Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Mwaka wa 2017/2018. Nataka kujikita katika maeneo machache na hasa nikiangalia maeneo ya kipaumbele katika mwaka huu wa 2017/2018. Viko vinne, lakini nitataja viwili tu. Kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, hiyo nakubali; kufunganisha uchumi na maendeleo ya watu; hapo ndipo ninapoona tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mahali ambapo kuna wananchi wengi ambao ndiyo wanataka focus yetu iangalie ni vijijini kwenye sekta kubwa inayoajiri wananchi wengi, ambayo ni Sekta ya Kilimo. Nilikuwa najiuliza, hivi bila kuweka kipaumbele katika kilimo, mifugo na uvuvi, tunafunganishaje uchumi na maendeleo ya watu? Kwani watu wengi wako katika sekta hiyo ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mwaka huu unaoishia 2016/2017, kilimo kilipata shilingi bilioni 3.369 sawa na asilimia 3.31; mifugo na uvuvi walipata shilingi bilioni 1.2 sawa na asilimia nane tu ya fedha iliyoidhinishwa na Bunge. Sasa tunaposema kilimo ndiyo uti wa mgongo wa nchi yetu ambao inachangia asilimia 28 katika maendeleo ya nchi yetu, Iweje basi asilimia 96.69 haikuidhinishwa, badala yake wamepewa asilimia 3.3 tu? Hivi kweli Sekta hii ya viwanda itakuaje kama hatuunganishi na malighafi kutoka kwenye kilimo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naona kwamba mambo yetu yako mismatch kwamba hatu-focus kwamba kama kweli tunataka viwanda na kama tunataka kuondoa umaskini, lazima concentration yetu iwe katika kilimo, ambapo kule ndiyo kuna wananchi wengi. Kule ndiko kuna maskini wengi na kwa ajili hiyo tukiongeza thamani kwenye mazao yao, kwenye viwanda tutakuwa tumewasaidia wananchi wetu kwa sehemu kubwa katika kuondoa umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia sekta nyingine ya Wizara ya Maliasili na Utalii, hii ni Sekta ambayo pia inachangia asilimia 25 (mnaweza kunisahihisha) katika uchumi wetu. Nayo ilipewa shilingi milioni 156.6 sawa na asilimia nane ya fedha walizoomba. Sasa hii ina maana kwamba asilimia 92 ya pesa yote waliyoomba hawakupata. Sasa ninachojiuliza, kama hata Sekta hii ya Utalii ambapo Balozi wa Marekani aliyekuwa Black American wakati ule hapa nchini, alisema, Tanzania hii kwa utalii wake tu kama wangeweka emphasis kwenye utalii, sisi tungetoka Marekani kuja kuomba msaada katika nchi hii. Sisi tunapuuzia zile sehemu ambazo ndizo zinachangia katika uchumi wetu kukua haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli kuweka barabara na reli ni kitu kizuri na ninakiunga mkono, lakini tuwe focused kwamba reli inaenda kuchukua nini kwa mfano Mwanza? Je, kilimo cha pamba tumekitilia mkazo? Je, viwanda vinavyowekwa ni vya kutengeneza nguo ili tuongeze thamani katika pamba zile au tunaweka huku kiwanda, usafiri unawekwa pengine na maji yanawekwa pengine? Sasa huu uchumi wetu wa Tanzania na huu umasikini tunauondoaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, najiuliza, maajabu gani tutakayopata sasa hivi kwenye kodi ambayo tutatoka kwenye ile shilingi trilioni 29 tuingie shilingi trilioni 31.7? Tunakusanya vitu gani? Pesa zinatoka wapi? Ukiangalia, hata hii tunayosema tuchukue kodi ya nyumba ambazo hata hazikuthaminiwa, kwa kweli ni maajabu sana. Kwanza itakuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu maskini, kwamba juu ya shida walizonazo vijijini, bado tuwaongezee mzigo ambao wanatakiwa walipe Sh.10,000/= kwa kibanda cha mbavu za mbwa! Hii kweli mimi siioni ni sawa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilitegemea kwamba aidha bajeti yetu ibaki ile ile, tu- address ule upungufu wote ambao kwa mwaka huu unaoisha hatukuweza kuufikia au ipungue ili tuwe very realistic, tuseme kwamba tutafanya kazi kwa pesa ambayo tunayo. Mfadhili akileta itakuwa bonus. Sisi tuna-assume kwamba hawa wafadhili watatuletea tu au tutapata mikopo as a result tunaweka bajeti kubwa ambayo mwisho wa siku tunarudi kusema ooh, bajeti ya maendeleo ilitekelezwa kwa asilimia
