Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tano, okay, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kwanza kabisa na kwa umuhimu, nimetumwa na wafanyabiashara wa Mbeya kuja kuiambia Serikali kwamba wanaiomba Serikali kwa level ya Mheshimiwa Waziri waende Mbeya mkae nao kikao kwa ajili ya kujadili masuala ya ulipaji kodi. Kwa sababu kumekuwa na vikwazo vingi sana kiasi kwamba Mbeya tunashindwa kuzalisha wafanyabiashara mabilionea wa kutosha kama ilivyokuwa kwenye majiji mengine ikiwemo Dar es Salaam, Arusha na Mwanza kutokana na sintofahamu zinazotokana na TRA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani unakuta mtu ana-declear labda mapato mwaka huu shilingi milioni kumi, mwakani ana declear milioni kumi again, mwaka unaofuata watatu aki declear milioni 30 wana back date wanamlazimisha kwamba wewe ulidanganya itakuwa hata kwa miaka mitatu, minne yote ulikuwa unaingiza milioni 30. Kwa hiyo, wana impose kinguvu kodi tofauti na mapato ambayo yule mfanyabiashara ame-declear. Hili ni tatizo kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango mfanyabiashara wa Mbeya akijenga nyumba nzuri inakuwa na madhara kwa sababu wanaenda ku double kodi kwenye biashara yake kwamba ulipata wapi hizi hela za kujengea hii nyumba. Ndio maana Mbeya tumechelewa kuwa mansion na mpaka leo hatuana mansion yako machache machache ndio kwanza yanaanza ukifananisha na majiji mengine na hii haiwezekani kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hii inasababisha wafanyabiashara wakifikia lengo level fulani ya mtaji inabidi wahame Mbeya waende kwenye miji mingine ili waweze kupata ustawi wa kibishara, lakini wakikaa Mbeya inakuwa migogoro na watu wa TRA.

Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri kwa level ya Waziri wafanyabiashara wa jiji la Mbeya wamenituma kwamba wanataka wanahitaji uende mkakae ili mjadiliane na haya mambo kwa sababu yamekuwa hivi maiaka nenda miaka rudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bajeti, naunga mkono maoni ya upinzani, kodi ikiwa kero inachotakiwa ni kuiondoa sio kuibadilisha kiujanja ujanja kama mlivyofanya kwenye masuala ya road licence kupeleka kwenye mafuta kiasi kwamba unawapa mzigo wananchi ambao wengine hawana magari kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni sahihi kwa mujibu wa Kambi ya Upinzani fedha hii ipelekwe katika maeneo hii shilingi 40 kama inalazimika kuongeza shilingi 40 kwa kila lita basi twende tuipeleke kwenye maji. Tukimaliza maji twendwe kwenye miundombinu ya elimu; yaani tunafanya vitu kwa miaka kwa series, miaka mitano maji, miaka mitano tunakuja kwenye miundombinu ya elimu ikiwepo nyumba za walimu na hata vyoo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa katika Bunge hili na Taifa hili viongozi wakubwa wa Serikali wanazungumzia masuala ya kununua nini hizi boeing mpya jetliner sijui ziende wapi, lakini wanafunzi wetu wa shule za msingi hawana vyoo, wanakunya nje. Kwa hiyo hivi vitu vidogo vidogo ndio tunatakiwa tuviangalie kwanza kabla hatujaangalia mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu madini na mimi nasema mikataba iletwe si ya madini tu, madini, gesi mikataba ya kununua ndege bombardier, nyumba za Serikali zilizouzwa mikataba yote iletwe ndani ya Bunge hili ili tuipitie upya. Tukisema mnasema tunampinga Rais hatumpingi tuko tayari kumsaidia na kumshauri lakini kwa sharti moja kama mimi binfsi Mjumbe wa Kamati Kuu sitaki uteuzi. Sitaki u-DC, sitaki sijui Ukuu wa Mkoa, sitaki Uwaziri ninachotaka afanye Mheshimiwa Rais ni kufungua mijadala atuache atusikilize mawazo yetu na ayafanyie, kazi hicho ndio kitu kibwa tunachokifanya, yaani sisi tunaweza tukamsaidia vizuri Mheshimiwa Rais tukiwa huku kuliko kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kirimanjaro au kuwa Katibu Mkuu wa Wizara fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunamuomba sana Mheshimiwa Rais achie mijadala tujadili vyanzo vya matatizo kwa kina, asitubane, hata kama matatizo hayo yatakuwa yamesababishwa na watu ambao sasa hivi ni Marais wastaafu wacha tujadili, ambaye yuko clean atabaki kuwa clean ambaye ana mawaa basi Sheria itachukua mkondo wake ili tutengeneze presidence kama inavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mwisho katika hizi dakika tano ni chache nikupongeze Dkt. Mpango, Mwakajoka amekuchana kiutendaji kazi, lakini mimi kwa tabia una-smile kidogo sasa hivi. (Makofi/Kicheko)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)