Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Kazi za Ubaharia wa Shirika la Kazi Duniani na Azimio la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Mabaharia Na. 185 wa Mwaka 2003 wa Shirika la Kazi Duniani.

Hon. Machano Othman Said

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Kazi za Ubaharia wa Shirika la Kazi Duniani na Azimio la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Mabaharia Na. 185 wa Mwaka 2003 wa Shirika la Kazi Duniani.

MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote naomba niishukuru Serikali kwa kuleta Azimio hili la kuridhia Mkataba wa kazi wa Mabaharia, Mheshimiwa muda ni mchache sana, kwa hivyo nitazungumza kwa haya mambo mafupi tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, imekuwa ni kawaida kwa Tanzania kutohudhuria vikao vingi vya IMO na pia Shirika la Kazi Duniani kuhusu Mabaharia. Bahati nzuri nchi yetu ina bahari kubwa na ina fursa nyingi sana katika eneo hili, kwa hiyo naomba Serikali isidharau. Mimi mwenyewe nilishawahi kuhudhuria vikao kama vinne vya IMO lakini upande wa Bara hawakushiriki.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, tukiridhia Azimio hili la mkataba huu tutanufaika sana, kwa sababu tuchukulie mfano Zanzibar kwa kupitia mamlaka ya usafiri baharini wamesajili meli karibu 400 duniani na kila meli sasa hivi wanatozwa dola 500 kwa sababu bado Tanzania hatujaridhia mkataba huu na kiasi kama dola 200,000 kila mwaka zinalipwa na ZMA kwa ajili ya suala hili. (Makofi)



Mheshimiwa Naibu Spika, sasa leo nafurahi kwamba Serikali inaridhia itatuwezesha Tanzania kwa ujumla kuongeza idadi ya Mabaharia lakini pia kutoa fursa nyingi za ajira kwa vijana wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili la ubaharia ni eneo pana sana na linaweza kutusaidia. Bahati nzuri Tanzania tuna vyuo viwili vinavyotambulika duniani, tuna Chuo cha DANAUSE kiko Zanzibar na tuna chuo cha DMI Dar es Salaam. Vyuo hivi wanatoa certificate na zinatambulika na vinatoa ajira kwa vijana wetu. Kwa hivyo niiombe Serikali kwamba ni wakati muafaka sasa tuseme kwamba tumechelewa kidogo, lakini maadam leo limeletwa hakuna tatizo, nafikiri Waheshimiwa Wabunge wote tutaridhia na sisi ili kuwezesha nchi yetu isonge mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo, naomba nimalizie hapo.