38. Ni aibu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, tukiingia kwenye hii kodi ya mafuta ya taa, kwa kweli mimi hili siliungi mkono kabisa. Mafuta ya taa ndiyo nishati kubwa sana vijijini, especially ukingalia kwa mama zetu wengi ndio wapishi, wengi hasa wa mjini pia, wanatumia haya majiko ya kichina ambayo yanatumia mafuta ya taa. Sasa hivi hapa kwenye Bunge lako tunaambiwa mkaa unakatazwa, kuni zinakatazwa, tusikate miti; kuna mwenzetu alisema sasa hivi tunaleta gesi. Hivi ana habari gesi hii miaka saba mpaka kumi ijayo ndiyo itaweza kuingia majumbani kwetu kwa kutumia mitungi? Ana habari hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hawa akinamama maskini vijijini, wakae miaka saba mpaka kumi wakingojea gesi? Mimi nafikiri hii kodi ya mafuta ya taa tuiondoe ili wanawake wengi ambao ndio wapishi; vibatari huko vijijini ndiyo vinatumia mafuta ya taa, tuwasamehe katika kuongeza hiyo Sh.40/= kwenye mafuta ya taa. Kwa hiyo, nasema kama hii bajeti kweli inajali maskini, nasema hii Sh.40/= itolewe kwenye mafuta ya taa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maji. Nashauri ianzishwe agency ya maji vijijini, maana tumeshaona pesa nyingi za maji zinakwenda kwenye maji ya mijini na kutokana na audit report ya CAG imeshaonesha kwamba kuna ubadhirifu mkubwa sana katika hii miradi ya maji ya mijini. Kwa hiyo, sioni kwa nini maji bado yaendelee kuwekwa mjini badala ya kupelekwa vijijini. Kwa hiyo, nashauri kwamba angalau asilimia 70 ya bajeti ya maji ipelekwe vijijini ili kusudi akinamama tuwatue ndoo vichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ajira, kweli hii inashangaza sana. Kama hatutatilia mkazo ajira na ukiangalia standard za ILO, tuzungumzie gainful employment, tusizungumzie tu ajira, maana ajira tunaambiwa mbona mashambani watu wanaajiriwa wengi, ardhi yetu ni kubwa! Tuangalie gainful employment, watu wapate kipato kutokana na ajira zile. Hapa katika mpango huu sioni mahali ajira ilipowekewa msisitizo. Kwa maana hiyo ni kwamba, tutatoa wanafunzi wengi wanaomaliza Vyuo Vikuu, wanamaliza VETA na maeneo mbalimbali ambao watakuwa mijini. Katika uzee wetu tutakuta wanatuingilia mpaka majumbani. Tunatengeneza majambazi wengi ambao kesho hatutaishi kwa amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema kabisa tungeangalia kwamba ajira zetu tunaziwekaje ili tuone tuna- create vipi ajira hii? Hii kusema kila mtu aanzishe viwanda, hiyo siyo practical. Viwanda vina systems zake, siyo kwamba mimi kila leo nikiamka naenda kuanzisha kiwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza uangalie mtaji unapata wapi? Kiwanda cha aina gani? Hata hicho kiwanda ukianzisha ume-import material. Vipuri unatoa wapi? Soko lako liko wapi? Ni kitu kikubwa ambacho kingetakiwa Serikali ibainishe yale maeneo muhimu ambayo tunasema tukianzisha kiwanda hiki, kitaajiri wananchi wangapi na material yake yatatokana na kilimo, tuta-add value na tuta- export wapi ili tupate ajira na tupate fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zetu za maendeleo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nasema bado sijaridhika kwamba uchumi wetu… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji