Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika taarifa ya shughuli za Kamati hii. Aidha, napenda kuwapongeza Wajumbe wa Kamati wote kwa kuandaa na kuiwasilisha kwa umakini kabisa taarifa hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia taarifa hii napenda kuchangia yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa usambazaji umeme vijijini; napenda kuwapongeza Serikali yetu kwa hatua na spidi nzuri ya kuwapelekea wananchi wa vijijini huduma hii. Umeme kwa sasa sio tena luxury ila ni kitu muhimu kwa maendeleo ya nchi hii na wananchi. Hata hivyo, bado inaonekana kuwa kasi ya usambazaji umeme haiendi sawa na kasi ya matumizi au uungaji wa huduma hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu katika suala hili Serikali iendelee kuwaelimisha wananchi wa vijijini umuhimu wa huduma. Ni vyema vikaundwa vikundi vya kitaalam na kuwezeshwa ili waweze kwenda vijijini kuwaelimisha wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ni vyema kukawa na msamaha wa gharama za kuunga umeme kwa wateja wa awali ili kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi wananchi wa vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.