Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nami niweze kuchangia Itifaki hii naomba nianze na hii Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimejaribu kuipitia vizuri na nimeilewa ni nzuri. Sisi kama nchi tunapaswa kuiridhia lakini kuna mambo machache ningetaka niseme, kwamba kuna nchi zimejiunga na zingine hazijajiunga na kwa kuwa Itifaki hii lengo lake ni kutatua migogoro ndani na nje ya nchi wanachama, kuzuia mauaji ya kimbari, kupambana na ugaidi, kupambana na uharamia na kadhalika ni jambo zuri sana. Hata hivyo, nchi hizi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaongozwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi zao na Katiba hizi zimetoa haki kadha wa kadha, lakini unakuta katika nchi hizi, viongozi ambao wako madarakani wanaamua kukanyaga Katiba ya nchi hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Katiba imetoa fursa ya demokrasia, Katiba imetoa fursa ya uhuru wa mawazo, Katiba imetoa fursa ya uhuru wa kujieleza, Vyama vya Siasa na kadhalika, anatokea mtu anakwenda kinyume na Katiba, huyu mtu siyo gaidi? Kwa hiyo, gaidi siyo wale wa kuvamia peke yake ni pamoja na viongozi wanaokwenda kinyume na Katiba ya nchi, wanaokwenda kinyume na sheria ya nchi. Kwa hiyo, nimefurahi kuona hii Itifaki kwamba pamoja na wale wanaozuia vyama vya siasa visifanye mikutano kwa mujibu wa sheria itawashughulikia, nimefurahi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ni vizuri mfahamu kwamba, amani siku zote ni tunda la haki. Kama viongozi wa nchi hizi ambao wako madarakani hawataki kutenda haki, hakutakuwepo na amani, ni vizuri tufahamu Muasisi wa amani ni Mungu mwenyewe. Kama viongozi wa nchi hizi ambao wako madarakani wanawaona wananchi wenzao hawana haki ambayo haki imetolewa kwa mujibu wa Katiba, Mungu atawahukumu siku moja na namshukuru Mungu ameanza kuwahukumu wengine leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi kama Mheshimiwa Ryoba ninaikubali hii Itifaki iko sawa sawa, Bunge liridhie ili wale viongozi wanaokwenda kinyume na Katiba ya nchi, kuzuia vyama vya siasa visifanye mikutano kwa mujibu wa sheria waweze kushughulikiwa na umoja huu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

T A A R I F A . . .

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika, huyu mtu hata hajasoma Kanuni, kwanza hajui Kanuni, lakini la pili hii Itifaki inaongelea amani na ukisoma ndani yake kuna kuzuia ugaidi, mauaji ya kimbari, nini source ya mauaji ya Kimbari? Ni Viongozi walio madarakani kutokutenda haki. Fuatilia kule Rwanda na Burundi nini kilitokea? Viongozi waliokuwa madarakani hawakutenda haki. Msipotenda haki kunaweza kukatokea mauaji ya kimbari, kwa hiyo ni vizuri haki itendeke ili watu wote wawe na amani. Msipofanya hivyo haina maana, ndiyo maana nikasema hii ni nzuri sana, kwa sababu itawazuia wale viongozi ambao hawatendi haki kwa wenzao. (Makofi)

Jambo lingine nilitaka niongelee hii Commission ya pamoja ya Bonde la Mto Songwe. Pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu ametoa tahadhari hapa kwa sheria iliyopitishwa. Pia niungane naye kwamba ni vizuri jambo hili liangaliwe vizuri ingawa maudhui ya Itifaki hii ni mazuri sana kwa sababu jambo hili kimsingi lilitakiwa lifanyike muda mrefu sana kwa ajili ya kutoa manufaa kwa wananchi wa maeneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo pia mabonde mengi sana, kuna Bonde la Mto Rufiji, kuna Bonde la Mto Mara na Mabonde mengine ambayo kama mabwawa yangetengenezwa, kilimo cha umwagiliaji kikafanyika, wananchi wa maeneo husika wangepata faida kubwa sana. Kwa hiyo, pamoja na weakness za kisheria ambazo zimeonekana, ambazo naamini kupitia Bunge hili mtazipitia mkaangalia nini kinaweza kufanyika ili Commission hii iweze kutekelezwa, lakini kimsingi maudhui yake ni mazuri lakini angalizo kubwa ni mgogoro wa mpaka.