Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Hon. Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naunga mkono hoja. Changamoto tuliyonayo kubwa inayokabili viwanda nchini ni pamoja na ukosefu wa mitaji na teknolojia ya uzalishaji kupitwa na wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto nyingine kubwa ni kutokuwa na uhakika wa umeme na maji ambayo inafanya viwanda vyetu kutoimarika, hivyo nashauri kuwa ili viwanda viimarike nchini, Serikali ihakikishe umeme na maji vimepatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa na mwenendo usioridhisha kutoa fedha za miradi ya maendeleo, hivyo kuchelewesha utekelezaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali iangalie namna bora ya kuiwezesha Benki ya Rasilimali Tanzania (Tanzania Investment Bank) ili ifungue matawi mikoani hasa Mkoa wa Kagera, hatua ambavyo itasaidia mikopo kuwafikia Watanzania walio wengi. Kuna changamoto ya kukosekana kwa soko kwa baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa nchini kwa sababu ya kukosa ubora unaotokana na gharama za uzalishaji kuwa juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Ongezeko la Thamani (VAT), hususan kwa wawekezaji wa viwanda vya madawa ya kilimo na mifugo kutozwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), unapunguza ushindani wa bidhaa zinazoingia nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali iboreshe Kiwanda cha Kagera Sugar ili kiweze kutoa sukari kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya Watanzania hasa waliopo Mkoa wa Kagera.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Kagera Sugar kipo Mkoani Kagera, lakini wananchi hawanufaiki na kiwanda hicho kwa sababu sukari inakuwa ni ya bei ya juu sana. Hivyo, naiomba Serikali iweze kutusaidia wananchi wa Kagera kupata sukari kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeongeza ugumu katika hatua ya kuanzisha biashara kwa kuongeza tozo za usajili. Jambo hili linaathiri juhudi za kuongeza ajira kwa vijana. Pia inafanya wajasiriamali wasifanye shughuli rasmi za kuingiza mapato ya Serikali na kupunguza ajira zitokanazo na biashara rasmi.