na Serikali za wanadamu ili haki itendeke kama upendavyo wewe Mwenyezi Mungu. Tunakuomba sisi Wajumbe wako utupe hekima na busara ili kujadili mambo yetu kadhaa, kadhaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka nijadili hii bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa mustakabali huu. Nafikiri ni vizuri kabla ya kujadili bajeti ya mwaka 2017/2018, tufanye tathmini ya bajeti iliyopita ili tujue what went wrong in the 2016/2017 budget, what are the challenges that we faced? Tukifanya hivyo tutakuwa tunaitendea mema bajeti ya 2017/2018. Bila hivyo, no, hatuitendei haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kubwa la bajeti ya mwaka 2016/2017 ni kuelekeza matumizi in such a way kwamba development budget tuitengee asilimia 40 na recurrent budget tuitengee asilimia 60. Sisi tulimpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Magufuli kwa sababu kwa mara ya kwanza anazungumzia maendeleo ya watu na huko nyuma ilikuwa chini ya asilimia 40. Sasa tuje kwenye ukurasa wa 30 wa budget speech ya Mheshimiwa Waziri. Naomba sana kama mna vitabu mfungue ukurasa wa 30. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 30 kwenye paragraph ya 41, sitaki nisome ile paragraph yote, lakini kwa ufupi anachosema hapa ni kwamba up to April, 2017 tumekusanya 20.03 trillion. Sasa hivyo kwamba tumeweza kutekeleza recurrent expenditure kwa asilimia 87.4 na tumetekeleza development expenditure kwa asilimia 38.5. Sasa Mheshimiwa Waziri waambie wataalam wako kule kwamba huku usifikiri Wabunge hawakusoma; sisi wengine tumeichambua neno kwa neno hotuba hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa if you add those two ingetufanya tupate 100 percent au tupate less than 100 percent kwa sababu hii ni mpaka Aprili lakini uki-add 87.4 percent na uka-add na 38.5 percent unapata 125.9 percent. Maana yake nini? Ni kwamba kile kilichokuwa kadirio kutumika katika bajeti hii, kimetumika na tumeongeza fedha nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye real na nominal terms; maana kuna wakati nilisema hapa, kuna vitu viwili; kuna kitu kinaitwa real terms and nominal terms. Is this budget real, ya 2016/2017? Is this real? Sasa nafikiri bajeti ya mwkaa 2016/2017 is not realistic. Angalau hii ya 2017/2018 now it is real, lakini angalau ni nzuri, it is healthier. Uki-compare bajeti mbili hizi; ya 2016/2017 na 2017/2018, hii bajeti ya sasa ni healthier kwa sababu imewalenga wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niishukuru sana Serikali kwa kubana matumizi, hilo wame-achieve vizuri, lazima tuwashukuru; lakini kwa maana ya mapato ambapo ndiyo msingi wa bajeti yote, bado tuna kazi kubwa. Nataka niwaambie, hakuna Serikali yoyote duniani inayoweza ku- survive bila tax revenue. Marekani imefika stage kwamba ikiwa wewe ni mgombea wa Urais kama ume-evade taxes, basi wanasema hufai kuwa Rais wa nchi hiyo. Kwa hiyo, naelewa umuhimu wa kukusanya kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka niseme, katika hili suala la kukusanya kodi kuna siri tatu; moja, collect taxes with minimum inconvenience to the tax payers; ya pili, kusanya kodi hizi rates za kodi ziwe affordable to the tax payers; lakini la tatu, kusanya kodi ili yule mlipa kodi aone kuna good returns katika maisha yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niipongeze Serikali; kwa maana ya minimum inconvenience to the tax payers Serikali imefanya vizuri sana. Tuna mifumo mbalimbali ya kielektroniki ambayo sasa hivi tunaitumia; juzi Kamati ya Bajeti tulikwenda kukagua ule mtambo wa TTMS ambao kwa kweli utawezesha kujua kodi za operators wa simu hawa on timely basis, lakini pia tuna mfumo pale katika Idara ya Forodha ambao unaitwa TANCIS; ni mfumo wa kielektroniki wa kujua ni nani aliyelipa kodi na wakati gani na kiasi gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ni kwamba ule Mfumo wa TANCIS bado ni TRA ndiyo imekuwa nao, lakini kuna wadau wengine ambao wanapaswa kukusanya kodi kwa niaba ya TRA, ule mfumo hawana. Nadhani ni vizuri tuishauri Serikali hapa kwamba wale wadau wengine nao wa-adhere to that TANCIS system.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niende haraka haraka. Kama kuna kitu ambacho kimesahaulika katika bajeti hii ya 2017/2018 ni suala la utalii. Mapato yatokanayo na utalii sasa hivi ndiyo mapato makubwa kwa maana ya foreign exchange tunayo-earn. Nafikiri kama sikosei, asilimia 17.5 ya mapato yetu ya nje yanatokana na utalii. Wenzetu wa Kenya wamechukua comperative advantage; wakati sisi tulikubaliana wote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwamba tutoze VAT, wao hawakutoza. Kwa hiyo, bei ya mtalii kuja Tanzania sasa hivi imekuwa ghali sana kuliko kwenda Hija. Tunakosa watalii wengi na huenda baada ya muda mdogo sana tukakuta mapato yetu yana-decline kabisa katika Sekta hii ya Utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tuna comperative advantage ukilinganisha na Kenya. Over the years kuanzia 2011 mpaka sasa hivi namba ya watalii in Kenya inapungua, sisi huku inaongezeka na inategemewa kwamba mwaka unaokuja namba ya watalii itakuwa kama milioni moja na kitu in Kenya na milioni moja na kitu hapa kwetu. Kwa hiyo, kama tutajipanga vizuri, tutaondoa kodi hii VAT on tourism, basi nina uhakika tuna uwezo wa kukusanya mapato zaidi ya Kenya. Kwa hiyo, naiomba Serikali inapokuja na Finance Bill iliangalie suala… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)