Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji

MHE. MARWA R. CHACHA: Naomba nianze na hii ya ukurasa wa 173. Mheshimiwa Waziri kwanza nichukue nafasi hii nikupongeze wewe na Naibu wako, kwa kweli ni moja ya Mawaziri ambao mnajitahidi ila shida tu ni kwamba hamna hela, kwahiyo hapa hata tukiwaadhibu hakuna lolote. Sasa mimi niwashawishi Wabunge kwamba wakubali, wasikubali Wizara ya Fedha ile shilingi 50 iongezeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Maji, hatuwezi kufanya hadithi hapa ya kuwafurahisha wananchi huko nje, lakini sisi Wajumbe wa Kamati ya Maji hukio ndani ndiyo tunafahamu uhalisia wa shida ya maji nchi hii sasa hiyo iongezeke, Mheshimiwa Waziri wewe furahi hiyo lazima iongezeke.

Sasa nilitaka wakati mnakuja kujibu Mheshimiwa Waziri hebu nisaidie, kwenye ukurasa wa 173 Mji wa Mugumu kwenye usambazaji wa maji kuna hizi fedha bilions almost 19 kutoka Serikali ya India. Nataka kujua na wananchi wa Serengeti wa Mugumu wanataka kujua ni lini zinakuja ili kazi ya usambazaji wa maji ianze, maana ile ya uchujio inaendelea vizuri na nikushukuru sana kwa kusukuma naona Yule mkandarasi anakwenda speed kweli kweli Mungu akubariki sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme moja tu, kwamba kuna hii Programu ya Maji Vijijini vimechimbwa visima vingi lakini wananchi wetu wa vijijini hawawezi kuendesha kwa kutumia majenereta na hata maeneo mengine ambayo yana umeme bado wnanachi wetu wanakuwa ni shida kuendesha miradi hii. Kwa hiyo mimi ningeomba Mheshimiwa Waziri kama jinsi tulivyoenda Shinyanga tukaona ule mradi wa Maganzo wanatumia solar, wanatumia na zile prepaid meter, naomba Wizara ichukue jukumu la kuhakikisha ya kwamba, miradi ya maji vijijini wanatumia umeme wa jua katika uzalishaji wa maji, hilo ni la msingi sana bila hivyo hii miradi itakuwa hapa tu na haifanyi kazi yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine ni kwenye umwagiliaji, unapokuja ku-wind up niambie mabwawa ya umwagiliaji ya maji ambayo tayari yamekwishatumia fedha za Serikali ya Bugerera kule Nata, Nyamitita kule kata ya Ling’wani, Mesaga kule kata ya Kenyamonta nataka kujua progress yake ikoje? Kwa hiyo, unapokuja ku-wind up note that, ninahitaji kusikia na wananchi wa Serengeti wanahitaji kusikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambi lingine nilitaka niseme, ukiangalia Sera ya Maji ya Namibia, wao kwenye sera yao wanaita Water For Survival. Wanatenga asilimia 60 ya bajeti yao kwa ajili ya maji kwa nini? Maji ndiyo chakula, bila maji hatuwezi kupata mazao ya chakula, leo Tanzania kila kona wananchi wanalia njaa. Lakini kama tungelikuwa na kilimo cha umwagiliaji kila kona naamini kungekuwepo na chakula cha kutosha; lakini leo tunalia. Ukiangalia kwenye takwimu maeneo ambayo ardhi inatumika kwa ajili umwagiliaji ni sehemu ndogo sana.

Kwa hiyo, mimi ningependekeza kwamba kwenye bajeti zinazokuja, kama kweli tunahitaji kufanya mapinduzi ya viwanda katika Taifa hili ni lazima tuwekeze kwenye miradi ya maji ya umwagiliaji. Kama hatuwezi kuwekeza kwenye miradi ya maji ya umwagiliaji hayo mapinduzi ya viwanda sijui viwanda vya namna gani, labda viwanda vya kuchomelea.